MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,607
Kama kuna binadamu ambae amenyanyaswa na kupuuzwa ni mtu mweusi. Mtu mweusi awe muislam, mkristo, au mpagani. Nimeshtushwa sana na utetezi wa manyanyaso ya mtu mweusi katika jamvi hili eti tu kwa vile huyo aliyemnyanyasa ni muislam au mkristo! Wewe mtu mweusi kweli unaweza ukajidhalilishs kiasi hicho Kisaka eti hate tea uislam au ukristo? Hawa weupe na wanjano bado wanaamini kuwa wewe ni inferior kwao. Sio binadamu mwenye uwezo wa kufikiri kama wao! Bado unashangilia eti utumwa na unyanyasaji wa mtu mweusi ni propaganda na chuki dhidi ya uislam au ukristo? Watu weupe walikuwa waislam au wakristo na waliyafanya hayo kwa baraka ya hizo dini zao! Hakuna mwaarabu au mzungu aliyezaliwa mbinguni! Wote ni binadamu wenye tamaduni na imani fulani ikiwapo hiyo kuwa mtu mweusi hafai! Wamekuwa na kuishi katika jamii iliyoamini hivyo toka papa hadi imam mkuu! Hawa ni binadamu na huwezi kuwatenganisha na utamaduni wao. Ndio kumekuwa na mabadiliko ya kimtazamo kuhusu mtu mweusi lakini ukweli unabaki pale pale kuwa mtazamo wa babu zao kuhusu mtu mweusi ulikuwa hasi! Narudia tena iwe kwa dini ya kikristo au uislam! Hivyo ukiuhalalisha unyama huo eti tu kwa kuwa wewe ni mwislam au mkristo ni kichekesho na dharau kwako wewe mwenyewe mweusi. Historia imevurugwa sana ili kuonyesha kuwa ukristo hauhusiki na utumwa as well as uislam. Ni uongo, maana hawa washenzi waarabu na wazungu ambao hawakuthamini utu wa mweusi walikuwa waislam na wakristo. Mabadiliko katika fikra na mitazamo ya kidunia na dini zake hayafuti huu ukweli. Kama kuna mchangiaji mwaarabu au mzungu anayetaka wewe mweusi eti ukubali unyama waliotufanyia kwa mgongo wa hizo dini mbili na wewe ukakubaliana nae basi jua anakudharau na ataendelea kukudharau! Mtu mweusi na akili zako anakwambia kuwa haya yanayotokea katika siasa Za leo ni sawa na utumwa aliofanyiwa babu na bibi yako na wewe unamuunga mkono eti tu kwa sababu una support uislam au ukristo! Akili yako iko sawa au na wewe bado ni mtumwa! Dharau aliyofanyiwa mtu mweusi, bahati mbaya bado inaendelea underground, haiwezi ikatetewa kwa misingi ya huo upuuzi mnaotaka kujivisha. Nenda bagamoyo, Zanzibar, na Goree island huko Senegal kisha urudi hapa na kutetea ushenzi huu eti tu kwa kuwa waliofanya ni wakristo au waislam. Ni aibu ambayo haijawahi kutokea kwa utu wa mtu uliofanywa na hao wakristo na waislam kwa babu na bibi zetu. Waache waislam waarabu na wakristo wazungu wabishane nani alitudharilisha kidogo na siyo wewe mweusi uliyedharilishwa na unaendelea kudhrilishwa kuwa mtetezi wa wadharilishaji. Ebu tuwe upande unaotustahili. Bahati mbaya sijui kama huyo Pasco na Mohamed Said nao ni weusi kama sisi au ni uzao wa hao wadharilishaji wazungu wakristo na waarabu waislam? Ebu tujivunie weusi wetu!
Katika kitu ninachojivunia hapa ulimwenguni ni kuzaliwa AFRICA. na Uafrika wangu hauathiriwi kwa chochote kile ambacho mkristo,mzungu, muislamu anasema au anafikiri kuhusu mimi.
Pamoja na ukweli kuwa mimi ni mkristo, mzizi wa msingi wa imani haufundishi chochote kuhusu hayo unayosema.
Bibilia imeacha loophole ya mtu yoyote kuitumia kwa kujinufaisha na ndivyo walivyofanya wazungu lakini ipo siku imewekwa ambayo KILA MWANADAMU anasimama mbele ya kiti cha hukumu to give account of what he did. Kupitia ukristo Makasisi, wamisionari, wachungaji walitumika kama vilainishi vya utumwa hili halifanyi ukristo kuwa batili ila hao ndio wanakuwa batili.
Kuna dimension ya mwanadamu, Mtu mweusi, mzungu, mchina,mwarabu au mhindi wote wanapaswa kuwa huru. Ukweli kuwa kuna watu wengi wako utumwani leo kuliko miaka hiyo hauufanyi utumwa ule uwe bora kuliko leo. Leo tunashuhudia WAAFRIKA WENZETU wanakuwa ndio Pioneer wa kuhujumu wa afrika wenzao na kukalia mali zote na kufanya maisha ya mamilioni kuwa mabaya kuliko enzi za utumwa baadhi ya maeneo.
Kuna waafrika wengi leo Tumeganda mawazo kama matokeo ya utumwa huo, Tunashindwa kuwa productive ktk dunia hii tukidhani haya ni matokeo ya utumwa. Kwa kutambua hilo Dr Martin Luther King ilibidi aandae speech nyingine "THE DILEMA AND THE CHALLENGE" kuwaambia watu weusi muda wa kulialia na kuchukia rangi flani umekwisha, iache iwei historia. Hitaji la mtu mweusi ni MINDSET Change, Wajiandae kuwa productive,creative, Performing work in high precision and accuracy. Because the time was coming when american/negro/african will not be judged by their color but The product of their character and mindset.
Tusipoteze Muda kulialia na vitu vilivyopita wakati leo hii Mtanzania mmoja anaweza kijilimbikizia trillion4 kodi za wananchi na kusababisha vifo vya maelfu ya watoto na wakina mama na watoto kwa ukosefu wa madawa, zahanati, chakula etc., Graduates wanalia ajira wakati wazungu, waarabu, wahindi wasio hata na diploma wanaingia nchini kufanya kazi nchini kwa rangi zao tu tunawaita experts wakati hawajawahi hata kufanya hicho kilichowaleta.
Huyu ni mbaya kuliko hata hao unaohubiri wachukiwe.
Waafrika wa sasa wengi wanajiweka utumwani kabla hata ya kutumikishwa, wanajibagua hata kabla ya kubaguliwa.