Mkuu Maalim
Mohamed Said
, chuki na Waislamu itoke wapi, hata hawa Waarabu niliowaandika hapa, sina chuki nao kabisa!, kwa taarifa tuu, mke wangu wangu mkubwa ni Mwislamu!, nilipoanza anza kazi RTD, nilipikwa na safu ya Watangazaji mahiri wote Waislamu, Suleiman Hegga, Abdul Ngarawa, Ahamed Jongo, Salim Seif Mkamba, Juma Ngodae, Ahamad Kipozi, Sekioni Kitojo, Salama Mfamao, Siwatu Luanda etc, niwachukie kwa lipi?!.
Nipoanza kazi, nilipangishwa nyumba ya Mwislamu pale Ilala Sharif Shamba, Mwajuma Mchuka wa ATC, nikiishi na Muislamu Aboubakar Liongo, nilikuwa napikiwa kwa Da Mwajuma, mwaka mzima na mwezi Mtukufu nilifunga, kanzu na kofia hadi leo ninavaa!. Alipohama kuamia Masaki, Mdogo wake Halima Mchuka (RIP) aliendelea kutuhudumia hadi ... sasa niwe na chuki na Waislamu za nini?!.
Nilipoondoka RTD, niliajiiwa DTV, waajiri wangu ni Waislamu watupu na Waarabu, Nilipoondoka DTV, nilitunza na kulelewa na Sheikh Jabir, nimefanyiwa mema mengi na Waarabu/Waislamu!. Japo mimi ni Mkristo Mkatoliki lakini naukubali sana Uislamu, hapa nilipo nina wake 3 bado mmoja nitimize nguzo!. Kwenye hoja ya mahakama ya kadhi, nimewatolea hoja muruwa kuhusu ufumbuzi wake kulikoni hata nyinyi Waislamu wenyewe, hebu kanisome hapa, kweli mtu mwenye kuuchukia Uislamu anaweza kutoa ushauri kama huu,
Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu?.
Kuna tatizo la baadhi ya Waislamu waliofilisika kuusianisha Uislamu na Uarabu!, hivyo ukizungumziwa udhalimu wa Waarabu, wao wanatafsii ni udhalimu wa Waislamu!. Udhalimu ni udhalimu, hauna dini , rangi, wala kabila!. Kama hoja ni Lugha ya Kiarabu, hata Nabii Issa Bin Maryam, alizungumza Kiarabu.
Mada hapa ni kuhusu unyama wa Waarabu waliowafanyia babu zetu!, sasa ili kuupunguza unyama wa Waarabu, sasa ndio unatuletea unyama mkubwa zaidi ya huo wa Waarabu, ili sote kwa pamoja tuseme, afadhali ya Waarabu?!, kama Spaniards nao ni wanyama kuliko Waarabu, na unyama waliofanyia Latin America?, pandisha uzi wake, tutachangia!. Uzii huu ni kuhusu unyama wa Waarabu!.
Pasco