battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,712
- 2,577
Maneno ya ajbu sana kwa karne hii ya uwazi na ukweli,Hivi kweli kuna watu na akili zao tena wasomi wanachukua propaganda hizi zilizovumishwa wakati wa siasa za chuki dhidi ya waarabu na kuzifanya eti ndio ushahidi wa tukio zima?Watumwa wa soko la Zanzibar waliouzwa Arabuni na Bara Hindi, ambapo baada ya kufika kule, wanaume wote walifanyiwa ukatili wa ajabu kwa kuhasiwa ili wasizaliane, na walifanyishwa kazi za shokoa.
Wanawake walifanywa wajakazi, kazi za wajakazi zinajulikana, wenye bahati zao, walifanywa masuria, wasio na bahati waliuliwa na wengine kujifia, ndio maana hakuna kizazi cha watu weusi India na Arabuni, hao machotara, ni kwa baadhi ya Waarabu wenye utu na roho nzuri, lakini the rest ni unyama unyama tu.
Idadi kubwa kizazi chotara cha machotara wa Zanzibar, Pemba na Arabuni, kulitokana na wanaume dhalimu wa Kiarabu, kuwaingilia kwa nguvu watumwa wa kike ambao walinunuliwa mahsusi kama wajakazi, na pale waliposhika ujauzito, wamiliki walikuwa huru, kuwafanya chochote watumwa wao, ikiwepo kuwatesa, kuwapiga hadi kuwaua kwa ukatili wa hali ya juu! Mtumwa mwanamke baada ya kuingiliwa ki nguvu, yaani kubakwa, ikitokea akashika ujauzito, mwanamke yule aliuwawa kwa kutobolewa tumbo, kutoa, kiumbe ambacho ndicho kilizikwa kama binadamu si ridhki, na mwili wa mtumwa ulifukiwa tuu kama mzoga!.
Je, wajua kuwa hata baada ya kupigwa marufuku kwa biashara haramu ya watumwa duniani kote, biashara hii iliendelea kufanyika Zanzibar kwa siri na kificho?!. Jee wajua kuna njia za chini kwa chini zimechimbwa Bagamoyo na Zanzibar ambapo watumwa walifichwa kwenye mapango na kupitishwa chini kwa chini hadi baharini?.
Je, ulikuwa unajua kuwa kila Sultani, wake zao na watoto zao, walipokufa, walizikwa na watumwa hai?!. Jee wajua mapokeo ya kwenye jengo la Beit Al Ajab, kwenye kila milingoti hapo, ndani walimuweka mtumwa hai mwanamume?!.
Ni kweli utumwa ulikuwepo Afrika mashariki,na nikweli waarabu walishiriki,wakiwemo waafrika wenyewe hasa machifu na wazungu.Na ki ukweli utumwa ilikuwa ni biashara ya dunia nzima,lakini hili la Pascal Mayala ,naliombea ushahidi wa kuthibitisha kuwa,watumwa walihasiwa,Waliingiliwa kinguvu,Kutobolewa tumbo eti kwa kushika Mimba ya bwana wake,
Eti jumba la Ajabu kila nguzo ina kichwa cha mtumwa ? Ahhhh,kweli akutukanae...........,
Mbona historia hii huku Zanzibar haipo,inasimuliwa na waandishi wa huko Bara tuu?
Mbona huku hakuna Freed Slaves family isipokuwa chache na hawana story hizo mulizonazo nyinyi huko Bara?
Hata mwandishi wa kitabu hiki hapa chini alibanisha kuwa Utumwa ulianzishwa na wareno ndo wakaurithi waarabu,
Na pia ndani ya kitabu hiki anakiri kuwa Hizo ulizoandika wewe hapo juu zilikuwa hadisi za propaganda zisizokuwa na ushaidi wowote zaidi ziliongeza hamasa kwa Waafrika ili waiunge mkono ASP na ajenda yake ya kuwakomboa waafrika.
(Ukombozi Ambao hadi hivi leo Bado wanaogelea kwenye wimbi la umasikini na ukandamizaji ,na shida za kimaisha zaidi ya zama zile zilizokuwa za ukoloni)