Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Kama kuna binadamu ambae amenyanyaswa na kupuuzwa ni mtu mweusi. Mtu mweusi awe muislam, mkristo, au mpagani. Nimeshtushwa sana na utetezi wa manyanyaso ya mtu mweusi katika jamvi hili eti tu kwa vile huyo aliyemnyanyasa ni muislam au mkristo! Wewe mtu mweusi kweli unaweza ukajidhalilishs kiasi hicho Kisaka eti hate tea uislam au ukristo? Hawa weupe na wanjano bado wanaamini kuwa wewe ni inferior kwao. Sio binadamu mwenye uwezo wa kufikiri kama wao! Bado unashangilia eti utumwa na unyanyasaji wa mtu mweusi ni propaganda na chuki dhidi ya uislam au ukristo? Watu weupe walikuwa waislam au wakristo na waliyafanya hayo kwa baraka ya hizo dini zao! Hakuna mwaarabu au mzungu aliyezaliwa mbinguni! Wote ni binadamu wenye tamaduni na imani fulani ikiwapo hiyo kuwa mtu mweusi hafai! Wamekuwa na kuishi katika jamii iliyoamini hivyo toka papa hadi imam mkuu! Hawa ni binadamu na huwezi kuwatenganisha na utamaduni wao. Ndio kumekuwa na mabadiliko ya kimtazamo kuhusu mtu mweusi lakini ukweli unabaki pale pale kuwa mtazamo wa babu zao kuhusu mtu mweusi ulikuwa hasi! Narudia tena iwe kwa dini ya kikristo au uislam! Hivyo ukiuhalalisha unyama huo eti tu kwa kuwa wewe ni mwislam au mkristo ni kichekesho na dharau kwako wewe mwenyewe mweusi. Historia imevurugwa sana ili kuonyesha kuwa ukristo hauhusiki na utumwa as well as uislam. Ni uongo, maana hawa washenzi waarabu na wazungu ambao hawakuthamini utu wa mweusi walikuwa waislam na wakristo. Mabadiliko katika fikra na mitazamo ya kidunia na dini zake hayafuti huu ukweli. Kama kuna mchangiaji mwaarabu au mzungu anayetaka wewe mweusi eti ukubali unyama waliotufanyia kwa mgongo wa hizo dini mbili na wewe ukakubaliana nae basi jua anakudharau na ataendelea kukudharau! Mtu mweusi na akili zako anakwambia kuwa haya yanayotokea katika siasa Za leo ni sawa na utumwa aliofanyiwa babu na bibi yako na wewe unamuunga mkono eti tu kwa sababu una support uislam au ukristo! Akili yako iko sawa au na wewe bado ni mtumwa! Dharau aliyofanyiwa mtu mweusi, bahati mbaya bado inaendelea underground, haiwezi ikatetewa kwa misingi ya huo upuuzi mnaotaka kujivisha. Nenda bagamoyo, Zanzibar, na Goree island huko Senegal kisha urudi hapa na kutetea ushenzi huu eti tu kwa kuwa waliofanya ni wakristo au waislam. Ni aibu ambayo haijawahi kutokea kwa utu wa mtu uliofanywa na hao wakristo na waislam kwa babu na bibi zetu. Waache waislam waarabu na wakristo wazungu wabishane nani alitudharilisha kidogo na siyo wewe mweusi uliyedharilishwa na unaendelea kudhrilishwa kuwa mtetezi wa wadharilishaji. Ebu tuwe upande unaotustahili. Bahati mbaya sijui kama huyo Pasco na Mohamed Said nao ni weusi kama sisi au ni uzao wa hao wadharilishaji wazungu wakristo na waarabu waislam? Ebu tujivunie weusi wetu!

Katika kitu ninachojivunia hapa ulimwenguni ni kuzaliwa AFRICA. na Uafrika wangu hauathiriwi kwa chochote kile ambacho mkristo,mzungu, muislamu anasema au anafikiri kuhusu mimi.

Pamoja na ukweli kuwa mimi ni mkristo, mzizi wa msingi wa imani haufundishi chochote kuhusu hayo unayosema.
Bibilia imeacha loophole ya mtu yoyote kuitumia kwa kujinufaisha na ndivyo walivyofanya wazungu lakini ipo siku imewekwa ambayo KILA MWANADAMU anasimama mbele ya kiti cha hukumu to give account of what he did. Kupitia ukristo Makasisi, wamisionari, wachungaji walitumika kama vilainishi vya utumwa hili halifanyi ukristo kuwa batili ila hao ndio wanakuwa batili.

Kuna dimension ya mwanadamu, Mtu mweusi, mzungu, mchina,mwarabu au mhindi wote wanapaswa kuwa huru. Ukweli kuwa kuna watu wengi wako utumwani leo kuliko miaka hiyo hauufanyi utumwa ule uwe bora kuliko leo. Leo tunashuhudia WAAFRIKA WENZETU wanakuwa ndio Pioneer wa kuhujumu wa afrika wenzao na kukalia mali zote na kufanya maisha ya mamilioni kuwa mabaya kuliko enzi za utumwa baadhi ya maeneo.

Kuna waafrika wengi leo Tumeganda mawazo kama matokeo ya utumwa huo, Tunashindwa kuwa productive ktk dunia hii tukidhani haya ni matokeo ya utumwa. Kwa kutambua hilo Dr Martin Luther King ilibidi aandae speech nyingine "THE DILEMA AND THE CHALLENGE" kuwaambia watu weusi muda wa kulialia na kuchukia rangi flani umekwisha, iache iwei historia. Hitaji la mtu mweusi ni MINDSET Change, Wajiandae kuwa productive,creative, Performing work in high precision and accuracy. Because the time was coming when american/negro/african will not be judged by their color but The product of their character and mindset.

Tusipoteze Muda kulialia na vitu vilivyopita wakati leo hii Mtanzania mmoja anaweza kijilimbikizia trillion4 kodi za wananchi na kusababisha vifo vya maelfu ya watoto na wakina mama na watoto kwa ukosefu wa madawa, zahanati, chakula etc., Graduates wanalia ajira wakati wazungu, waarabu, wahindi wasio hata na diploma wanaingia nchini kufanya kazi nchini kwa rangi zao tu tunawaita experts wakati hawajawahi hata kufanya hicho kilichowaleta.
Huyu ni mbaya kuliko hata hao unaohubiri wachukiwe.

Waafrika wa sasa wengi wanajiweka utumwani kabla hata ya kutumikishwa, wanajibagua hata kabla ya kubaguliwa.
 
Mi nashangaa mtu mweusi kulalamika kubaguliwa,kama kweli mtu mweusi anaamini kuwa yeye hana tatizo ni binadamu wa kawaida kama walivyo watu weupe je,haya malalamiko ya kubaguliwa ya nini?

Watu weusi wanabaguana nao kwa mambo mbalimbali na hata weupe nao pia hubaguana, ila sijaona weusi kuwabagua watu weupe kwa sababu ya weupe kama wafanyavyo weupe kwa watu weusi.

Hii ina maana ya kuwa weusi ni tatizo na si sawa kama walivyo watu weupe na ndiyo maana mtu mweusi hujichubua ili awe mweupe na mambo mengi tu hufanya mfano wa HILO.
 
Pasco upande mmoja anasema machotara wote ZNZ ni zao la ubakaji,upande mwingine anasema kulikuwa na ndoa baina ya waarabu na wasfrika
Labda tumkumbushe watumwa wengi waliuzwa kwa Waarabu na waafrika wenzao
Kweli mkuu mm naweza kuwa na mbuzi wangu Natafuta mteja Si lazima nitafute mnunuzi sawa watumwa wengi wakiuzwa na ndugu zao wakiuzana kama mbuzi.
 
pasco,

Humo kwenye maandishi mekundu, naomba ufafanuzi zaidi

1. Wageni wa mwanzo walikuwa ni wairani(washirazi) na baadae wakaja hao waomani. Wairani ni shia na waomani ni maibadhi ( % kubwa ya nchi hizi ). Dini ya kiislam haikuletwa na hao watawala bali ilikuwepo zamani sana, kwa rekodi za wareno waliwakutwa waswahili ( watu wa mwambao ) ni waislam, na hio ni kabla ya kuja kwa waomani.

2. Shehe Abeid Aman Karume aliowa mwanamke wa kiarabu na yule alokuwa rais wa Zanzibar Karume mdogo pamoja na kaka yake ambae ni waziri wa mawasiliano kwa sasa wa kule Zanzibar Ali karume ni machotara. Sio machotara wote ni wa baba wa kiarabu na mama wa kiafrika, Ukoo wa kisultani una damu ya kiafrika kwa maana Huyo babu yao mkuu hakuja na mke huku pwani, aliowa na akazaa na wanawe wakawa masultani. Picha zao utawaona kama sio warabu halisi bali ni machotara.

3. Je, hio biashara walikuwa wanafanya na nani ? maana watumwa walitakiwa na soko halikuwa arabuni tu bali hata amerika ya kusini hususn brazil, kweli usemalo ndo maana yale mapango ya watumwa kule MANGA PWANI NA BWAGA MOYO ila hapa tusiwasahau wanunuaji.

4. Mi miliskia ngome kongwe kila nguzo ina kichwa cha mtu, kama kweli basi waingereza walifanya kitu kibaya sana, maana beit la jaib lilijengwa na Muingereza, sultani walilipa tu hakujenga yeye.Hizo nahisi itakuwa ni hadithi za kusadikika (nionavyo mimi).

5. Sasa hichi ni chanzo cha habari kizuri ila kawaida ya Waingereza maisha kuponda wenzao na kujikweza wao, kama ilivyokuwa kwa yule Livingstone, etc ( juzi juzi tu waliomba radhi kwa kusema eti Irak lilikuwa ni kosa kuivamia, na Obama nae kuhusu Libya). kumbuka hawa mabeberu hawawatakii mema wasio wao, anakupa sh 100 ila ujue atakunyang*anya 5000 (maoni yangu ).

6. NB sisemi kama utumwa ni mzuri wala watawala ( Warabau na Wazungu ) hawajatufanyia unyama ila kwa sasa tuyaache na kusonga mbele kwani sasa pia wanatuburuza kiakili.
 
Nilipokuwa mdogo niliambiwa kwamba katika kila nguzo ya Beit el Ajaib kulikuwa na mtumwa aliyejengewa pamoja na hiyo nguzo, na niliamini hivyo. Lakini ndugu yangu Pasco pamoja na uelewa wako wa mambo kwa hili ni jambo la uongo kabisa. Nikupe ushahidi wa hili ni kwamba hivi karibuni kiasi cha mwaka mmoja hivi, lile jengo lilianguka upande mmoja pamoja na baadhi ya nguzo pia.

Kwa bahati nzuri nilikuwepo katika visiwa vya marashi wakati huo wa tukio hilo na nilikwenda kuangalia ila cha ajabu hapakuonekana dalili yoyote wala ushahidi wa kile ambacho tukiaminishwa wakati huo kwamba zile nguzo zilijengewa watu ndani yake. Huu ni uongo na historia potofu tuliyolishwa. Wakati mwengine ukiambiwa changanya na zako.

Cc
Pasco
 
Mawazo ya Watanzania wa zama hizi unaweza kila kwa kuwasikitikia lakini tambueni jambo moja ukatili ni ni ni moja ya nyenzo ya kufanikisha makusudio yao ya kutawala ama kujipatia mali ama kubaki madarakani. Hivi toka tupate uhuru hakuna kipindi ambapo watz wamepita kwenye wakati mgumu kwa kusababishiwa na wenzetu, acheni kupatiliza watu makosa ya babu zao.
 
Kama hao waarab waliwapa mimba kisha kuwaua hao wamatumbi na kuzika mama na mtt hao machotara walitka wapi??au walishushw mbingun?
Soma uelewe, umeambiwa kuna wengine pamoja na kwamba waliwanunua kama watumwa waliwapenda watumwa wao na ndo maana mpo machotara kibao
 
Na Pasco na wale akina yeriko Nyerere yakapingwa makanusho yao na baadhi ya member humu wenye kujitambua, ikawa ule mjadala umeenda sawa sawa na Historia ikafahamika.

Mseza mkulu, nafikiri hukunielewa au sijakuelewa! Kulialia na hiyo mind set unayosema ni pamoja na kutokujitambua mwenyewe. Ukombozi wa mwafrika ni pamoja na kujitambua kuwa yeye ni binadamu mwenye uwezo kama mwingine! Sikugusia hata kidogo nini mwafrika afanye, ila nimekosoa na ni naendelea kukosoa kutojitambua kwa mwafrika!

Leo hii mjinga anatokea na kusema eti utumwa ni fiction eti tu kwa sababu unahusishwa na ukristo ( mzungu) au uislam (uarabu) na wewe mweusi unasema it is ok! Distortion ya historia ya utumwa inaingizwa na kuusafisha huu unyama simply because imegusa uislam na ukristo na wewe unasema tungange yajayo!

Nitaanza kwanza kuweka historia katika ukweli na ni heshimike kwa Hilo then I move forward. Mbona antisemitism ni kosa la jinai? Nakubaliana na wewe kuwa tunatakiwa tujikwamue kielimu, utawala bora, etc, lakini sio kwa kutukana na kufuta yaliyowakuta babu zetu kwa kuwasafisha waarabu na wazungu simply because they belong to my faith.

Unfortunately, I, first belong to my colour of my skin then others follow. Dini zote lengo ni wema lakini zina uhusiano wa karibu na mila na utamaduni wa huko zilikoanzia. Soma Quran tukufu au agano la kale la biblia takatifu. Yaani kitu kibaya kikiwa na connection na hizo imani za wazungu na waarabu basi mweusi mjinga yuko tayari kuukana weusi wake!
 
Kwa Mzanzibar halisi waarabu kwao walikuwa ni watu waliowajali na kuwaheshimu, ni waarabu hao hao kutoka Omani ndio waliokuja kumkomboa Mzanzibar asili kutoka kwenye mateso na madhila waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa Makafiri ya KIRENO.

Niwaarabu hao hao ndio waliowafundisha ushujaa akina abushiri, mkwawa, kinjengetile na wengineo kuonesha chuki za waziwazi katika kupinga unyanyasaji wa Kijarumani.

Hakuna historia inayosema kuwa watu wa unguja na pemba walishawahi kuuzwa utumwani au kugeuzwa watumwa!! ACHENI UAPEDOMIA.

Mtoa mada anatofauti gani na wale wagalatia wa anglikana pale mkunazini unguja!! Ukienda kwao hadithi za uongo watakazokupa pale mwenyewe ukitoka pale chuki tele dhidi ya waarabu na dini yao!!! Maskini wagalatia wale wanasahau kuwa aliewapa kiwanja cha kujengea kitengo cha propaganda zao dhidi ya waarabu na dini yao ni hao hao waarabu waliokuwa wanatawala Zanzibar!!! Wanadhani watu hawayajui haya.

Lakini haya hatuyashangai kutoka kwa wagalatia wa tanganyika!! Niwao waliounda jeshi na kwenda kuipindua serikali halali ya zanzibar na kuwauwa watu zaidi ya elfu ishirini.

Niwao wanaohubiri chuki makanisani kwao (LUKUVI) huku wakisahau kila siku hodi hodi kwenye nchi za waarabu.

Mwisho mtoa mada atambue hakuna ushahidi wowote ule utakaonyesha wazanzibar waliuliwa kwa wingi na waarabu kuliko walivyouliwa na watanganyika katika MAPINDUZI YA 1964 NA KWENYE MAANDAMANO YA JANUARY 21/ 2001


fe9e9-annamakindaoman.jpg
images-7.jpeg
c3580-img_20141019_110606.jpg
IMG_20141019_111448.jpg
PG4A7387_1.jpeg
 
1460809518614.jpg
Inasikitisha sana kama binaadamu anafikia kumfanyia mwenzake anaefanana nae kasoro rangi tu mambo kama haya,hakika mtu huyo ni mnyama,halafu anatokea mweusi kama mimi kuwatetea waarabu huwa napata shaka na uelewa wake..mwarabu ni mtu mbaya sana nafanya nao biashara huwa sitakagi hata tuzoeane zaidi ya kazi tu.nakumbuka mwaka 2012 kulikuwa na friend match ya Simba vs Yanga(hii tunayoita mtani jembe),

Simba walishinda sasa ikatoka crew ya mashabiki wa tawi la Upanga kuelekea lilipo jengo la Simba kwa kupitia mtaa wa Msimbazi ilipo Home Shopping Center ilikuwa majira ya jioni saa moja kasoro,walipofika hapo kwenye jengo la HSC me nilikuwa pembeni kama hatua 50 nikasikia mlio wa risasi kitambo kidogo nikasogea nikakuta mabishano kati ya wale jamaa na mwarabu mmoja mfupi hivi kazungukwa na mabaunsa huku kuna dogo kalala chini damu zinamtoka mguuni..kilichonitisha na kunitia hasira ni kule kumsikia yule kenge wa kiarabu kusema kwamba “nilikuwa natest bastola yangu isije ikapata kutu".

Kutest silaha kwenye mwili wa mtu!!!baadae kuuliza nikaambiwa kuwa ndiye mmiliki wa hilo duka la mapazia na kwamba hilo alilofanya ni jambo dogo sana kwake huwa haogopi kufanya chochote.mkuu Pasco nashkuru kwa post yako hii nzuri,nimejifunza kitu hapa.
 
View attachment 339245
Inasikitisha sana kama binaadamu anafikia kumfanyia mwenzake anaefanana nae kasoro rangi tu mambo kama haya,hakika mtu huyo ni mnyama,halafu anatokea mweusi kama mimi kuwatetea waarabu huwa napata shaka na uelewa wake..mwarabu ni mtu mbaya sana nafanya nao biashara huwa sitakagi hata tuzoeane zaidi ya kazi tu.nakumbuka mwaka 2012 kulikuwa na friend match ya Simba vs Yanga(hii tunayoita mtani jembe),Simba walishinda sasa ikatoka crew ya mashabiki wa tawi la Upanga kuelekea lilipo jengo la Simba kwa kupitia mtaa wa Msimbazi ilipo Home Shopping Center ilikuwa majira ya jioni saa moja kasoro,walipofika hapo kwenye jengo la HSC me nilikuwa pembeni kama hatua 50 nikasikia mlio wa risasi kitambo kidogo nikasogea nikakuta mabishano kati ya wale jamaa na mwarabu mmoja mfupi hivi kazungukwa na mabaunsa huku kuna dogo kalala chini damu zinamtoka mguuni..kilichonitisha na kunitia hasira ni kule kumsikia yule kenge wa kiarabu kusema kwamba “nilikuwa natest bastola yangu isije ikapata kutu".kutest silaha kwenye mwili wa mtu!!!baadae kuuliza nikaambiwa kuwa ndiye mmiliki wa hilo duka la mapazia na kwamba hilo alilofanya ni jambo dogo sana kwake huwa haogopi kufanya chochote.mkuu Pasco nashkuru kwa post yako hii nzuri,nimejifunza kitu hapa.

Jee anapotokea mtu akatetea haya kisa kayafanya mzungu jee huyo mtu tumuelewe vipi!!???

Mateso na manyanyaso wanayopta watu weusi kutoka kwa wazungu ni mabaya kuwahi kutokea!! Kama huamini waulize akina Etoo watakuhadisia.
FB_IMG_1456312347887.jpg

images-5.jpeg
Ota-Benga-at-Bronx-Zoo.jpg
 
ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA PILI)

Je, kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni sawa na Isa?

Taarfa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.

Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa == Gabrieli alivyomtokea mama wa Yesu:

WAISLAM-JIBRIL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa Msikitini Qurani 19:16-17
WAKRISTO-GABRIEL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa nyumbani kwake - Lk 1:26-28

WAISLAM-Mariamu Mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji kipi wala mji gani wala hata nchi haijulikani. Isitoshe Quran inasema kuwa Jibril ndiye aliyemletea utume Muhammad asiwapelekee Mayahudi (hana kosa) Sura 2:97
WAKRISTO-Lakini Mariamu Mama yake Yesu alitokewa na Malaika Gabriel akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya Israeli (Lk 1:26) Mariamu Mama wa Yesu ni Myahudi.

WAISLAM-Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu mama wa Isa ila alijimithilisha kwa umbo la binadamu aliye kamili - Sura 19-17
WAKRISTO-Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu – Luka 1:28

WAISLAM-Jibril alimwambia Mariamu kwamba mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe mwana mtakatifu - Sura 19-19
WAKRISTO-Lakini malaika Gabrieli alimwambia mama wa Yesu kuwa utachukua mimba – Luka1: 31

WAISLAM-Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye mtoto muujiza kwa wanadamu – Sura 19: 21. Isitoshe Jibrili hakutaja jina la mwana kwa Mariamu. Bali alisema ili nikupe mwana mtakatifu.
WAKRISTO-Malaika Gabrieli alisema kwa Mariamu mama ya Yesu kuwa mtoto jina lake utamwita Yesu (Luka 1:31; 2:21) Gabrieli hakusema kuwa atampa mwana Mariamu. Bali alisema, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani motto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.

TOFAUTI YA KUZALIWA KWA ISA NA YESU
Isa bin Mariam Yesu Kristo
WAISLAM-Isa alizaliwa katika shina la Mtemde – 19:23
WAKRISTO-Yesu kazaliwa katika hori la kulishia ng’ombe. Luka 2:7

WAISLAM-Kuzaliwa kwa Isa haijulikani mimba ya mama yake ilichukua muda gani maana malaika Jibrili alisema nikupe mwana mtakatifu mara akachukua mimba na kuzaa. (19: 22-23)
WAKRISTO-Lakini Mariamu Mama wa Yesu siku zake za kuzaa zilitimia. (Luka 2:6-7)

WAISLAM-Qurani haionyeshi kama Isa alitabiriwa na manabii kuwa atazaliwa

WAKRISTO-Lakini Biblia inatuthibitishia kuwa Manabii walitabiri kuzaliwa kwa Yesu, (Isaya 7: 14; 9:6) utabiri huu ulitolewa na Nabii Isaya miaka 750 kabla ya Yesu kuja kuzaliwa nao ulitimia (Mathayo 1:18-23)

WAISLAM-Isa haijulikani alizaliwa katika kijiji gani wala mji, wala nchi aliyozaliwa Qurani haikueleza.

WAKRISTO-Biblia inatujulisha kuwa Yesu alizaliwa Bethelehemu ya Uyahudi katika Mji wa Daudi umbali wa maili 5 toka kusini mwa Yerusalemu nchi ya Israeli (Lk 2:8-16). Kuzaliwa kwake mahali hapo pia ni kutimiza unabii uliotolewa na nabii Mika miaka 750-686 kabla ya kristo kuja wakati wa wafalme hawa wakitawala – Jotham, Ahaz na Hezekia wafalme wa Yuda. Yesu mwenyewe alizaliwa kama mwaka wa 4 wakati wa Mfalme Herode.

WAISLAM-Isa aliongea na watu akiwa mototo mchanga, na kusema kuwa yeye ni mja wa Mungu amepewa kitabu na amefanywa Nabii (Sura 19:30-33)

WAKRISTO-Yesu hakuongea na mtu akiwa mtoto mchanga. Alianza kuwauliza maswali na kutoa majibu akiwa na wazee Hekaluni akiwa na miaka 12. (Luka 2: 42-49)

Hivyo tunaona kwamba tuna tofauti nyingi tu kati ya Bwana Yesu na Isa. Swali kwako mfuatiliaji je, Isa bin Maryamu ndiye Bwana Yesu Mwokozi? Tafakari.

Mungu awabariki sana na tuendelee kujifunza tofauti za Isa wa Quran na Yesu wa Biblia.

Mungu awabariki sana.

Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,

For Max Shimba Ministries Org,

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

April 8, 2016

View attachment 339259

Ni kweli ndugu Nabii Issa bin Mariam na Yesu unaemhubiri wewe ni vitu viwili tofauti kama vile zilivyo mbingu na ardhi.

Nabii Issa bin Mariam alikuwa mwanadamu wa kawaida na Nabii wa M/Mungu wakati Yesu unaemhubiri wewe ni full KINYONGA!! Mara awe Mungu aliepigwa na viumbe vyake, mara awe Nabii na mara awe binaadamu wa kawaida!!

Nabii Issa bin Mariam M/ Mungu alimlinda na kumuepusha dhidi ya njama za mayahudi za kutaka kumuuwa na kutundika msalabani maana mungu wake alijua kifo cha msalaba ni LAANA, Yesu unaemhubiri wewe alijilipua ili afe kifo cha msalabani ili iwe kama sadaka kwenu ya kubebewa madhambi yenu na pia alitaka kuthibitisha uwezo wa wanadamu wa kumchapa Mungu na kumuuwa katika kifo cha LAANA ( Msalabani)
 
Udhalimu ni mchakato wa kudumu hapa duniani! Hata sasa kinachoendelea Iraq, Syria nk. ni mifano iliyodhahiri. Na mingine itafuata kwa sababu imeandikwa!
 
Ligi tamu sana, mkuu Pasco ulileta hoja nzuri sana ila majority ya waarabu ni waislamu sasa ndugu zetu hawa wanaona kutajwa kwa waarabu kushiriki kwenye biashara ya utumwa wanaona ni kama kutusi uislam na ni kitu ambacho si kweli wengi wachangia kwa hisia kuliko reality
 
Msione kimya tunasoma na kuangalia upepo ,ila msiguse kwenye dini wala msihusishe na dini, maana huko kwengine ni kubovu kumeoza na kunazidi kuoza ,bora kusitiri tu maana kuingia kwenye nyumba ya ibada na vimini, mikwapa wazi, ni sawa tuwache huko.

Kuhusisha utumwa na au ndio uislamu mtakuwa mnasema ukiristo ndi chanzo cha umalaya ,waliofanya utumwa wakati huo waliowauza wenzao kwa kuwakamata na kuwapeleka sokoni inakuwaje mnunuzi ana kosa ,kufunga au kuwafunga minyororo ni kuwadhibiti wasikimbie baada ya kununuliwa, iweje leo wafungwa wanakuwa na pingu, utumwa upo hadi leo ,wapo wanaotumiwa kivita na biashara za ugahaba, ni watu wa dini zote wamo humo la kujiuliza kama Je dini zao zinayaruhusu hayo?

Kwa ufupi wale waliomo ndani ya dini hizo wamevunja sheria na kwa kuvunja kwao sheria haina maana dini yao imeridhia ,uovu uliotokea, kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, sasa nyinyi mnaozuka leo je mmekusudia kuwasaidia kubeba mizigo yao?
 
Back
Top Bottom