Globu
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 8,659
- 2,227
Mkuu Battawi, kwanza asante kwa vitabu.
Kuhusu hizi propaganda ushahidi upo, sii ile milingoti ipo, enzi zile kulikuwa hakuna metal scanner, sasa kuna mobile scanner zile za containers bandarini, tulete, tuscan, propaganda hizo zifutwe, kwa sababu zamani ma Pharao, walizikwa na watumwa hai kule kwenye ma pyramids, wafalme walizikwa na mke anayempenda sana. Machifu walizikwa na mtu hai, India, mume akifa, ile siku anachomwa, mke shujaa, kukimbilia na kujitupa kwenye moto akiwa hai na kuteketea na mumewe etc. Hivyo japo ni propaganda, ila pia inaweza kuwa kweli, lolote linawezekana, kwani mtumwa alikuwa sii mtu ni bidhaa!.
P
Mkuu Paskali kwa hili la milingoti kuwa na vichwa vya watu ndani yake ni uongo uliopitiliza, kwasababu hivi karibuni hiyo milingoti unayoizungumzia ilivunjika, cha ajabu hapakuonekana hivyo vichwa vya watu kama tulivyolishwa hizo sumu za chuki na propaganda dhidi ya Waarabu.
Na ukitaka uhakika zaidi tembelea leo pale Forodhani Unguja ujionee kwa macho yako kwenye hilo jengo,haina hata ulazima wa kutafuta scanner, kwasababu bado ukarabati wa jengo hilo unaendelea.