Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Maneno ya ajbu sana kwa karne hii ya uwazi na ukweli,Hivi kweli kuna watu na akili zao tena wasomi wanachukua propaganda hizi zilizovumishwa wakati wa siasa za chuki dhidi ya waarabu na kuzifanya eti ndio ushahidi wa tukio zima?
Ni kweli utumwa ulikuwepo Afrika mashariki,na nikweli waarabu walishiriki,wakiwemo waafrika wenyewe hasa machifu na wazungu.Na ki ukweli utumwa ilikuwa ni biashara ya dunia nzima,lakini hili la Pascal Mayala ,naliombea ushahidi wa kuthibitisha kuwa,watumwa walihasiwa,Waliingiliwa kinguvu,Kutobolewa tumbo eti kwa kushika Mimba ya bwana wake,
Eti jumba la Ajabu kila nguzo ina kichwa cha mtumwa ? Ahhhh,kweli akutukanae...........,

Mbona historia hii huku Zanzibar haipo,inasimuliwa na waandishi wa huko Bara tuu?
Mbona huku hakuna Freed Slaves family isipokuwa chache na hawana story hizo mulizonazo nyinyi huko Bara?

Hata mwandishi wa kitabu hiki hapa chini alibanisha kuwa Utumwa ulianzishwa na wareno ndo wakaurithi waarabu,
Na pia ndani ya kitabu hiki anakiri kuwa Hizo ulizoandika wewe hapo juu zilikuwa hadisi za propaganda zisizokuwa na ushaidi wowote zaidi ziliongeza hamasa kwa Waafrika ili waiunge mkono ASP na ajenda yake ya kuwakomboa waafrika.
(Ukombozi Ambao hadi hivi leo Bado wanaogelea kwenye wimbi la umasikini na ukandamizaji ,na shida za kimaisha zaidi ya zama zile zilizokuwa za ukoloni)
 

Attachments

  • historia ya zanzibar 3 001.jpg
    246.9 KB · Views: 9
  • historia ya zanzibar 1 001.jpg
    268 KB · Views: 10
  • historia ya zanzibar2 001.jpg
    96 KB · Views: 7
Hata mwandishi wa kitabu hiki hapa chini alibanisha kuwa Utumwa ulianzishwa na wareno ndo wakaurithi waarabu,
Na pia ndani ya kitabu hiki anakiri kuwa Hizo ulizoandika wewe hapo juu zilikuwa hadisi za propaganda zisizokuwa na ushaidi wowote
Mkuu Battawi, kwanza asante kwa vitabu.
Kuhusu hizi propaganda ushahidi upo, sii ile milingoti ipo, enzi zile kulikuwa hakuna metal scanner, sasa kuna mobile scanner zile za containers bandarini, tulete, tuscan, propaganda hizo zifutwe, kwa sababu zamani ma Pharao, walizikwa na watumwa hai kule kwenye ma pyramids, wafalme walizikwa na mke anayempenda sana. Machifu walizikwa na mtu hai, India, mume akifa, ile siku anachomwa, mke shujaa, kukimbilia na kujitupa kwenye moto akiwa hai na kuteketea na mumewe etc. Hivyo japo ni propaganda, ila pia inaweza kuwa kweli, lolote linawezekana, kwani mtumwa alikuwa sii mtu ni bidhaa!.

P
 
Mkuu Nguruvi3 kule kwenye mnakasha mwingine kaeleza vzr kuhusu hawa jamaa tatizo lao kubwa hawataki mwarabu asemwe kwa lolote, kwao kusemwa kwa mwarabu wananasibisha na deen ya haki.

Na wanashindwa kutonasibisha utu wa mwarabu na deen ya haki, ni kama vile wenye tafakuri wasivyonasibisha kauli za kardinali pengo na ukatoliki.
 
battawi
1. Unaweza kunipa maelezo yenye mifano hai ambayo inaonesha waarabu hawajafanya biashara ya utumwa?
2. Kinachoendelea nchi za waarabu kinadhihirisha hata mababu na mabibi zetu walifanyiwa unyama. Waarabu kwa Waarabu wanauana kama kuku halafu wanamsingizia Marekani. Yaani wewe na dini yako nzuri ya amani halafu anakuja mtu baki hata humjui anakuambia shika panga ukamchinje ndugu yako na wewe unabeba panga na unamchinja ndugu yako. Je, hayo mafundisho ya dini yako yapo wapi?
Shida ya wafrika wanaona kuonesha ubaya wa waarabu basi umegusa uislamu. Dini isikufanye kipofu ukaona wewe ni sawa na mwaarabu wakati wewe ni mwafrika pure. Kuna waarabu siyo waislamu
Kubali kataa waarabu walifanya biashara ya utumwa hata huko Libya na Syria kuna wafrika wameshikiliwa na waarabu kama mateka mpaka walipwe ndiyo waachiwe. Iko hivi kuna baadhi ya wafrika wanazamia ulaya kupitia Libya na Syria sasa wakishafika huko, hawa waarabu wanawateka ili wapewe fedha.
Kuwait kuna wafanyakazi wa ndani wa Kiafrika wanauzwa kama bidhaa mpaka ninavyoongea sasa hivi
Wanapozungumzia ubaya wa mwaarabu siyo wanazungumzia uislamu. Ukumbuke hata wazungu walifanya hii biashara na hao hao wazungu walikomesha utumwa na siyo waarabu.
Laiti mababu zetu na mabibi zetu wangekuwa wanafufuka wangewashangaa sana wanao muunga mkono Mwaarabu na Mzungu.
Dini isikupofushe ukajiona ukiwa dini fulani basi wewe ni mkamilifu. Huko kwenye nchi za waarabu na wazungu ubaguzi wa rangi na dini unaendelea mpaka sasa hivi. Acha historia isimuliwe. pascal amezungumzia biashara ya watumwa iliyofanywa na waarabu na hajazugumzia dini.
 
Ukiabudu dini itakufanya uwe na uwezo mdogo sana wa kufikiria. Pascal amezungumzia biashara ya watumwa iliyofanya na Waarabu pamoja na maovu waliofanyiwa wafrika lakini kutokana unaabudu dini umeona kama umezungumziwa uilsamu. Kwenye kichwa chako umejenga picha kuwa Mwaarabu ni Muislam lakini kuna waarabu siyo waislamu. Na ukiwa kwenye dini fulani haikufanyi wewe kuwa mkamilifu. Unabisha kabisa kuwa waarabu hawakufanya biashara ya watumwa na hawakuwanyanyasa wafrika? Unakimbilia ni propaganda za wazungu.
Kama Waarabu wote ni waislamu na hawatendi dhambi imekuaje kwenye nchi zao wanauana kila kukicha na kujilipua mabomu? utasema wamerekani wanawachochea. Sasa wewe na dini yako ya haki imekuaje mtu baki akuambie shika panga au bunduki umuue ndugu yako na wewe unamuua?. Hayo mafundisho mema ya dini ambayo waarabu wanayafuata wameyatimiza?
Nenda darasani ukajifunze upya achana na hizi dini maana hazina uhalisia wowote ingekuwa hivyo wala wasingekuwa wanavaa mabomu wanajilipua wala kufanya ushoga. Waafrika mnafeli sana kumtetea Mwaarabu na mzungu kwenye biashara ya utumwa na maovu yake. Wewe matumbi kutoka kijijini unajiona upo sawa na Mwaarabu yaani ndugu yako Mwaarabu. Wafrika wanachekesha sana, ndiyo maana tunafananishwa na nyani.
The South: a Christian Republic






Six of the first eight US presidents were slave owners, five from the South.
 


Umeandika kwa jazba, hata huelewi dini ni kitu gani ??

Waislamu hawaabudu dini , Wanamwabudu Mwenyezi Mungu,Allah , ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa wala hana aliyefanana naye. Fullstop

Wachungaji wako kanisani hawasemi hata siku moja kuwa wazungu kuwa ndio walioanzisha biashara ya utumwa kila vurugu husukumiwa waarabu na kwa propaganda za kanisa kila muislamu awe mweusi kuliko makaa huitwa muarabu.

Wapi nilibisha kuwa waarabu hawakufanya biashara ya utumwa.

Hii biashara ilifanywa kama ilivyo bishara ya unga hivi sasa. Mpaka hiyo CCM yako kuna viongozi wanauza unga au nasema uongo??

Hata kanisa ndio hao wanaouza unga hivi sasa ukitaka ushahidi nitakuwekea lakini kimya umezushwa ugaidi ambao husukumiwa waislamu na waarabu
 

Unaweza kunitajia jina la huyo bibi yako aliyefanywa mtumwa ?? Labda utumwa wa CCM na Magufuli wake😛😛😛
 
Umendika kwa hasira na chuki sana, haya sasa tuletee za Wazungu walivyowachukua Waafrika kwa mamilioni.
Umepewa haya Ma nchi tujitawale lakini tumefeli tumeshindwa kabisa nchi zote za kiafrika ni balaa hatujiwezi. Itazame hiyo
 
Sasa umenipa moyo kama msomi kukubali kuwa kuna kasoro katika kulielezea hili suala utumwa wa waarabu.
Sasa tutumie facts za Kiakili ikiwa umekubali kuwa Hakuna ushahidi isipokuwa mlingoti na yale masanamu ya Cathedral ya Mkunazini na Stori zao za Kiuchochezi Mule kanisani kwenye jiwe la Damu za watumwa.Wao wamelivalia njuga suala lile kwa kuwa limewahusu Waarabu Waislamu ili kuwapunguzia Credit za kiimani na kuwa win wateja wao,ili wao waonekane ni wema huku wakiendeleza Kupandikiza chuki kwa Watanzania waliohuru .
Any way

1.Muarabu aliekuja Baada ya Ujio wa Mtume Muuhammad(SAW) na Uislamu,ambaye ki
ukweli alikuja akiwa tayari ni muislamu ,huyu alikuwa na ruhusa ya KUMILIKI WATUMWA NA KUWAUZA ENDAPO ATAKUWA NAYE WA KUMUUZA.Lakini Dini yake ilimtaka kuwatendea wema watumwa hawa kwa kuwapa huduma za kibinadamu na kufanya hivyo ni tendo la kiuchamungu na kumpa thawabu nyingi tuu.

2.Endapo mtumwa wake huyo ni wa nyumbani,na ni mwanamke,mwanamume huyo akiona amempendeza na kamkalia vizuri kimapenzi(yaani si unajuwa wanawake na maumbile yao ya kinyakyusa) ,Uislamu unamruhusu kumuingilia kimapenzi kama mkewe naakipata mimba ,mtoto atakuwa sawa na watoto wa mke wake wa ndoa na kwa maana hiyo, watamrithi haki zote ni zake.Aidha Mtoto huyo hatokuwa mtumwa,na yule mama yake huitwa SURIA,si

3.Mtumwa wa kiume ambaye alikuwepo Zanzibar, alikuja kwa ajili ya kufanya kazi,aghalabu alipewa eneo la kujilimia chakula chake mwenyewe, na huku akimlimia bosi wake shamba lake .Ama wale waliouzwa kwenda Arabuni ,vizazi vyao bado wapo hadi lao na si watumwa tena,maana walipewa uhuru na wamiliki wao ikiwa ni fidia ya makosa ya kidini yaliofanya ma wamiliki wao, na tayari wengine wameingiliana na Waarabu na kuwa raia.Hata rangi zao zimefifia.

4.Kule Misri kuna ''freed slaves''-Mameluke https://www.britannica.com/topic/Mamluk
walifika hadi kuwa watawala wa nchi kwa miaka zaidi ya100 -jinsi Uislamu ulivyo wabadili waarabu na kuthamini utu wa mtu.
'' Mamlūk, also spelled Mameluke, slave soldier, a member of one of the armies of slaves that won political control of several Muslim states during the Middle Ages. Under the Ayyūbid sultanate, Mamlūk generals used their power to establish a dynasty that ruled Egypt and Syria from 1250 to 1517. The name is derived from an Arabic word for slave.''
Hata Hivyo wapo majambazi hadi hivi leo ambao wanafanya unyama ,pamoja na Uislamu wao,hizi ni case zipo kila mahali na hatuwezi tuka Generalize kwa waarabu wote.
Mfano Yule mzungu aliyepiga waislamu risasi kule New Zealand hatutasema kuwa Ndivyo wazungu wote walivyo au wakiristo wote walivyo. Hivyo hivyo kwa Waarabu Maharamia.

Mwisho namalizia kwa kusema kuwa Habari hizi Za kuwanasibisha Wapinzani wa Siasa Zanziba na Uarabu au wanataka kurudisha waarabu au Ni vijukuu wa waarabu, lengo lake ni kuongeza chuki.Haya ndo hufanya sana na CCM na Wakubwa wao.Isipokuwa Nyerere na Mzee mwinyi sikumbuki kuwasikia lakini
Mh.Lukuvi, Mh.Mkapa Mh.Sefu Muhamed Khatib na wengineo wanposhindwa hoja za KisiasHUKUKIMBILIA KUPANDIKIZA CHUKI NA KUFUFUA STORI HIZI ZA KUUMIZA KWA KUWANASIBISHA WAPINZANI NA UTUMWA na UARABU WA SULTANI.ILHALI MASULTANI NI WAO ccm KWA KUNGANGANIA MADARAKA
Pitia hii document utasoma kitu.toka kwa waarabu wenyewe.
 

Attachments

Mkuu Battawi, asante sana kwa ilmu hii nzuri, vitu vingine ni kuelimishana tuu.

P
 
Biashara ya utumwa ilifanyika ulimwengu mzima,hakuna kabila wala taifa duniani,halikuwahi kutofanywa watumwa.Kuanzia waafrika,waarabu,wazungu,wahindi,wachina nk.
Watumwa walikuwa wakipatikana kwa njia za mateka wa vita,madeni(mtu kudaiwa)anafanywa mtumwa yeye au familia yake,kulipa deni,kuzidiwa nguvu kwa unyonge.Na watumwa wakipatikana kupitia kwa watemi wa sehemu husika,ndio wakiwauza kwa wageni.Na askari wa mtemi,ndio waliohusika kukamata hao mateka,na kuuzwa kama watumwa.
Historia inaonyesha,waarabu wa asili sio weupe,kama hawa unaowaona sasa,walikuwa weusi,ila baada ya kuingizwa watumwa weupe,kutoka nchi za mashariki ya ulaya,hasa wanawake,na kuoana na hawa waarabu,ambao walikuwa ni weusi,ndio kukapatikana kizazi cha waarabu weupe,baada ya mchanganyiko huo.Waarabu waasili,wamebakia katika kisiwa kimoja,cha Scotra,ambacho kiko Yemen,ndio wapo wengi,na ndio waarabu wa asili ni weusi.Na pia katika nchi za kiarabu wapo wachache,ambao hawakuchanyika na damu za wazungu wa mashariki.Na huu mchanganyiko,ndio unaosababisha,wengi waarabu wenye asili ya uzungu,kurudi tena ulaya,bila kujijua.
Mkuu Battawi, asante sana kwa ilmu hii nzuri, vitu vingine ni kuelimisha tuu.

P
 
Mkuu Kikwajuni 1, asante sana kwa ilmu hii nzuri, vitu vingine ni kuelimishana tuu
P
 
Muarabu asili yake ni mweusi,sio mweupe,ni kutokana na kuoana na wazungu watumwa,waliopelekwa nchi za mashariki ya kati,ndio kukapatikana machotara,weupe.Huwa sisi tunakosea,tunapowaona waarabu weusi ndio tunawaita machotara,kumbe ndio waarabu wenyewe.Twaweza kusema,katika taifa,linalopotea ni la waarabu wa asili,weusi.
Mkuu Kikwajuni 1, asante sana kwa ilmu hii nzuri, vitu vingine ni kuelimishana tuu
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusisahau hata jina Darusalaaam.... Dar es salaam ni Lao kwahyo muhame mji

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena sio jina tuu la Darusulum, hata lile jengo pale patakatifu petu, wamejenga wao, Mjerumani akataifisha, na kujifanya kajenga yeye, Mwingereza
kakarabati akajifanya kajenga yeye!.

Kaisikilize video kwenye uzi huu
P
 
Bora mzungu kuliko mmanga mwarabu. Waarabu wabaguzi sana wahed
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimwambia mwarabu asili yake mweusi atavunja uzazi wako.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko umeenda mbali sana. Tungejiuliza tu waamerika weusi walifikaje Amerika. Senema ya roots ina majibu yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…