Wengi wetu hatufahamu uhusiano kati ya Oman na Zanzibar/Mombasa/Kilwa Na Pwani hii ya Mashariki..wengi tunafundishwa kuwa Wa Oman walikuja kutawala Znz Na pwani yake....Tukumbuke Wa Oman walifika Znz kitambo kwa biashara na Makaazi ya kawaida. Zile Pepo za bahari ziitwazo Moonson zilianza hata kabla ya Yesu...visiwa hivyi na pwani hii ilikua tayari imeshavuka na kufikia dunia nyengine.
Tusome Makala hii ambayo ni nadra kwa vijana wa leo kusomeshwa mashuleni na tumekua wavivu wa kusoma na kufanya tafiti za maana . Tumekua tukiamini kama
Pasco anavo amini propaganda za kisonge kuhusu kufagia kwa matiti...
tuone vipi wa Oman walifika mashariki na kuhamia Znz nz Mombasa..namna gani walisaidia kuondoa ukoloni wa kireno walotawala Znz kwa miaka 200. Wareno walifanya ushenzi na hujuma kubwa na mateso lakini haya husomeshwi shule ..kwani tume chaguliwa ya kufundishwa ..
Lakini moja walo liacha Pemba ni Mchezo kufukuzana Na Ngombe !
Uvamizi Zanzibar Msumbiji na kilwa mombasa na Mogadishu na Wareno
Wareno waliivamia Oman na Zanzibar katika karne ya kumi na sita 16.
lakini baadaye wa Omani walifanikiwa kujikomboa kutoka kwa wareno Ukombozi wa Omani ndio ulioleta tija ya kukombolewa kwa zanzibar, kwani ni wa Oman hawa hawa ndio walioikomboa zanzibar Oman ilivamiwa mwaka 1508.
Chini ya Aifonso Albuqueque ambaye aliishambulia Sohar, Maskat, na karyat na kuziweka chini ya Himaya yake wakati Zanzibar Unguja ,ilivamiwa mwaka 1503. chini ya Lawrenco Ravasco na baadaye ilishambuliwa pemba na Francisco da Seixas De'Cabrera.kama ilivyokuwa Kilwa ilivamiwa Fransisco De Almeida akishiriana na vasco Da Gama Mwaka 1505,)
kushambuliwa Unguja kuanzia mwaka 1503 Unguja ilishambuliwa Miezi Miwili Mfululizo na Wareno chini ya Laurenso ravasco hata ilipofika mwaka 1508, Don Duarte Delemos, Gavana Wa Kireno Nchini Ethiopia Alifika Unguja ili kukusanya Kodi, akakataliwa
watu wa Unguja wakapambana Kiume wakishirikiana na wenzao kutoka visiwavywa Pemba na katika mwaka 1631 Francisco de sexas Cabreira alipiga Bomu kasri ya Malkia Mwana wa Mwana na kuifukia kama ilivyopigwa bomu Kiilwa na bagamoyo.
Malkia Mwana wa Mwana alikimbilia na kuhamia Yenen na hakufanikiwa kurudi tena Mpaka Umauti ulipomfika akiwa Jiddah Saud Arabia Mwaka 1638.)
Kasri yake wakaivamia Wareno na kuifanya kuwa kanisa dogo la mwanzo, lakini baadaye kanisa hilo lilivunjwa na I mamu Seif wa Oman alipokuja kuikomboa Zanzibar ' ngome kongwe ndio ilokuwa ikulu ya Malkia Mwana wa mwana hapo zamani ,
katika Unguja baada ya tukio hilo watu wengi sana walikimbilia Oman ili kwenda kujipanga vizuri na kufundishwa mbinu na kupambana na mreno, mwaka 1632 Yusuf bin hassan bin Ahmed kutoka pemba aliishambulia ngome ya Wareno Mombasa,
kushambuliwa pemba kwamara ya mwanzo,kwa mujibu wa waraka wa Jamba Ngome ulioandikwa mwaka 1606 na Mmoja kati ya wazee wa pemba chini ya usimamizi maelekezo wa Sharif bin yusuf bin burhan
waraka huo ulikutwa katikati ya Msahafu (Qur an) na Shekh Theniya bin Khalfan ambaye aliupiga Copy nakala kisha ukatafsiriwa kwa kiingereza na Shekh Abdur rahman bin muhammad bin Jidawy wa kahkama kuu ya Zanzibar na kuhifadhiwa katika makumbusho ya taifa ya beitul Aman. waraka huo unasema hivi,
Baada ya Francico De sexas Cbreira kuivamia Pemba akiwa na kisoni bin jojo ambaye aliingia pemba na meli tano na wanavita wa msalaba wa kireno kutaka kulipwa kodi.
wenyeji wa pemba walikusanyika pamoja na maalimu Juma bin kombo na kiongozi wa pemba akasema tazama hapa wewe kisoni hatutakupa chochote,hatukujui wewe ni nani? sisi sio watumwa wako, kwanza wewe ni nani?
kwa sababu hii kisoni akatangaza Vita lakini wenyeji wa pemba wakapambana kwa muda wa siku 32 kisoni akashindwa kwa mshikamano huo akakimbia na kuondoka katika mwaka 1652, kisoni alirudi tena na meli 65 za wana vita kudai kodi kutoka kwa wenyeji wa pemba lakini walikataa kata kata na walipigana kwa muda wa siku 60, waliua Wareno 1304 na wenyeji 364 walikufa mashahidi, Kisoni hakupata kitu akarudi na watu wake,'
katika mwaka 1656. Kisoni alikuja na Meli 70 za kijeshi zikatua Ras-Mkumbuu zikajipanga kwa mapambano ya siku saba wenyeji wa pemba walijikusanya kutoka kona zote za pemba,ilikuwa ni maadalizi ya kujitolea muhanga zidi ya wareno kufa kupona,
wakati kisoni alipotaka kodi majlis Shura iliyowajumuisha maalimu juma kombo Shsme bin ali, Mfalme haruna bin hassan bin ali na Mwinyi bin Sharif bin Qutb bin mahaz Al Baalawy ,
maalim juma kombo alimwambia Kisoni tumekubaliana kwamba hatukulipi kodi yoyote Kisoni akasema Mkubali msikubali Mtalipa kodi kama kawaida maalim akasema hatuogopi sieee'...
Waraka unaendelea kusema kuwa mwisho walikubaliana kiujanja kuwa watalipa Dirham 12000 na baadaye wataongeza Dirham 16000, lakini zitaanza kulipwa mwaka utakaofuatia
waraka huo unabaini kuwa walifanya hivyo ili bwana kisoni aondoke wapate kujipanga zaidi kwa mapambano, na alipoondoka walisoma Ahlal badri kumuomba mwenyezi mungu kwa tawasul ya watu waliopigana vita vya badr ndani ya wakati mgumu wa mwezi wa Ramadhan...pamoja na nyiradi mbanimbali
husemwa kuwa hiyo ndio dua iliyoombwa kuwa asipatikane Mzanzibar yeyote kuritadi kutoka katika Uislamu ikiwa ataritadi apatwe na madhara na hii imetokezea mara nyingi katika vizazi vya zanzibar,
Mwisho ilishambuliwa pemba na wareno kutamalaki Hollings Worth anahitimisha kwa kusema
hakuna shaka yeyote wala ubishi kkkkwamba wareno walikuwa na hamu kubwa ya ajabu kuhakikisha kuwa wanausambaratisha Utawala wa kiislamu na Ustaarabu wake katika kisiwa cha pemba
na katika Mwaka 1651 Oman ikiongozwa na imamu nasir bin murshid al yaaroud ambapo alifanikiwa kuukomboa Mji wa ormuz mwaka 1622 na Mwanawe imam seif ibm nasir ibn murshid alyaarod alifakiwa kuwatowa kabisa wareno katika mwaka 1631/
Lakini zanzibar ilikaa chini ya Utawala wa kireno tena mpaka mwaka 1696 baada ya kushindwa kwa majaribio mengi ya kutaka kujikomboa, yaani mwaka 1585 waliposaidiwa tena na Utawala wa Uturuki Ottoman Empire/ na kupitia kwa Shambulizi kubwa alilofanya yusuf Ahmed mwaka 1630 ambalo halikuzaa matunda/
Lakini ilipokombolewa Oman mwaka 1632 ndio Chachu ya kukombolewa kwa Zanzibar kwani machifu wa kizanzibar kutoka tumbatu na peeemba wakishirikiana na watu wa Kilwa
waliteua wajumbe kwenda Oman jahazi lilichogwa chwaka Uguja nakwenda kukutana Imam seif ili afanye Ukombozi wa kuwasaiidia zanzibar nae alikubali pale alipokusanya majeshi na kutangaza vita dhidi ya mreno kuanzia mwaka 1696-1698 alipofanikiwa kuikamata Ngome kuu ya mombasa
wakati huo zanzibar katika kasr ya Fatma na Mwinyi Mkuu tayari wareno walishajenga kanisa digo ndani ya ngome kogwe , unaweza kuyaona makombora aliyotumia Imam seif kumtowa mreno yamewekwa mbele ya ndome hiyo kogwe na sasa mengine mbele wa forodhani ikiwa kama kumbukumbu ya tukui hilo,
baada ya kumaliza kuikomboa Zanzibar Imamu seif bin murshid alikuwa tayari kuyarejesha majeshi yake nyumbani kwake oman kama walivyofanya waturuki Ottoman Empire mwaka 1585. lakini Wazanzibar walijikushanya nakuweka shura ya kukubaliana kwamba majesshi ya oman yasirudi kwanza
hivyo kwa kuhofia kwamba wareno watarudi kama walivyorudi mwaka 1586 baada ya waturuki Ottoman empire''walivyorudi kwao, walimsihi imamu sei ayabakishe majeshi yake hapo na washirikiane katika Uamuzi wa zanzibar hivyo basi imamu seif alikubali tena maombi ya ndugu zake katika iman akabakisha majeshi yake hapo, bali akiwa oman aliteua magavana mbali mbali wenye kufanya kazi katika mwambao wa Africa mashariki kupitia Zanzibar na pia wapo Wazanzibar waliteuliwa kwenda kufanya kazi oman chini ya mashirikiano hayo,.
kadhalika alianza kuitumikia zanzibar kwa misaada kuendeleza kilimo bora cha minazi ni yeye ndio aliyeanzisha ukarabati wa njia na kuttawenya visima vywa maji safi na kufanya rutuba iliyowezesha zao la minazi na miti mingine
imamu seif alifariki mwaka 1711, akateuliwa imam seif II kushika Uimamu, lakini naye alifariki mwaka 1728)
akaja Inan said ibn Ahmed ibn ssultan ibn said al Busaid
(sayyid said)
Uchaguzi wa mwaka 1741ulimuweka madarakani imam Ahmed bin said bin sultan al busaid Ambaye naye alishika Uimamu yeye alibadili mfumo wa Utawala na kuwateua magavana (maliwali) wapya na huko mombasa ambayo ilikuwa chini ya uliwali wa Mazrui na huko pate walikuwa ma- al harth
katika mwaka 1746 imam Ahmed alimteua Addullah bin Djad kuwa Liwali Mpya wa Zanzibar, na mombasa na pate,ndipo mazrui wa mambasa na ma-al harth wa pate walipokataa na kujitangazia utawala wao (mombasa Sheikhdom)
katika mwaka 184 sayyd said alikamata madaraka ya Oman na Zanzibar kwa taratibu za kisheria kwa mujibu wa dhehebu lake la ibadhi ni yeye aliyefanikiwa kuumaliza mzozo wa mombasa na pate lakini baadaye mwaka 1826 aliwapa tena indhar
wakati yote yanatendeka mwinyi mkuu wa zanzibar Hassan ambaye ndio Mtawala wa kienyeji aliyewakaribisha wa- Oman zanzibar akimsihi sana sayyid said bora ahamishe makao makuu kuyatoa Oman aje kuishi zanzibar ili ijengeke kama makao makuu au mji mkuu sayyid said hakufanya khiyana aliitikia wito wa nduguye katika iman hatimaye mwaka 1833 alianza kuikarabati Ngome kongwe na 1840 kuhamia ambapo mwanzo aliitumia Mwinyi Mkuu mara baada ya kuondoka wareno
john middleton na jane Campbell wanalezea vizuri tukio hilo la kiungwana kinyume na wale wanaosema sayyid said amekuja kuteka nchi ya zanzibar
sayyid said bin sultan hakuwa ni mwenye kuteka lakini kuitikia wito wa ndugu zake wa iman
Ndio hapo ukaimbwa wimbo wa kibuzi buzi, kuwa ni fumbo la kuimbwa na watoto kueleza
(Njama za kwenda manga omaaan uitwae fumo mkuki na Upanga huku sinba mreno karegea karegea kongwe Mzee hajiwezi)''
mwinyi Mkuu akajenga dunga bweni na kuhamia huko ili kumpisha sayyid said.
mwinyyi mkuu wa zanzibar hassan bin sultan bin Alawy Mtoto wa Mwinyi Mkuu wa kwanza kuhamia hapa Unguja alikuwa Mfalme mwwwaka 1710... na mwinyi mkuu hassan bin Ahmed ndie wa kwanza kuhamia Dunga, kaskazini ya dunga Bweni akimpisha Sayyid said bin sultan mjini,.
kwani fahari wawili hawakai zizi moja ingawa akija sana Mjini kumtembelea na wakisikilizana na akipendwa sana na wananchi mpaka Nyimbo ya kkumbembelezea Mtoto ikimbwa kwa jina lake
karatasi nakupeleka
kwa Mfalme Hassani
na fimbo ya Henzirani,
makosa niliyokosa
nina muombeazi kweani,
Mwombezi wangu nyota
na baraka ramadhani...'''
Lakini pia viongozi hawa walikuwa ni viongo muhimu katika baraza la mawaziri wa sayyid said
Tuwashukuru wa Oman kwa kuwatoa Wareno..
askari wa Malkia baada ya vita ya saa dakika 38.....
View attachment 341277