Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Hii topic tu hapo juu ni enough kukuondoa katika watu waliokua na akili timam.
Wacha waarabu kuuliwa hadhani kama paka, mwisho Karume alianza kuwauwa wasomi wote.
Kina Abdul Aziz Twala, Othman Sharif, Mohamed Hamoud, Saleh Sadala, Abdallah Kassim Hanga, Mdungi Ussi, na wengine wengi.

Uliza historia, hao hapo juu wamefanya nini na wamekufa vipi? Maana hata makaburi yao hayapo.
Thank you for the useful information.
 
Narejea ktk maelezo yangu ya awali.
Na ningependa Unijibu km nilivyokuuliza. Historia ilioandikwa na Mzungu huyo huyo inasema KABLA YA 1807 legislation Ndani ya Miaka 300. wazungu walifanikiwa KUBEBA WATUMWA WA KIAFRIKA ZAIDI YA 12,000,000 kutoka Pwani ya East africa na Savannah area of Africa (which includes countries such as Mali, Niger, Chad and Sudan) and the Horn of Africa (which covers Djibouti, Somalia and Ethiopia).

Sasa Swali ni kwamba! Je MZUNGU Hapa HAKUHUSIKA HATTA KIDOGO ktk BIASHARA HII ya WATUMWA WA Huko EAST AFRICA Including ZANZIBAR?

Nadhani wewe ni Mswahili km mimi ktk matumizi ya Lugha. Na neno "KUHUSIKA" nina imani maana yake unaijua.
Ntakupa mfano hai hapa.

During the second half of the 18th century, France opened up larger sugar plantations on the islands of Reunion, Mauritius and in the Indian Ocean. na Hapa WAFANYAKAZI WOTE Walikuwa WATUMWA WA KIAFRIKA.

Mfano wa Pili.

Je! Umeshawahi Kumsoma Napoleon 1 of France ktk Mswada wa Sheria alioupitisha Mwaka 1802 kuhusu UHALALI WA WATUMWA?
Baada ya Hapo NINI KILIWATOKEA WAZEE WETU wa EAST AFRICA?

Sasa Naomba Jibu lenye USHAHIDI na udadavuzi ulio wazi. Sio Jibu la Mitaani.
Mkuu naomba nikurekebishe kwenye modern slavery wahabeshi,wasomali na sudan wenye light skini hawakupelekwa utumwani naomba kutoa hoja
 
Wee Baragashi, ulikuwepo kuyashuhudia hayo au umehadithiwa?!. Mimi nakiri sikuwepo ila sijahadithiwa bali nimesikiliza mimi mwenyewe shududa wa Mapinduzi yale Matukufu, yalivyorudisha hishma kwa visiwa vile, yena ili kuondoa ubaguzi, wamatumbi wakawao Waarabu kinguvu!.Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa, Walikimbia Wenyewe!.

Nimemsikia aliyepindua akisema hakuna Mwarabu alyefukuzwa Zanzibar, walioomdoka, waliondoka wenyewe bila yoyote kutimuliwa!. Kwa taarifa tuu, hata ASP wapo waliopote maisha!.

Pasco
PASCO
Nadhani kuanzia leo unite kaka na uniheshimu.

Mapinduzi na unyama wake nimeushuhudia kwa macho yangu, sikuhadithiwa. Nakumbuka waziwazi alipouliwa Inspector Sketi(?) na mkewe kwa mapanga mapolisi wazalendo kuwekewa vigogo vya mnazi kifuani, na wamakonde wakiwa na mishale wakiranda mitaani kuwaambia watu wawafichue mahizbu waliowaficha wapelekwe ( rahaleo) kituo cha madhila kilichowakusanya (mateka) wa hizbu na chachandu(ZPPP)

ASP waliopoteza maisha kwa ajili ya Mapinduzi ni wachache sana, hata kumi hawafiki! Uliza yalipo makaburi ya waasisi wa Mapinduzi. Yalikuwa ni mauaji ya upande mmoja. Ninachojua kuwa ASP wa Zanzibar waliwahifadhi wanachama wa hizbu wasiuawe na " wakombozi" kutoka bara na nchi jirani.

Ule uwanja wa Kibanda maiti uliobatizwa jina la uwanja wa demokrasia ndio una " mass graves" za wazanzibari waliouwawa Mapinduzi kwa kosa moja tu la kuwa wanachama wa ZNP/ZPPP. Tuombe mungu tu atusmehe madhambi yetu.

Mimi nimeshudia uhuru na hata kushiriki kumuaga Gavana Sir. George Mooring pale Forodhani ikishushwa bendera ya Union Jack na kupandishwa Bendera rasmi ya watu wa Zanzibar na Gavana akaingia kwenye meli ya Uingereza, huku mkewe akilia kama mtoto kuondoka Zanzibar ( yenye neema). Mimi sasa ni mzee( lakini si kikongwe)
 
Wengi wetu hatufahamu uhusiano kati ya Oman na Zanzibar/Mombasa/Kilwa Na Pwani hii ya Mashariki..wengi tunafundishwa kuwa Wa Oman walikuja kutawala Znz Na pwani yake....Tukumbuke Wa Oman walifika Znz kitambo kwa biashara na Makaazi ya kawaida.
Tuwashukuru wa Oman kwa kuwatoa Wareno..
View attachment 341277
Mkuu Crabat ukisikia ilmu ndio hii, uzi wako huu umenifundisha mengi ambayo sikuyajua na miongoni mwa haya ni kuwa kumbe Sultan Said Sayyid alipohamisha makao makuu ya sultanate yake toka Oman na kuyahamishia Zanzibar ile mwaka 1832, hakuivamia Zanzibar bali alikaibishwa na mtawala wa Zanzibar aliyeitwa Mwinyi Mkuu!. Wajerumani na Waingereza, Wabelgiji, Wareno, Wataliano, Wahispania, etc kila wakishika maeneo, waliingia mikata na wenyeji, hivyo lazima kuna mkataba Mwinyi Mkuu aliingia na Waarabu kuitawala Zanzibar, hata kama sio mkataba wa maandishi, lakini there must be something, haiwezekani Mwenyeji ampishe tuu mgeni!, kwa mujibu wa bandiko lako, sababu kuu ya Wenyeji wa Zanzibar chini ya Mwinyi Mkuu, kuwakaribisha Waarabu Zanzibar, ni ulinzi wa visiwa hivyo visivamiwe tena na Wareno!.

Hivyo basi pia kuna uwezekano Mwinyi Mkuu aliwaeleza uzao wake, hivyo tishio la uvamizi wa Wareno lilipoisha kabisa, wajukuu wa Mwinyi Mkuu wakawafuata wajukuu wa Said Sayyid, kuwaambia sasa imetosha, tupisheni nyumbani kwetu, na nyinyi rudini kwenu Oman?!, Yaonesha Waarabu walikataa na sijui waliwafanya nini hao waliodai chao! (nahisi waliwafunga mawe shingoni na kuwatosa baharini, na ndio maana Karume kuna watu aliwafanza vivyo hivyo!). Inawezekana kabisa walio organize yale Mapinduzi Matukufu ya 1964 ni masalia ya familia ya Mwinyi Mkuu!, hivyo mapinduzi yale ni haki na halali kabisa ya wenye haki kudai chao kutoka kwa wageni waliowakaribisha tuu kwa makubaliano fulani?!.

Kama Mwinyi Mkuu alivyowakaribisha Waarabu ili kuwalinda dhidi ya Wareno, ndivyo Karume aliwakaribisha Tanganyika kuingia muungano ili kuvilinda visiwa hivi visivamiwe tena na Waarabu?!, hivyo kama ilivyokuwa halali kwa Sultan Mkaribishwa kuitawala Zanzibar kama yake, vivyo hivyo ni halali Mtanganyika mkaribishwa kuitawala Zanzibar ili Mwarabu asithubutu kurejea kwa mlango wa mbele wa kukaribishwa, au kwa mlango wa nyuma wa vikaratasi vya kura?!.

Asante nimejifunza kitu, ila mada yangu katika uzi huu iko based kwenye taarifa hii A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba, hivyo ukiisoma na kuichambua lipi ni la kweli na lipi ni la uongo au limetiwa chumvi utanisaidia sana kukubali kumbe wazungu hawa ni waongo, wanawasingizia tuu Waarabu ukatili!.

Ahsanta.

Pasqwa.
 
PASCO
Nadhani kuanzia leo unite kaka na uniheshimu.

Mapinduzi na unyama wake nimeushuhudia kwa macho yangu, sikuhadithiwa. Nakumbuka waziwazi alipouliwa Inspector Sketi(?) na mkewe kwa mapanga mapolisi wazalendo kuwekewa vigogo vya mnazi kifuani, na wamakonde wakiwa na mishale wakiranda mitaani kuwaambia watu wawafichue mahizbu waliowaficha wapelekwe ( rahaleo) kituo cha madhila kilichowakusanya (mateka) wa hizbu na chachandu(ZPPP)

ASP waliopoteza maisha kwa ajili ya Mapinduzi ni wachache sana, hata kumi hawafiki! Uliza yalipo makaburi ya waasisi wa Mapinduzi. Yalikuwa ni mauaji ya upande mmoja. Ninachojua kuwa ASP wa Zanzibar waliwahifadhi wanachama wa hizbu wasiuawe na " wakombozi" kutoka bara na nchi jirani.

Ule uwanja wa Kibanda maiti uliobatizwa jina la uwanja wa demokrasia ndio una " mass graves" za wazanzibari waliouwawa Mapinduzi kwa kosa moja tu la kuwa wanachama wa ZNP/ZPPP. Tuombe mungu tu atusmehe madhambi yetu.

Mimi nimeshudia uhuru na hata kushiriki kumuaga Gavana Sir. George Mooring pale Forodhani ikishushwa bendera ya Union Jack na kupandishwa Bendera rasmi ya watu wa Zanzibar na Gavana akaingia kwenye meli ya Uingereza, huku mkewe akilia kama mtoto kuondoka Zanzibar ( yenye neema). Mimi sasa ni mzee( lakini si kikongwe)
Du!. Mkuu Baraghash, heshma mbele!. Nitakuheshimu kama ninavyomheshimu Mkuu, Maalim Mohamed Said, ila nawe lugha yako, michango yako na kauli zako zifanane na umri wako na zireflect heshima hiyo!.
Nakiri Mapinduzi Matukufu ya 1964, yameacha majeraha na makovu makubwa ndani ya mioyo ya watu!, namna pekee ya kutibu majereha haya na makovu haya ni kuundwa kwa tume ya peace and reconciliation, watenda wajitokeze kukiri kutenda, na sababu zilizowafanya watende hayo waliyoyatenda, na kujutia na kuomba msamaha, na watendwa wajitokeze na kusema walishuhudia nini kikitendwa, kisha wawasamehe walio watenda na kuwahakikishia hawana kitu machoni wala moyoni!.

Hii itasaidia yule jamaa yenu akishinda, atakabidhiwa nchi!, kwa hali ilivyo, kuna watu ukiwaona machoni, unaviona visasi viko wazi dhahri shahir, hivyo ukiwapa nchi, kazi ya kwanza itakuwa kuwalipizia kwa yale waliowatenda!.

Pasco
 
1) Waraabu hawakuwatesa babu zetu.

2) Waraabu na Wazanzibari weusi (Waislamu) ndio walioteswa na John Okello (kutoka Uganda) na wafuasi wake walipo ipindua Serekali ya halali ya Zanzibar (John Okello na wafuasi wake walifanya mauwaji ya kinyama kabisa, waliuwa maelfu ya Waislamu bila ya hatia yeyote ile).

3) Kwenye uzi huu wa bieshara ya watumwa, kwanini huyu Pasco hakuwataja Wazungu waliowatesa sana Waafrika? na kuwauza Waafrika huko South American na Europe? na wanaendelea kuwatesa Waafrika mpaka hivi leo kwa siasa zao za ubaguzi.

4) Pasco Acha chuki dhidi ya Waislamu

Huu mzunguko wa mapinduzi, waislamu, John Okello ni kwenda mbali sana ili kutaka kuvuruga kinachojadiliwa.
Eleza kwa ufupi biashara ya utumwa ya Afrika Mashariki na Maziwa Makuu.

Kwa kukusaidia tu, biashara ya utumwa imetokea miaka mingi sana katika mazingira, jamii na hali tofauti. Kubwa zinazokumbukwa Africa ni Trans- Antlantic Slave Trade iliyohusisha misafara sehemu kubwa ya Afrika Magharibi, Americas na Ulaya, na kuna hii ya East African Slave Trade iliyohusisha pwani ya Afrika Mashariki na Uarabuni. Hebu jadili hii ya Afrika Mashariki utupe labda ukweli ambao sisi wengine hatuujui
 
Wee Pasco, unatukana watu (Waislamu) kisha unatarajia kukumbatiwa?

Sometimes, inabidi tutumia dawa ya moto ni moto, kukujibu uongo wako huu unaoandika hapa.

Ukitaka heshima, anza wewe kuheshimu watu na wewe utaheshimiwa, In Sha Allah.

Heshima kamwe hailetwi na matusi.
(kama wewe unavyo fanya, eti unatafuta heshima kwa kutukana watu, kamwe hauzi kupata heshima mpaka ujirekebishe na uwaheshimu watu wote).
Mkuu Mandago, ukinionyesha sentesi moja tuu niliotukana Waislamu, nitakushukuru!, huu uzi sio kuhusu Waislamu ni kuwahusu Waarabu dhalimu waliofanya biashaa ya utumwa!. Unless kama unamaanisha nikisema Mwarabu ndio kumaanisha Uislamu!, hapo nitakuelewa kidogo, na bado kwenye bandiko zima sijatukana popote!, ila nakiri katika majibishano, kuna vichaa humu tunakutana nao, sasa kwa vile na mimi ni kichaa fulani, tukikutana na vichaa tunazungumza nao lugha moja, na tukikutana na Wataarabu kama Waarabu kina Maalim
Mohamed Said
tunaongea lugha za kistaarabu!.

Pasco
 
Sielewi kuhusu Sudan na Somalia, lakini ninachokijua kuwa wahabeshi hawajawahi kutawaliwa

Ni kweli pia watu wenye ngozi angavu na nywele laini hawakuchukuliwa utumwani,wafugaji kama wamasai,Bedouin,wafulani,wanubi pia hawakufanywa watu wengi walitakiwa wabantu wenye miili mikubwa iliyojijenga wanaofanya kazi hasa za kilimo
 
Pasco,
Mimi ni mtoto wa Mama Daisy.

toW0HLKw0_eZRKHUURD38LIxZWcW5RXD7goNoYJWFVWEj8kMEyL1bPXqHWB5CmfrXmD1mA=w329-h566-no

Kushoto: Mama Daisy, mbele ni Bi. Titi Mohamed
na kushoto yake ni Bi. Zainab mkewe Tewa Said Tewa
katika maandamano siku za mwanzo za uhuru

Ingekuwa si huu uhusiano wa kindugu Mama Daisy asingenieleza
chochote katika historia ya mumewe marehemu Abdulwahid Sykes.

Wakati ule watu walikuwa wakiogopa sana kusema lolote lililo kinyume
na historia ambayo watu walikuwa wameaminishwa.

Jina la Abdul Sykes na mdogo wake Ally na wazalendo wengine kama
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi, Tatu bint
Mzee, Iddi Faizi Mafongo
, Oscar Kambona kuwataja wachache yote
yalikuwa yamefutwa kabisa.

Siku ile Mwalimu Nyerere ambayo aliwahutubia Wazee wa Mzizima
yaani Dar es Salaam kuwaaga ambayo kwa bahati mbaya sana ndiyo
siku aliyosema hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani katika
TAA yeye alipoingia TAA Mama Maria Nyerere alikuwa na kikao kifupi
na akina Mama wa Dar es Salaam hapo hapo Diamond Jubilee Hall.

Mmojawapo katika hao akina mama alikuwa Mama Daisy.

Mama Maria aliwaeleza akina mama wale kuwa yeye na mumewe
walipokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes.

Wanamajlis,
Mtakumbuka siku niliposema kuwa Mwalimu Nyerere alisema kuwa
hakumbuki cheo cha Abdul Sykes katika TAA palizuka ubishi mkubwa
sana hadi Yericko Nyerere kusema yeye ataiweka hapa hotuba hiyo
tusikize kama kweli Mwalimu Nyerere alitamka kweli maneno yale.

Mama Daisy hakuwa na wasiwasi na mimi akinieleza kila kitu na kubwa
ambalo lilinishtua sana ni siku aliponiambia kuwa Allah ndiye atoae
ufalme, ''Baba yako yeye akimtaka sana Chief David Kidaha Makwaia
ndiyo aingie TAA wamchague president kisha waunde TANU.

Lakini Chief hakutaka.

Kila Chief akija Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya Legico tukimualika
nyumbani kwa chakula cha jioni na mimi nilikuwa pale nikiwaandalia na
nikisika mazungumzo yao yote.

''Bwana Abdul akimwabia Chief Kidaha, ''David hebu achana na hao
Waingereza bwana njoo huku tudai nchi yetu.''

Mama Daisy alikuwa na mengi na akizungumza alikuwa hana uchungu
kwa yale yaliyopita akizungumza huku ametulia kabisa.

Hali ya siasa katika TAA ilikuwa hivi katika miaka ya mwanzoni ya 1950.
Yako mengi lakini kwa leo haya yanatosha.

Anaetaka zaidi kuhusu Chief Kidaha Makwaia aingie hapa:
Mohamed Said: Chief David Kidaha Makwaia 1922 - 2007

Pasco,
Naona nikuage na picha ya maalim wako Chama Omari Matata:

Puqofe5Tukr_vrldX_KQCZcqhvlYql-3hCv-oKJO-g1VWax5tICiWzpb0MDvmuITpWKqmd3blpXyvub9H-iGAuNay4yMjnJf1rRGPe_90xFsSy2qQDYaSPbToEMwDdYuRgpHqEgYos6Upc_ifqPAnqx_pDsu-OSldzYHbqlArvt4ht50E9S6ipMo4D43g0jmE_hkAcKH5obdFF0-x7C05xgNbnLCsHgaapRC7_XhCFMV3bh8uy8nudlzYsjvBH3wVu9f_IFCounOxeinqidMa0BiJ0dow5L-jqNvptswbjtkB025NZblov1nnSv2tyuug5H82U-QdeUnosWZtqs4Xr4ltM_ynlrhw7jsXQaWueNH9fwzeLPP5iOqRtHustQV7C_Uc65rCTSoQbm0wDPpNR1xDS2MzKbZ3BvTdCYnydNs1yQ6i5oWDHmBMVhdYpGwmwXRzJXYVE4dsVhJLq_ja6fwyTohjV0rOlxgWZij9v5x9Iq8e_xt_-N8nBNHXXQaeG_83MhL1D1Frp9PtbBokJmiUTGOP78f2P36XjmWoRD5qlPz9iqim__owZ6Mgq6micizCQ=w878-h658-no

Kushoto: Ali Saleh, Mwandishi, Chama Omari Matata na aliyesimama nyuma ni
Balozi Mohamed Maharage BBC Club, Bush House London 1991
Mkuu Maalim Mohamed Said, wewe ni hazina kubwa sana humu jf na kwa taifa letu kwa ujumla, tatizo lako ni dogo tuu!, yale mambo yetu yale....ukiliondoa hilo, unastahili kuwa among the few members wa jf ambao wao ni ma great thinkers wa ukweli na ma walking Encyclopedia Tanzannica!.

Pasco
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, wewe ni hazina kubwa sana humu jf na kwa taifa letu kwa ujumla, tatizo lako ni dogo tuu!, yale mambo yetu yale....ukiliondoa hilo, unastahili kuwa among the few members wa jf ambao wao ni ma great thinkers wa ukweli na ma waliking Encyclopedia Tanzannica!.

Pasco
Pasco,
Tatizo unalo wewe na mfano wa wewe.
Mimi naalikwa kote kwa kuwa nina ilm ambayo haikufahamika kabla.

Ilm ambayo wewe inakutaabisha.
Kote nakwenda nahadhiri kuhusu ''Islam and Politics in Tanzania.''

Hiki ni kitu ambacho hawakukijua kuwa kulikuwa na ''strong Muslim
movement'' katika kupambana na ukoloni kuanzia Vita Vya Maji Maji
hadi katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Ni kweli pia watu wenye ngozi angavu na nywele laini hawakuchukuliwa utumwani,wafugaji kama wamasai,Bedouin,wafulani,wanubi pia hawakufanywa watu wengi walitakiwa wabantu wenye miili mikubwa iliyojijenga wanaofanya kazi hasa za kilimo
Wakamata watumwa, walikamata watu ambao ni makabila ya majembe kazi!, watu wa makabila ya nyanya hawakushughulika nao kabisa, ndio maana hata huko Zenj, hawakukamata watumwa!.

Pasco
 
Pasco,
Tatizo unalo wewe na mfano wa wewe.
Mimi naalikwa kote kwa kuwa nina ilm ambayo haikufahamika kabla.

Ilm ambayo wewe inakutaabisha.
Kote nakwenda nahadhiri kuhusu ''Islam and Politics in Tanzania.''

Hiki ni kitu ambacho hawakukijua kuwa kulikuwa na ''strong Muslim
movement'' katika kupambana na ukoloni kuanzia Vita Vya Maji Maji
hadi katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Maalim,
Mohamed Said
hakuna ubishi kwenye the role of Muslim katika ukombozi wa taifa hili, tatizo ni it was not the only ones, bat kulikuwa na wengine wengi tuu nao walichangia pakubwa na kuna wengine wengi tuu pia walikwamisha, tatizo ni pale recognition inapokuwa attached kwa kikundi kimoja as if there were the only one, ndio huu mimi nauita urongo!. Mfano Baghdellah alifungwa jela moja na Robert Makange na kosa lili lile, kisha mtu ajitokeze amtaje Baghdellah pekee na kacha kumtaja Makange!.

Kwenye maendeleo ya elimu, kuna tatizo mahali linalochangiwa na imani ya dini za kukaririshwa, kuna wengi wenu, immetoka kielimu kwa msaada wa seminari na sio madrassa, lakini hili ni nadra sana kulisikia mkiwasifu!, huo huo mfumo Kristu japo uliumiza baadhi ya watu, uliwakomboa wengi!, hivyo sometimes we have to swallow the bitter with the sweeter!, kwenye hili, ukilisoma bandiko, HILI ...ukanigundua ni kitu gani ambacho sikukisema, ujue kwa huyu jamaa aliyepo sasa, Juliasi ni afadhali!. Alianza na wa TRA, akaja na NSSF ataendelea mpaka awamalize wote!.

Pasco
 
Wakamata watumwa, walikamata watu ambao ni makabila ya majembe kazi!, watu wa makabila ya nyanya hawakushughulika nao kabisa, ndio maana hata huko Zenj, hawakukamata watumwa!.

Pasco
Wanamajlis,
Naona kuna hofu kuu ya kuzungumza mateso na mauaji yaliyofanyika
Zanzibar katika na baada ya mapinduzi.

Wenzetu wanakimbilia historia ya miaka zaidi ya 170 iliyopita.

Wnataka wawahukumu watu kwa historia ya mababu na babu
zao.

Kisa cha mbwa mwitu na mwanakondoo.
Pasco,
Nimekuwekea ushahidi wa Aman Thani umekuwa kimya.

Huna lolote la kusema kuhusu mauaji ya akina Twala, Hanga
Saleh Saadala
na wengineo?

Hawa si kizazi cha wakamata watumwa wa mika 200 iliyopita.
Huna chochote?
 
Maalim,
Mohamed Said
hakuna ubishi kwenye the role of Muslim katika ukombozi wa taifa hili, tatizo ni it was not the only ones, bat kulikuwa na wengine wengi tuu nao walichangia pakubwa na kuna wengine wengi tuu pia walikwamisha, tatizo ni pale recognition inapokuwa attached kwa kikundi kimoja as if there were the only one, ndio huu mimi nauita urongo!. Mfano Baghdellah alifungwa jela moja na Robert Makange na kosa lili lile, kisha mtu ajitokeze amtaje Baghdellah pekee na kacha kumtaja Makange!.

Kwenye maendeleo ya elimu, kuna tatizo mahali linalochangiwa na imani ya dini za kukaririshwa, kuna wengi wenu, immetoka kielimu kwa msaada wa seminari na sio madrassa, lakini hili ni nadra sana kulisikia mkiwasifu!, huo huo mfumo Kristu japo uliumiza baadhi ya watu, uliwakomboa wengi!, hivyo sometimes we have to swallow the bitter with the sweeter!, kwenye hili, ukilisoma bandiko, HILI ...ukanigundua ni kitu gani ambacho sikukisema, ujue kwa huyu jamaa aliyepo sasa, Juliasi ni afadhali!. Alianza na wa TRA, akaja na NSSF ataendelea mpaka awamalize wote!.

Pasco
Pasco,
Hakuna aliyetoa mchango kuwashinda Waislam kuanzia watu
hadi fedha.

Au mengine Mama Daisy hakukuambia?
Nimekuwekea picha yake umeiona?

2016%2B-%2B1
 
Wanamajlis,
Naona kuna hofu kuu ya kuzungumza mateso na mauaji yaliyofanyika
Zanzibar katika na baada ya mapinduzi.

Wenzetu wanakimbilia historia ya miaka zaidi ya 170 iliyopita.

Wnataka wawahukumu watu kwa historia ya mababu na babu
zao.

Kisa cha mbwa mwitu na mwanakondoo.
Pasco,
Nimekuwekea ushahidi wa Aman Thani umekuwa kimya.

Huna lolote la kusema kuhusu mauaji ya akina Twala, Hanga
Saleh Saadala
na wengineo?

Hawa si kizazi cha wakamata watumwa wa mika 200 iliyopita.
Huna chochote?
Uzi wa mauaji upo na tumeichangia kule, huu ni uzi wa madhila ya Utumwa na mababu zetu walichofanyiwa na Waarabu!.

Nyuzi zipo, tena kipindi hicho mimi nilikuwa newsoom, ni mimi niliyeripoti yale ya Mwembechai, ni mimi niliyeripoti yale ya Zanzibar, na Mwembe Madema nimelala, tena niliwa na Ali Saleh wa BBC, kumbe mwenzangu ana chama!, saa hizi yuko bungeni!. Mimi sina chama niko mtaani!.

Pasco
 
Pasco,
Hakuna aliyetoa mchango kuwashinda Waislam kuanzia watu
hadi fedha.

Au mengine Mama Daisy hakukuambia?
Nimekuwekea picha yake umeiona?

2016%2B-%2B1
Hakukuwa na mashindano ya kuchangia, lakini kama ni fedha taslim, hakuna aliyeichangia TANU kama Mzee John Rupia!. Kunawezekana shilingi elfu moja ya tajiri Mzee John Rupia, inaweza isiwe na thamani kama thumuni ya masikini muokota makumbi!.
Mama Daisy hakunihadithia mambo ya michango, bali the role ya wanawake kwenye harakati za uhuru na jinsi alivyomfunza Mama Maria ujasiliamali, kukanda chapati, kuokota makumbi, kuuza mauta ya taa, na walitembea peku!, ndala ni siku ya Jumapili!.

Pasco
 
  • Thanks
Reactions: bdo

Ni kweli ni Sykes walimlea Nyerere na kumpokea kuishi nae kwao baada ya kutokea Pugu, kabla hatahamia Magomeni!.

Pasco

Pasco
Pasco,
Ondoa hiyo sentensi yako ya mwisho,
Haina maana yoyote.

Muhimu katika yale niliyoandika kuhusu Mama Daisy
ni ule mkakati wa kuunda TANU na nafasi ya viongozi
waliokuwapo wakati ule.

Ndipo nilipomleta Chief David Kidaha Makwaia.
Hapa ndipo ungeuliza maswali.

Kuna kisa kizuri sana hapo.

Katika Dar es Salaam ya wakati ule hakuna kiongozi
ambae alikuwa hafiki nyumbani kwa Abdul Sykes
anza na Chief Abdallah Fundikira na malizia na
Chief Thomas Marealle.

Nyerere
alifika kwa Abdul Sykes kama walivyofika
hawa watu mashuhuri wengine.

Nyumba ya Abdul Sykes ilikuwa nyumba ya mipango
ya kumg'oa Muingereza Tanganyika.

Ndipo nilipocheka kumsikia Msekwa anasema ati Nyerere
alimshawishi Abdul Sykes na wenzake wakubali kuigeuza
TAA kuwa chama cha siasa.

Ingia hapa:
Mohamed Said: PIUS MSEKWA NA HISTORIA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
 
Pasco,
Ondoa hiyo sentensi yako ya mwisho,
Haina maana yoyote.

Muhimu katika yale niliyoandika kuhusu Mama Daisy
ni ule mkakati wa kuunda TANU na nafasi ya viongozi
waliokuwapo wakati ule.

Ndipo nilipomleta Chief David Kidaha Makwaia.
Hapa ndipo ungeuliza maswali.

Kuna kisa kizuri sana hapo.

Katika Dar es Salaam ya wakati ule hakuna kiongozi
ambae alikuwa hafiki nyumbani kwa Abdul Sykes
anza na Chief Abdallah Fundukira na malizia na
Chief Thomas Marealle.

Nyerere
alifika kwa Abdul Sykes kama walivyofika
hawa watu mashuhuri wengine.
Kwa mujibu wa nilivyohadithiwa, ilikuwa ni zaidi ya hivyo, lakini kwa vile umenishauri nifute nimefuta ila mambo ya jf, hata vitu visivyo na maana huwa tunaacha tuu. Hicho kisa kizuri kifungulie uzi wake!.

Pasco
 
Du!. Mkuu Baraghash, heshma mbele!. Nitakuheshimu kama ninavyomheshimu Mkuu, Maalim Mohamed Said, ila nawe lugha yako, michango yako na kauli zako zifanane na umri wako na zireflect heshima hiyo!.
Nakiri Mapinduzi Matukufu ya 1964, yameacha majeraha na makovu makubwa ndani ya mioyo ya watu!, namna pekee ya kutibu majereha haya na makovu haya ni kuundwa kwa tume ya peace and reconciliation, watenda wajitokeze kukiri kutenda, na sababu zilizowafanya watende hayo waliyoyatenda, na kujutia na kuomba msamaha, na watendwa wajitokeze na kusema walishuhudia nini kikitendwa, kisha wawasamehe walio watenda na kuwahakikishia hawana kitu machoni wala moyoni!.

Hii itasaidia yule jamaa yenu akishinda, atakabidhiwa nchi!, kwa hali ilivyo, kuna watu ukiwaona machoni, unaviona visasi viko wazi dhahri shahir, hivyo ukiwapa nchi, kazi ya kwanza itakuwa kuwalipizia kwa yale waliowatenda!.

Pasco

Ni heshima ya mkwe kufunika uso kwa vidole huku ukichungulia! Lugha yangu ni fasaha na ya kizanzibari ijapokuwa imechafuka kidogo kutokana maisha yangu niliyoyaapotezea Tanganyika kwa muda mrefu.

Mimi sijali nani anashika dola, lakini awe na mapenzi na Zanzibar na watu wake. Aheshimu silka, Imani na desturi na Mamlaka ya Zanzibar.

Uundwaji wa tume ya maridhiano ilikuwa moja ya ahadi ya chama cha CUF kama ikiingia madarakani.Wazanzibari wakaitikia wito na kuichagua CUF. Lakini Uamuzi wao ulizikwa pale majeshi ya JWTZ ilipozima demokrasia na azimio hilo limegeuka ndoto.

Mtawala Tanganyika hapendi kuiona Zanzibar kuwa kitu kimoja. Wanaendeleza siasa za DIVIDE & RULE ili kuzidi kututawala pamoja na rasilmali zetu
 
Back
Top Bottom