Kaka uarabu umekutawala sana east african slaves ndo unawaona waarabu weusi huko uarabuni na dada na mama zao walizalishwa huku wanaume wakiasiwa.waliokuwepo Europe na america from west Africa.
Fanya Kupata Darsa. Sio kama waraab hawakuchukua watumwa...walishiriki lakini main sponour na wahitaji wakuu wa watumwa ni Wazungu ili kufanya kazi kwenye mashamba na viwanda kazi kabla ya kuvumbuliwa umeme na technolojia ..wao ndio walo kuwa wahitaji.
Oman miaka hio walikua jua kali tupu . wao wenyewe ni shida tupu hakuna shamba zaidi la mitende sasa wachukue watumwa wakafanye nini huko jangwani ikiwa wao wenyewe kwa maelfu wamehamia pwani ya Afrika mashariki miaka na miaka ?
ni akili ya kawaida wala hai hitaji kufundishwa. Kule Oman sehemu za salala wapo Wa-Oman waki Afrika wengi tu na na tena Huko salala wao ma Alwatan..wanajidai na mji wao huwezi kufanya deal za kibishara bila yao..wana haki kweli kweli...Lakini hawa wlifika vipi? Hawa wengi ni watumwa walokua wakipelekwa Ulaya kupitia Suez Canal kukamatwa baada ya Zanziabr na Uiengereza kupiga marufuku biashara hii haramu. hawa waliteremshwa na kuwekwa hapa salala ..ni meli nyingi za kiingereza ziliwashusha hapa...huo dio ukweli na hawaja hasiwa kama unavotaka kuaminishwa na walimu wenu na kivukoni propaganda.
hawakuhasiwa kwa sababu huu mjii sana ni wao na wana haki zaidi ya wewe kua nayo nchini kwako..wanapata kila kitu wakitakacho kutoka serikali yao.
hebu nikupe darsa kidogo likusaidie soma kisa cha kuanza kwa biashara afrika mashariki
Vasco Da Gama
(1498 )'
Vita vya Msalaba vita hivi vilianzishwa'na Pope'Urban 'katika karne ya 13, vilidhoofisha ustaarabu mkubwa wa Kiislamu, isitoshe vilianzishwa kwa malengo ya kuumaliza kabisa Uislamu
Vita hivi vilikwenda awamu nne viliongozwa na majeshi kutoka Ufaransa Ujerumani na Uingereza Askari hao waliivamia Jerusalemu na kuipiga (Dola ya kiislam )na kuiba mali mbalimbali pamoja na vitabu vya Waislamu vya kihistoria na baadhi yake kuvichoma moto.
Ndani ya Hispania pia Chuo Kikuu cha Cordova kilishambuliwa na takriban zaidi ya Vitabu 80,000 vilichomwa moto na vingene 400,000 kutoka gaghdad vilichokuliwa na vingine vilitupwa baharini-
Kipigo hicho walichokipata Waislamu ndicho kilicho sababisha ya Wareno kugundua pwani ya africa mashariki na historia yake ndefu baada ya kupata nyaraka zilizopelekwa na Ibn Batuta.kadhalika baada ya kupata fununu hizo kuhusu dola kubwa ya kiislamu iliyoenea katika pwani ya Azania walitaka pia kumaliza hamu yao kwa kuipoteza kabisa katika kitabu cha kanisa katoliki kiitwacho HJistoria ya kanissa vipindi vya saba -F. portnann, kinaeleza mipango na maandalizi ya kuja kuishambulia dola hiyo ya kiislamu, kadhalika kueneza Ukristo kwa nguvu
IAMEELEZWA KUWA HIVI
Mwaka 1494 papa Aleksanda V.l alizigawa nchi za karibu na bahari ya Atlantiki; Wareno wazichukue zile za masharikki Wahispania wazichukuwe zile za mmagharibi nao wate waliambiwa wajitahidi pia kueneza dini ya Kikristo kila mahali'Kutokana na agizo hilo Wafalme Wareno na Wahispania walitambua kwamba walipewa mamlaka ya juu ya kanisa walioanzisha katika nchi zile yaani kupima majimbo kuweka maaskofu na kuwachagua Wamisinari nao Wareno walikubali Wamisionari Wakireno tu
kufikia mwaka 1497 ndipo walipotumwa Maaskofu wawili yaani bishop (Vasco Dagama na nduguye ) ili wafuate njia ambayo mchunguzi wa mwanzo Batholomea Diiaz alipita katika mwaka 1486, ambaye alifaulu kufika Africa ya kusini rasi ya tumaini jema (Cape of Good hope).
Hivyo vasco dagama na paulo dagama baada ya kusafiri katika nchi zenye mawimbi makkubwa hatari nyingi walifika katika nchi kavu katika siku waliyo iita ya kuzaliwa kwa yesu yaani Noel waliita nchi hiyo Natal kwa kireno ikiwa na maana ya kuzaliwa, walipumzika kidogo kisha wakaendelea na safari yao
tarehe 02/03/1498 walifika katika nchi ya manyika (Msumbiji ya leo ) wakapokelewa kwa amani sana walifikiria ni Waislamu kutoka Uturuki, mtawala wa hapo alipanda katika Merikeb yao iitwayo Berrio akatoa ushanga na kumpa nahodha kama zawadi...
Walipobaini kuwa wale sio Waislamu mapenzi yote yakaisha kwa kuwa Vasco Dagama alianza kupiga Mizinga na kuishambulia Msumbiji, Wenyeji hawakukubali walijibu mashambulizi vita vikkapamba moto kwa muda fulani na kumfanya vasco Dagama kushindwa kuendelea na safari yake ndani ya Msumbiji kutokana na hali hiyo hawakufaulu kufika Kilwa kwa merikebu zao zote zilikimbilia maeneo ya Mafia Unguja na pemba ambapo kuna sehemu walijificha
tarehe 7/4/1498 ziliingia mombasa, merikebu moja ilikwama (pwelea) mchangani merikebu hiyo iliitwa (san raphael ) na walipoona bara lenye milima mingi waliita milima hiyo ''serade san raphael yaani milima ya san raphael kwa hakika ile milima ilikuwa ni milima ya Usambaa
Walipofika katika bandari ya tanga wakatia huo Mtangata waliona mashua zilizosheheni matunda na viungo mbalimbali kutoka tongoni pamoja na vyakula mbalimbali vikiwazunguka na kuwakaribisha kwa amani pamoja na kuwaruhusu wachukue chochote kile wanachotaka katika shehena hiyo kwani ndio iliyokuwa desturi ya Waislamu kuwafanyia ukarimu wageni wao
baada ya hayo wenyeji walimuomba Vasco Dagama ateremke nchi kavu aingie mji wamfariji zaidi lakini alihisi hatari hivyo akawatuma wafuangwa wawili walio kuwa kama ni watumwa ili wakathibitishe amani iliyopo hapo nao wakarejesha majibu mazuri juu ya ukarimu waliofanyiwa na watu hao pamoja na utamaduni wao wa upole zaidi na kuwa ni Waislamu hasa wa kweli hawana madhara
Vasco Dagama akaona yafaa kuupiga mji ule pia ni katika kulipiza kisasi cha wale ndugu zao wa Msumbiji na ni moja katika malengo yao ya muda mrefu baada ya kuimaliza dola ya kiislamu ya Hispania Ghafla wakapiga Mizinga na wakazikamata mashua mbili na kuwateka watu wake kisha wakawashurutisha wawapeleke katika mji wa kilwa walipelekwa malindi na kilwa na vibaraka walio wafanya watumwa
Walipofika kilwa walipokelewa vizuri kama ilivyokuwa ada wakatembezwa katika mji yote muhimu mana walijifanya kama watalii wa enzi hizo walitembezwa mpaka nchi ya mussa bin hassan (Msasani), mwisho walioneshwa Njia ya kuelekea India
Wakati huu kilwa ikiwa chini ya fudeli bin suleiman kwani baada ya Muzhafar alitawala mohammed Suleiman'hussen kisha momammed kiwabi akifuatiwa na fudeli bin suleiman bin hussein
katika mwaka 1499 vasco dagama alirudi ttena na merikebu 4 zenye watu 148 na wafungwa 12 wakaenda na biashara mpaka india na kurudi hivyo hivyo mpaka kufikia tarehe 9/3/1500 alikuja na merikabu 13 na watu 1200 kutoka Ulaya ya wareno na mapadre 8 ili wajaribu kufundisha Ukristo''
katika kikao cha wanafalsafa na Wanasoshologia kilichosimamiwa na mataifa ya kirumi Kiyahudi kireno, Kijerumani na kipoland kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu cha filosofi na Soshologi kilichokuwa kinaitwa konisisisterg University nje kidogo ya mji mkuu wa Ujerumani nchi ya Uenyekiti wa Bishop George berkely.
Agenda kuu iliyojadiliwa na kupitishwa katika kikao hicho ni Treatise of government Namna ya kuzishika Dola katika masuala ya kijamii mada nyingine ni Essays' Moral and political Mwenendo wa maadili na siasa principle of sufficient reasons Sababu za kufanikiwa katika malengo na nyinginezo
Hivyo kutokana na maafiano ya kikao hicho ilifuatiwa na utekelezaji wa maazimio yale yaliyopitishwa wakati huo wareno walikwisha fanikiwa kiasi fulani katika Africa ya Azania na maeneo ya kongo walifanikiwa kumbatiza mani Kongo Zingankuwa na kumpa jina la john ll, kadhalika mwenae aliyekuwa akiitwa Mwemba na kupewa jina la Alfonso
Kutokana na maamuzi hayo pope nicholas V alimpa mfalme Alfonso ambaye alikuwa kibaraka wa wareno Africa alihodhi biashara yote ya Afica kwa mabavu na alimuagiza na kumuamrisha kuwa
(Tunamruhusu na tunampa uhuru wote Mfalme Alfonso wa kuwashika na kuwakamata na kuwapiga vita na kuwafanya kutii amri zetu waarabu na Waislamu wote na wasio na dini popote pale walipo Aidha na kukamata nchi zao falme zao zote mali yao ardhi zao na utajiri wao wote walionao na kuwaingiza katika Utumwa wa daima milele
Wachukue fursa hiyo wakawatumia wao na vizazi vyao na kwa vile Mfalme Alfonso na wenzake wameeepokea nguvu hizo basi watandelea kukamata kwa haki na daima visiwa hivyo na bahari na utajiri)
Kutokana na maagizo hayo fransisco D"Almeida na Vasco Dagama Walikuwa na kazi ngumu ya kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa kutokana na utaratibu maalumu walioupanga,'
Kilwa ikiwa chini ya Amir ibrahim wakati huo Fransisco D'almeida alipewa ugavana wa india ili kuweza kudhibiti mwambao wote wa pwani hiyo ya bahari ya Hindi
tarehe 12 july, 1502 vasco dagama aliwasili tena kilwa ili kuweza kutekeleza maagizo ya pope nicolas V. Vasco Dagama alimtaka Amir ibrahim afike katika marikebu yake haraka ili wafanye ushauri juu ya dola hiyo ya kilwa wakati huu ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Amir ibrahim kwa kuwa wareno walifanikiwa kuweka vibaraka puppets''wao katika kilwa na kumsaliti kiongozi wao
Wakati huo watu wengi waliingia karika usaliti huo wakiongozwa na Ankoni hayo yote yalikuwa ni matunda ya Antonio fernandas Mreno aliyekaa katika dola hiyo kwa muda mrefu kwa lengo la kuwaandaa wasaliti kutokana na hali hiyo Amir ibrahim aliukataa mwito huo wa vasco Dagama lakini vasco dagama allimtishia kumfunga kama mfungwa ndani ya merikebu kama atamkamata kwa nguvu yake na kisha autie moto mji wote wa kilwa
Kutokana na vitisho hivyo Amir ibrahimm alikubali na mashauriano yakawa ni lazima dola ya kilwa ilipe kodi kwa wareno na isitoshe wareno walisimamisha bendera yao pahala pa ikulu ya amir ibrahim (Huzuni kubwa )kwa nguvu hii ni kuashiria kwamba Waislamu wa dola ya kilwa wamenyang'anywa rasmi uhuru wao
Tangu yaishe mashauri hayo ilipita miaka miwili waislamu hao hawakufanya chochote katika yale waliolazimishwa kufanya
tarehe 22 july 1505,kamanda d.Almeida akiwa na merikebu 22 zilizojaa wanajeshi 1500 miongoni mwa hao walishawishiwa na vasco dagama kumsaliti kiongozi wao malengo makubwa safari hii ni kutimiza ile azma yao ambayo iliyobagwa
wareno walitaka kuwalazimisha waislamu kuingia katika Ukristo na walikuwa tayari kufanya hivyo kwa lazima kama ingewezekana
Amir ibrahim alitakiwa kwenda katika merikebu ya kireno ili akajibu kwa nini mpaka muda huo wote hawakulipa kodi mashauriano yalllllikuwa magumu sana amir ibrahim aliomba udharura kidogo ili akashauriane na watendaji wake pamoja na viongozi wake juu ya jambo hilo
Wareno walimtaka ibrahim aweke rehani mpaka hapo watakapo afikiana Amir ibrahim akapata nafasi ya kumuweka rehani yule msaliti wake yaani mohammed ankoni awe ndio rehani wakati ambao mammaed ankoni alipowekwa kwa wareno kama rehani naye aliitumia vizuri nafasi hiyo kwa kuwapa maelezo ya jinsi ya kuishambulia dola hiyo
maeneo sita yalikuwa ni muhimu sana eneo la kilwa mombasa rhapta (Mwanamakuka)songo mnara ras ya sofala na mogadishu humo ndimo alimo piga (Vasco Dagama na ndio mwanzo wa utumwa africa ya mashariki)