Hao ni wazuri wa kuwadanganya watu. nawaonea huruma watu ambao wanafumba macho. Hawa SMZ wanasema Maalim atarudisha utumwa, usultani, wakati ilivokuja meli kutoka Oman, waon ndio wa kwanza kwenda kuipokea kwa shangwe meli hio, kimbelembele ni wao kujipeleka, bandari ilifungwa ikawa hakuna mzigo kushuka wa kupanda kisa imepaki meli ya Oman, halafu hao hao wanakaa kwenye majukwaa wakiwaita waarabu wasshenzi, hao hao wanadai Maalim Seif anataka kurudisha usultani, na hao hao, walikuwa wanagombania wakabidhiwe msikiti ulojengwa na Serikali ya oman wauendeshe..... Bora Afya ni moja ya watu mashuhuri zanzibar wanaotukana waarabu na machotara, lakini yupo mstari wa mbele kwenda kula biriani na pilau ya hao machotara kwenye shughuli.
Sio Zamani sana, Jumba la Ajabu Zanzibar lilipata matatizo na upande mmoja kubomoka, Mbona hakuna skeleton ya mtu kwenye nguzo zilobomoka? Nnavoijua SMZ kama wangekuta mfupa japo wa kuku tu kwenye nguzo dunia ingepata habari, lakini ni aibu kwao kwa sababu ndio ilikuwa njia ya kuwakomba wajinga kwa kuwadanganya.
If i might not be wrong, Naamini, Waarabu walipokuja Zanzibar kutawala, hakuna mzanzibari alifanywa mtumwa, Ila watumwa walikuwa wanatoka nje ya kisiwa cha Zanzibar na kuletwa Zanzibar Kuuzwa kwa waarabu, wazungu, wahindi n.k
Ndio maana, mapinduzi haya yalifanywa na watu wasio wazanzibari wenyewe bali wakuja. SMZ iligawa mashamba ya waarabu kwa wazanzibar, wengi wao waliyakataa kabisa. Na mpaka miaka ya ivi karibuni, wale ambao waliyachukua kutoka serikali wanahangaika kuwatafuta wenyewe waya kabidhi kwa wamiliki halali.
Lakini sishangai watu wakiwa wanafumba macho.... 😀 😀 😀