Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Unajua Waafrika dini zinatufanya tuwe kama wehu! Hapa wengine watatetea wazungu wengine watatetea Mwarabu lakini chachu ikiwa ni Ukristo na Uislamu!

Waarabu na Wazungu wote ni wafedhuli tu linapokuja suala la biashara ya utumwa kwa sababu wote hawa walikuwa wanadaka na kuuza Waafrika na wote walikuwa wananunua na kutumikisha Waafrika!

Hata hoja kwamba Wazungu walipiga marufuku biashara ya utumwa nayo ni nonsense kwa sababu pamoja na kwamba tunataka kujitoa ufahamu; majority tunafahamu kwamba Wazungu hawakupiga marufuku biashara ya utumwa kv walitupenda au kutuhurumia bali walifanya hivyo baada ya ku-shift production zone from Europe to Africa! Sasa watu wameshaamua mashamba yao wahamishie Africa bado mnatarajia wangeendelea kupeleka Watumwa Ulaya? Wakafanye nini wakati nguvu zao walitaka kuelekeza Africa?

Tanzania tuna historia ya vita vya Maji Maji ambavyo kimsingi vina - reflect hoja ya hapo juu kwamba; agricultural production ilihamishwa from Europe to Africa. Wale wazee ambao walichoka na kuanzisha mtiti dhidi ya Mjerumani nao walikuwa watumwa tu ndani ya nchi yao ya Tanganyika.
 
Mada ipo pale pale, ila ninakuonyesha kuwa hao wamisionari wako wa kizungu walikuwa, wanazo dharau kushinda hao uliowasema wewe!!!

Mimi nishakupa picha halisi za kamera kusibitisha maneno yangu sasa lingekuwa jambo jema ukaweka picha mfano wa hizo kuyapa nguvu maneno yako dhidi ya wahindi na waarabu.View attachment 339085

Picha ya camera kwa vile wazungu waligundua camera na kuwa nayo, waarabu hawakwa nayo ulitegemea wapige picha na nini? ulisoma bado hujaelimika kuna soko la watumwa Bagamoyo, Goldcoast, Senegal (goree) Zanzibar etc uwe unapenda kusoma si kulishana ujinga.
 
Pasco Kama unaijua na kukuuma Zanzibar njoo na history ya Zenj Empire, Mwarabu hakuvamia na kuiba visiwa mnavoviita vyenu vya unguja na Pemba. Pia kumbukumbu zinaonyesha bila ya Mwarabu usingekua Mkristo leo, rudi tena shule update your history nani kamdhalisha mnyika na hao babu zako.
 
pasco,

Pasco unajichanganya hapo mwisho. Huwezi ku-generalise eti Waarabu wa sasa ni wema wakishinda wapewe nchi. Sijui una maana gani. Ujue mwandishi unaye mkosoa ni Mwislam mhafidhina. Uislaam unaruhusu utumwa na mwenye mtumwa anaweza kumtendea mtumwa wake vyovyote.

Yapo mambo yasiyofaa kwa sasa katika imani ya kikristo ila wakristo wamekua wepesi kutoyatilia nguvu isipokua sio katika uislam. Bahati mbaya mtu mweusi mbele ya Mwarabu hadi leo ni mtumwa.

Tumeona na kusikia jinsi watumishi/wafanyikazi Waafrika wanavyotendewa uarabuni hadi leo. Ndio maana muandishi Mohamed Said anaona kuuliwa Waafrika na Waarabu sio chochote maana walikua watumwa.

Anachokiona yeye ni mauaji ya Waarabu katika mapinduzi ya 1964 maana hao ndio walikua watu. Kutokana na msingi wa historia, kuna kila sababu Mwafrika kua macho na kujihami na Mwarabu.
 
Mtoa mada nadhani unataka kuturudisha enzi zile za mzee wa kuota ndoto na kutabiri (Nyerere)

Katika rundo la picha ulizoweka kwanini kila picha inayoonyesha mateso ya waarbu kwa mtu mweusi iwe ya kuchora! Hivi wakati huo kamera zilizokuwepo zilikuwa hazipigi picha za mateso bali za furaha tu!?

Mada yako haina tofauti na hadithi za kusadikika wanazopewa wageni kila wakitembelea kanisa la mkunazini Unguja!!?? Wagalatia wa kanisa lile na wengineo wamesahau kuwa aliewapa kiwanja cha kujenge kituo chao cha kuzalisha propaganda dhidi ya waarabu ni uislamu ni Sultani wa kiarabu ambae ndie aliekuwa mtawala wa zanzibar!!??


Suala la kujiuliza ikiwa soko la watumwa lilikuwepo pale penye kanisa la mkunazini na wao ndio wenye kanisa, jee niwakati gani soko lilikuwepo na baadae ikapatikana nafasi ya kujenga kanisa!!???

Akili za kuambiwa.......

Mihemuko mingine shida sana. Heebu someni muelewe, ameshawaambia siyo Waarabu wote waliokuwa wakiwatesa watumwa,tena amerudia sijui mara ngapi? na akaenda mbele zaidi akasema wapo waarabu waliowapenda watumwa kwa dhati, na wengine wakawaoa na kuwazalia watoto!,hivi, kwa nini akili zenu zimefunikwa sana na hilo kaniki la dini?!.

Umeandika pumba nyiingi, kama hao wamissionari waliweza kuwalipia hao watumwa ili wakombolewe toka utumwani kwa mwarabu, wangeshindwa vipi kununua hivyo viwanja vya kujengea makanisa?
 
Picha ya camera kwa vile wazungu waligundua camera na kuwa nayo,waarabu hawakwa nayo ulitegemea wapige picha na nini?ulisoma bado hujaelimika kuna soko la watumwa bagamoyo,goldcoast,Senegal (goree) Zanzibar etc uwe unapenda kusoma si kulishana ujinga wa madrasa

Jiulize ipatikane picha ya kumpiga picha huyu mtawala wa kiarabu katika mwaka 1880 na yahuyu tiptip anaeambiwa ndio kinara wa biashara ya utumwa

009bb47e36b15c6b279e76c7beedf4dd.jpg
images.jpg
 
WE Pasco Mimi nikifikiri ni mchambuzi kumbe ni mtu wa chuki.

Hata hivyi nakuarifu hakuna Mzanzibari aliefanywa Mtumwa. Wafalme wa Zanzibar hawakutesa raia zao hata siku moja.

Ukweli utabaki Zanzibar ilikua ni kituo cha Biashara ya watumwa walokua wakiletwa na wazungu kutoka ndani Bara. Pale ndio ilikua ni soko na wanunuzi na wazungu.

Hakuna Mpemba, Mmakunduchi, Mdole, Mtumbatu Mkojani alo wahi kufanywa mtumwa. Walikuwepo wafanya kazi wa mashamba ya karafuu nao sio Wazanzibari ni manamba kutoka mainland bara.

Hivyo mada iko sahihi kabisa ya Mohamed Said kuwa hakuna Sultan alowahi kutesa wala kuua subject wake hakuna ushahidi huo..ndio maana Masultani waliheshimiwa na wakitembea biloa ya vifaru wala askari, walikua wakipita mashamba na mitta yote ya zanzibar bila ya wasi wasi.

Mapinduzi yaliuza watu kati ya 15,000 - 20,000
Sasa wakati huo znz ilikua ni watu 125,000 sasa wewe fikiria mwenyewe.
 
Pasco unatuwekea picha za kuchora halafu unatuaminisha kuwa ni picha za kweli.

Hizo picha ni za kuchora hazina tofauti na picha za Bulicheka na mke wake Elizabeth na Wagagagigikoko, au ile hadithi maarufu. ya ‘Heri mimi sijasema’.

Au picha za Juma na Roza, cha kufurahisha kuna watu wanakubalina na hizo picha.

Teh teh teh!
 
Pasco upande mmoja anasema machotara wote ZNZ ni zao la ubakaji,upande mwingine anasema kulikuwa na ndoa baina ya Waarabu na wasfrika.

Labda tumkumbushe watumwa wengi waliuzwa kwa Waarabu na Waafrika wenzao.
 
Pasco unatuwekea picha za kuchora halafu unatuaminisha kuwa ni picha za kweli.

Hizo picha ni za kuchora hazina tofauti na picha za Bulicheka na mke wake Elizabeth na Wagagagigikoko, au ile hadithi maarufu. ya ‘Heri mimi sijasema’.

Au picha za Juma na Roza, cha kufurahisha kuna mapunguani wanakubalina na hizo picha.

Teh teh teh!
Kumbuka umeamrishwa nini kuhusu picha na masanamu?
 
mimi siamini kama kuna waarabu wema,dharau ya mwarabu na mhindi kwa mu Africa ni mara 10 ya dharau ya mzungu
Bado tatizo lipo kwa Waarabu. Wale wageni wanaojenga viwanja kule Qatar wanalalamika, kina dada wanaotoka huku (Tanzania na Kenya) kwenda kufanya kazi nchi za kiarabu wengi wao hawatendewi kibinaadamu.

Kuna bwana aliwahi kutoa habari yake kupitia kipindi cha Njia panda(clouds) anaitwa Samadu (kama sikosei) alielezea madhila aliyokumbana nayo akiwa "utumwani" ikiwepo kuambiwa na wenyeji wake kuwa wao (weusi) wapo duniani kwa ajili ya kuwa Watumwa.
 
slavery.jpg

Hawa nao waarabu? Acheni chuki Zenu, Pasco wewe ni mdini na ni mmoja kati ya wanaoeneza chuki za kidini humu jamvini! na ni mbaguzi wa hali ya juu ! hatutakiwi kueneza chuki baina ya waTanzania lakini nyie mmezidi propagarnda,!

Mnaishambulia dini ya Kiislam kwa mwamvuli wa waarabu! MKOME!!!
 
View attachment 339100
Hawa nao waarabu? Acheni chuki Zenu, Pasco wewe ni mdini na ni mmoja kati ya wanaoeneza chuki za kidini humu jamvini! na ni mbaguzi wa hali ya juu ! hatutakiwi kueneza chuki baina ya waTanzania lakini nyie mmezidi propagarnda,!

Mnaishambulia dini ya Kiislam kwa mwamvuli wa waarabu! MKOME!!!
Hivi na wewe ni Mwarabu?
 
Pasco upande mmoja anasema machotara wote ZNZ ni zao la ubakaji, upande mwingine anasema kulikuwa na ndoa baina ya waarabu na waafrika
Labda tumkumbushe watumwa wengi waliuzwa kwa Waarabu na waafrika wenzao

Hivi hujui kuliwahi kuwa na sheria ya kulazimisha wanawake wa Kiarabu kuolewa kwa nguvu?
 
Back
Top Bottom