Mkuu Ilani, Yesu baada tuu ya kuzaliwa Bethlehemu, baada ya kutimiza 40, alikwenda kuishi Misri na kurejea kidogo Israel alipokuwa na miaka 12, kisha akarejea Misri hadi akiwa na umri wa miaka 30!. Misri ni nchi ya Kiarabu na ina lugha moja tuu, Kiarabu!. Hivyo it is a common sense mtu aliyeishi Misri kwa miaka 30, alizungumza lugha gani!.
Na pia kuwasaidia wasio jua, Yesu alivaa kanzu na kilemba kama wavaavyo Waarabu!, Wakistu wa kwanza wote walivaa kanzu na wanawake hijab!. Kanisa la kwanza limeanzia Arabuni, katika jiji la Constinapole!. Ndipo utawala wa Kirumi ukavamia na kuvunja hekalu hilo na kupora kila kitu na kuhamishia Vatican!, hivyo Vatican imenjengwa on a loot!.
Tukizungumzia ukatili wa binadamu, Warumi ndio walioongoza kwa ukatili na walikuwa na kikosi maalum cha mauaji kwa mateso, ikiwemo michezo kama ya gladiators, au kutupwa kwenye tundu la simba wenye njaa na kushangilia jinsi binadamu anavyorrauliwa etc!.
Mada yangu ni ukatili wa Waarabu kwenye biashara ya utumwa wa Unguja na Pemba na sio dini!. Kwa vile toka mwanzo niliweka angalizo la uwepo baadhi yetu ambao ni mufilisi, baadhi ya michango humu imenifundisha kuwa kumbe jf tunao members mufilisi wengi zaidi kuliko tulivyodhania!.
Mimi Kitu pekee ninachoweza kuwaambia ni Mwarabu ni mtu, na sio dini!. Uislamu ni imani na sio Uarabu!.
Ila nakiri kuna tatizo kubwa la inferiority complex miongoni mwa baadhi ya Waislamu humu kujishutukia, likisemwa baya lolote la Waarabu, kwao wanaona kama ni Iislamu ndio unabezwa!.
Mimi ni Mkristo Mkatoliki, nimeanzisha mada chungu nzima kuwabeza wazungu na hata kupingana na kanisa langu Katoliki, lakini sikuona watu wakitukana!. Kutukana na lugha za machukizo ni dalili ya kufilisika kihoja!.
Mimi ni Mkristo Mkatoliki lakini ninaikubali mahakama ya kadhi na nimeitetea sana humu!. Waislamu, kanisomeni
Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu
Pasco