Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Umepanic sana, pole.
 
Mkuu naomba nikurekebishe kwenye modern slavery wahabeshi,wasomali na sudan wenye light skini hawakupelekwa utumwani naomba kutoa hoja
Historia inasema Nchi zote zilizoko ktk Fukwe za Bahari ya Hindi zilihusishwa ktk biashara ya Utumwa.
Hatq BIBLIA book of Leviticus INAELEZEA UTUMWA uliokuwa Huko ETHIOPIA Wakati huo hata Somalia ilikuwa ndani ya ABYSSINIA. Na kabla ya hapo ikiitwa THE Kingdom of Kush(1070 BC–AD 350)

Sasa unaposema Wasomali na Wahabesh hawakuwemo Ungeambatanisha na Ushahidi wa HISTORIA Inaokubalika ili tukufahamu Vizuri vinginevyo utakuwa Unaleta vitu kutokana na Fikra zako binafsi. NA Hili ni kosa Kubwa sana Ktk Kuandika Historia.
 
Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika iliyomegeka miaka mingi nyuma, yule Mwinyi Mkuu aliyemkaribisha Mwarabu, ni Mtanganyika, walipomchoka Mwarabu, wakamtimua na kuitawala Zanzibar wenyewe. Kati ya Tanganyika na Zanzibar, nani anatumia rasilimali za mwenzake?!.

Mali ni yako mwenyewe unakuwa huru kuitumia utakavyo!, ila kuna mtu alikaibishwa, akazoea na kujiona mali za makaribisho ni zake, aliporudi mwenyewe mwenye mali zake, mgeni mkaribishwa kaambiwa akae kando, anaona kama anaonewa!.

Pasco
 
Pasco,
Ally Saleh ni ''level'' nyingine.

Yeyote mwenye uwezo wake ana haki ya kuwa Mbunge
na zaidi ya Mbunge.

Namfahamu vyema Ally Saleh.

 
Hii ni hatari, nilidhani una makengeza pekee lakini natongo pia. Hiyo historia iliosema Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika iliomeguka umeisoma Kisonge au Lumumba. Basi na mie nakwambia Tanganyika ni sehemu ya Zanzibar kwa kuitawala kwa karne mpaka akaja mjerumani kukomboeni

Waliomkaribisha mwarabu kuja kuuondoa utawala dhalimu wa kireno ni jopo la maulamaa ( masheikh) kutoka Zanzibar( Mafia, Kilwa,Mombasa, Pemba) waliosafiri kwenda Oman kuwaomba ndugu zao katika imaan, kuja kuwasaidia kuondoa dhulma na fitina ya wareno ambayo ilishanza kuota mizizi.


Nakumbuka mwaka 1974 wakati wa utawala wa Alhaj Jumbem kwenye uwanja wa Amani, Mwl. Nyerere katika hotuba zake za " kisungura" alipoitaka Zanzibar kuchangia shughuli za Muungano si kwa ukubwa la eneo lake lakini kwa mujibu wa ustawi wa Uchumi wake.Huko nyuma Karume alikuwa kagoma kutoa senti kuipa Tanganyika, akilipiza kisasi kuwa Benki ya Tanzania kuilazimisha Zanzibar kununua pesa za madafu za Tanzania kwa fedha za kigeni.

Tanganyika uliuporomosha uchumi wa Zanzibar kutoka kisiwa tajiri kuwa ombaomba. Mafuta yetu mnayakodolea macho. Watu 1.5 Million na rasilmali tuliokuwa nazo ni rahisi kuifanya Zanzibar kuwa Singapore ya Afrika. Lakini hili linawezekana tu tukiwa na Mamlaka kamili ya nchi yetu.
 
Akili za kawaida zishatolewa na kuwekewa kinyesi kichwani. Dini zimeshawafanya mataahira hamjitambui wala hamtaki kuifagamu historia yenu. Baya la Mwarabu linahalalishwa na baya la Mzungu....pumbavuuuuuuuu
 
Kwa mujibu wa nilivyohadithiwa, ilikuwa ni zaidi ya hivyo, lakini kwa vile umenishauri nifute nimefuta ila mambo ya jf, hata vitu visivyo na maana huwa tunaacha tuu. Hicho kisa kizuri kifungulie uzi wake!.

Pasco
Pasco,
Fungua wewe uzi huo mimi In Sha Allah nitakuja kutoa darsa.
 
Mkuu pasco ame base zanzibar labda uzi anzisha maeneo mengine .vp au ww mwarabu?
 
Thank you very much for the useful information.
 
Wewe Pasco, naona sasa unaandika pumba tu, eti nahisi nahisi.

Huna hoja wewe.

Kuhisi sio hoja au sio Historia.

Unaweza kuhisi kitu lakini ikawa sio kweli unayohisi.

Dear members, asiwapotezee wakati wenu huyu Lofa Pasco mbaguzi wa rangi (mwenye chuki kwa Waislamu, tena sana).
 
Watu wote waliosoma wanajua vyema kwamba meli za wazungu ndio zilikuwa zikiwachukua watumwa wa Africa na kuwapeleka south American, Europe na North America (mpaka leo wapo huko). Acha kujidanganya.
 
Watu wote waliosoma wanajua vyema kwamba meli za wazungu ndio zilikuwa zikiwachukua watumwa wa Africa na kuwapeleka south American, Europe na North America (mpaka leo wapo huko). Acha kujidanganya.
Mkuu Mandago, haya usemayo ni kweli, ila biashara hii iliitwa Trans Atlantic Slave Trade, na pia ni kweli sio tuu vizazi vya watumwa hao vipo hadi leo, bali pia baada ya kusitishwa biashara hiyo, watumwa waliokuwepo Marekani na Uingereza walipewa fursa ya kurejeshwa Afrika, Wamarekani wakaja Afrika, wakatafuta pori, wakalifyeka, wakajenga makazi, na kuunfa nchi ya Liberia na kuwarejesha watumwa waliokuwa Marekani, Uingereza nao wakaunda Siera Leone na kuwarejesha watumwa wake waliotaka kurejea Afrika kwa idhaa zao.

Biashara ya utumwa iliyofanywa Afrika ya Mashariki, soko kuu la watumwa lilikuwa Zanzibar eneo la Mkunazini, watumwa hawa walipelekwa Arabuni, na India na wengine walibakizwa Zanzibar kwa matajiri wa Kiarabu. Watumwa hawa wa soko la Zanzibar, hatua ya kwanza waliyofanyiwa ni kuhasiwa!. Huu ni ukatili wa hali ya juu kwa binadamu kuliko ukatili mwingine wowote!, afadhali hata kuuliwa!. Hii genocide ilipelekea kusiwe na kizazi cha watumwa Zanzibar, Arabuni na India. Ila mabwana wa Kiarabu walkiwatumia watumwa wa kike kama wajakazi, hivyo kuwaingilia kwa nguvu. Wale walioshika mimba, waliuwawa kwa kutobolewa matumbo kiumbe kilicho tumboni tuu ndicho kilizikwa kama sii rizki na mwili wa mtumwa alifukiwa tuu kama mzoga!.

Ila kufuatia baadhi ya wanawake wa bara, kukolea kuliko wanawake wa Kiarabu katika mambo yale, ilitokea kwa mabwana wengi wa Kiarabu kuridhika na huduma za hao wajakazi watumwa, hivyo wakawapenda kwa dhati, na wakawaoa, hivyo kupanda cheo, kutoka ujakazi na kuwa masuria. Mtumwa akiishapanda cheo kuwa suria, anakuwa sio mtumwa tena!. Hawa masuria walipopata ujauzito, hawakuuliwa, bali waliendeleza ukoo, na ndio kisa cha kuwapo machotara Unguja, Pemba na Arabuni. Hili la mtumwa kugeuka suria, liliukumba hadi ukoo wa Sultani, ambapo yupo Sultani mama yake alikuwa mtumwa, na pia yupo mwana Sultani mwingine aliyezaliwa na mjakazi kwa siri, baada tuu ya mjakazi huyo kushika ujauzito, aliondolewa kwenye kasri, na kwenda kuozeshwa mahala pengine, ambapo mwana sultani alizaliwa huko, na kuonekana ni mtoto wa familia ya huko alikozaliwa, ila ukoo wa sultani uliokimbilia Uingereza, umeendelee kuihudumia familia ile hadi leo!, mwana huyo yungalipo hadi leo!.

Pasco
 
Watu wote waliosoma wanajua vyema kwamba meli za wazungu ndio zilikuwa zikiwachukua watumwa wa Africa na kuwapeleka south American, Europe na North America (mpaka leo wapo huko). Acha kujidanganya.
Kule mashariki ya kati walipelekwa na meli ya nani?
 
Mkuu hamna ushahidi wa wenyeji kuenda Oman kuomba msaada et kwa wenzao toka lini sisi waaafrica nyie waarabu mkawa wenzetu? Kamma however ni watawala wa city states za pwani walioomba uma wa waislam kuwasaidia kupambana na wareno,na aliengoza jahazi ni Mir Ali Bey ambaye ni mturuki na sio mwarabu
 


Sikatai hoja yako ili umeipeleka kale mno ndio mana nimesema modern slavery sasa kama ni ya kale hata Genghis Khan aliwakamata waasia wakiwemo warabu na waturuki na kuwapeleka Mongolia utumwani
 
Wakamata watumwa, walikamata watu ambao ni makabila ya majembe kazi!, watu wa makabila ya nyanya hawakushughulika nao kabisa, ndio maana hata huko Zenj, hawakukamata watumwa!.

Pasco

Mkuu pasco kwenye nyanya sijakuelewa unaweza fanya ufafanuzi
 
Mkuu pasco kwenye nyanya sijakuelewa unaweza fanya ufafanuzi
Kuna makabila ni majembe kazi, watu wa makabila hayo ni wagumu, wachapakazi kutokana na kula vitu vigumu vigumu kama ugali maharage, mihogo, magimbi. Makabila nyanya ni makabila laini laini, watu wake wako legelege kutokana na kula vitu laini laini, kama tende, halua, chips, wali, urojo, chapati maji, visheti etc.

Pasco
 
Haahahahhahah mkuu pasc
mkuu Pasco kwanza nashukuru kwa ufafanuzi yakinifu lakini pembeni naona umewachokoza kina ritz,faiza zamilun,barghash etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…