Udini: Mwalimu Mkuu na wanafunzi wa Kikristo wakimbia shule Bagamoyo kuhofia maisha

Status
Not open for further replies.

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Mgogoro mkubwa umeibuka katika Shule ya Sekondari ya Bagamoyo mkoani Pwani kati ya wanafunzi wa Kiislamu na Kikristo na kusababisha Mkuu wa Shule hiyo, Bonus Ndimbo, kuikimbia shule na familia yake kuhofia usalama wa maisha yake.

Pia, baadhi ya wanafunzi wa Kikristo wamekimbia shule hiyo na kurejea majumbani mwao kutokana na vitisho wanavyopewa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salehe Mbaga, akizungumza na NIPASHE jana kwa simu, alithibisha kuwepo kwa mgogoro huo, lakini alisema hajapata taarifa za kukimbia kwa Mkuu wa Shule.

“Kama kweli Mkuu wa Shule amekimbia shuleni atakuwa amefanya vizuri kwa sababu alikuwa hatakiwi na wanafunzi,” alisema Mbaga ambaye hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi chanzo cha mgogoro huo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alipotafutwa, alisema mgogoro huo upo, lakini alikataa kutoa maelezo zaidi na hatua zilizochukuliwa yatolewe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Hata hivyo habari zilizopatikana shule hapo zinaeleza kuwa mgogoro huo ulianza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa serikali ya wanafunzi.

Wakati wa uchaguzi huo walijitokeza wagombea wawili wa nafasi ya Kilanja Mkuu wa Shule, Answal Abdul na Emmanuel Mmari ambao walikuwa wakichuana nafasi hiyo. Wote ni wanasoma kidato cha tano.

Chanzo cha habari kinaeleza kuwa kampeni zilipoanza wanafunzi wa Kiislamu ambao baadhi yao ni viongozi wa msikiti uliopo shuleni hapo, walianza kumpigia kampeni mgombea wa dini yao na wa dini ya Kikristo walianza kufanya hivyo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa wakati kampeni zikiendelea, inadaiwa Mkuu wa Shule aliwasihi wanafunzi wa Kiislamu waache kupiga kampeni kwa kufuata misingi ya dini.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Shule inadaiwa iliwakera wanafunzi wa Kiislamu ambao walichukua uamuzi wa kumuondoa katika kinyang’anyiro mgombea wa waliyekuwa wakimpigia kampeni, Answal Abdul na kubakia mgombea pekee Emmanuel Mmari.

Habari zinaeleza kuwa siku ya uchaguzi wanafunzi wote walishiriki, lakini wanafunzi wa Kiislamu licha kupewa karatasi za kupigia kura hawakuandika chochote katika karatasi hizo huku wanafunzi wa Kikristo wakipiga kura.

Baada ya uchaguzi huo, Mmari alichaguliwa kuwa Kiranja Mkuu wa shule hiyo.

Mkuu wa Shule hiyo, Ndimbo baada ya kukamilika uchaguzi huo alitangaza siku ya kuapisha viongozi wa serikali ya wanafunzi waliochaguliwa na ndipo mgogoro ulioanza.

Siku ya kuapisha viongozi hao, wanafunzi wa Kiislamu inadaiwa walimvamia Mkuu wa Shule na kumnyang’anya karatasi zilizokuwa zimeandika majina ya viongozi waliopangwa kuapishwa, hali iliyozua vurugu ambazo hata hivyo, baadaye zilitulia.

Mtoa habari watu amesematangu siku hiyo wanafunzi wa Kiislamu walianza kushinikiza Mkuu wa Shule ahamishwe na kwamba hawautambui uongozi wa shule uliochaguliwa na pia hawataki walimu Wakristo shuleni hapo.

Habari zaidi zinasema kuwa vitisho viliendelea na kuwa nyakati za usiku watu wasiofahamika walikuwa wakipita na pikipiki kuzunguka mabweni na shule.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi wa Kikristo waliamua kuondoka shuleni hapo kurejea majumbani hadi sasa kuhofia usalama wa maisha yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Samuel Saliyanga, alipoulizwa alisema bodi ya shule hiyo ilikuwa inakutana jana kutoa maamuzi ya suala hilo na kwamba yeye atapata taarifa kupitia kwa Afisa Elimu ya Sekondari.
CHANZO: NIPASHE
 
gazeti hili la NIPASHE serikali ingelipiga BAN kwa kueneza udini., habari hizi ni za uwongo kabisa.
 
gazeti hili la NIPASHE serikali ingelipiga BAN kwa kueneza udini.

Hivi hizi tabia za kinyume nyumbe zinawasaidia nini? Ukweli mnaita uongo! Uongo mnaita ukweli! Maandishi yanaenda kushoto! Tafakarini, dunia inawashangaeni!
 
Hata mimi nimeipata hii taarifa. Haya yote ni matunda ya udini wa JK.
 
ungefafanua vizuri mkuu ni shule gani ili nasi tuwawahi watoto wetu.
 
gazeti hili la NIPASHE serikali ingelipiga BAN kwa kueneza udini., habari hizi ni za uwongo kabisa.

Eti hiki chama ndio kina ndoto za kuongoza nchi yenye wakristo na waislamu.. Cha,a cha kidini kabisa hiki. Pumba**vu kabisa .. Mtatiro unaona ?
 
mbona umeweka nusunusu?
shule gani?
wilaya gani?
sio wote tunaweza kupata hilo NIPASHE tukasoma hiyo habari!

Katika kile kinachoonekana udini sasa umekomaa mwalimu mkuu pamoja na familia na wanafunzi wote wa kikristo wamekimbia shule mara baada ya ubaguzi wa kidini ulionyeshwa wazi shuleni hapo na jamii kwa ujumla na kutishia maisha yao kwa kuwambia wazi kuwa wao ni wakristo na wapo katika ardhi ya waislam ma wasipo fanya hivyo watauliwa.

Sasa kwa mtazamo wangu hakuna wa kuuzima huu moto ndani ya serikali hii kwa maana kwa njia moja au nyingine inawasaidia watawala katika divide and rule.

Source Nipashe
 
Hawa Christian watakuwa wanajishtukia tu na wameondoka kwa sababu zao binafsi. Wasisingizie ubaguzi wa kidini.
 
Hivi hizi tabia za kinyume nyumbe zinawasaidia nini? Ukweli mnaita uongo! Uongo mnaita ukweli! Maandishi yanaenda kushoto! Tafakarini, dunia inawashangaeni!........

Hapo kwenye bold ulitaka kumaanisha nini? Kwamba maandishi yanakwenda kushoto ni yale ya qurani? wewe hujui korani kwa nini maandishi yanakwenda kushoto.

Ningekufundisha ila kwa kuwa inaonekana huupendi uislamu wacha nikupongeze kwa kukupa "home work". Kwa kuwa kwenda kushoto inaonekana ni "kituko" basi nenda kwa ma injinia uwaambie wafungue nati yoyote kwenye engine au kifaa chochote kinachohusisha mechanics.

Waambie waifungue nati hiyo KWA KUIZUNGUSHA KWENDA KULIA!!!!! Nadhani itafunguka........na dunia "haitakushangaa".
 
Hawa Christian watakuwa wanajishtukia tu na wameondoka kwa sababu zao binafsi. Wasisingizie ubaguzi wa kidini.

ushawahi kuishi Bagamoyo mkuu?
huko ustaarabu wa dini ya Kiislamu ni sehemu ya maisha kwa asilimia kubwa ya vijiji, mimi nilidhani kwa nafasi yako kama muislamu mstaarabu ungekemea hilo badala ya kunyoosha kidole na kutoa hukumu.
 
Mgogoro mkubwa umeibuka katika Shule ya Sekondari ya Bagamoyo mkoani Pwani kati ya wanafunzi wa Kiislamu na Kikristo na kusababisha Mkuu wa Shule hiyo, Bonus Ndimbo, kuikimbia shule na familia yake kuhofia usalama wa maisha yake.

Pia, baadhi ya wanafunzi wa Kikristo wamekimbia shule hiyo na kurejea majumbani mwao kutokana na vitisho wanavyopewa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salehe Mbaga, akizungumza na NIPASHE jana kwa simu, alithibisha kuwepo kwa mgogoro huo, lakini alisema hajapata taarifa za kukimbia kwa Mkuu wa Shule.

"Kama kweli Mkuu wa Shule amekimbia shuleni atakuwa amefanya vizuri kwa sababu alikuwa hatakiwi na wanafunzi," alisema Mbaga ambaye hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi chanzo cha mgogoro huo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alipotafutwa, alisema mgogoro huo upo, lakini alikataa kutoa maelezo zaidi na hatua zilizochukuliwa yatolewe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Hata hivyo habari zilizopatikana shule hapo zinaeleza kuwa mgogoro huo ulianza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa serikali ya wanafunzi.

Wakati wa uchaguzi huo walijitokeza wagombea wawili wa nafasi ya Kilanja Mkuu wa Shule, Answal Abdul na Emmanuel Mmari ambao walikuwa wakichuana nafasi hiyo. Wote ni wanasoma kidato cha tano.

Chanzo cha habari kinaeleza kuwa kampeni zilipoanza wanafunzi wa Kiislamu ambao baadhi yao ni viongozi wa msikiti uliopo shuleni hapo, walianza kumpigia kampeni mgombea wa dini yao na wa dini ya Kikristo walianza kufanya hivyo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa wakati kampeni zikiendelea, inadaiwa Mkuu wa Shule aliwasihi wanafunzi wa Kiislamu waache kupiga kampeni kwa kufuata misingi ya dini.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Shule inadaiwa iliwakera wanafunzi wa Kiislamu ambao walichukua uamuzi wa kumuondoa katika kinyang'anyiro mgombea wa waliyekuwa wakimpigia kampeni, Answal Abdul na kubakia mgombea pekee Emmanuel Mmari.

Habari zinaeleza kuwa siku ya uchaguzi wanafunzi wote walishiriki, lakini wanafunzi wa Kiislamu licha kupewa karatasi za kupigia kura hawakuandika chochote katika karatasi hizo huku wanafunzi wa Kikristo wakipiga kura.

Baada ya uchaguzi huo, Mmari alichaguliwa kuwa Kiranja Mkuu wa shule hiyo.

Mkuu wa Shule hiyo, Ndimbo baada ya kukamilika uchaguzi huo alitangaza siku ya kuapisha viongozi wa serikali ya wanafunzi waliochaguliwa na ndipo mgogoro ulioanza.

Siku ya kuapisha viongozi hao, wanafunzi wa Kiislamu inadaiwa walimvamia Mkuu wa Shule na kumnyang'anya karatasi zilizokuwa zimeandika majina ya viongozi waliopangwa kuapishwa, hali iliyozua vurugu ambazo hata hivyo, baadaye zilitulia.

Mtoa habari watu amesematangu siku hiyo wanafunzi wa Kiislamu walianza kushinikiza Mkuu wa Shule ahamishwe na kwamba hawautambui uongozi wa shule uliochaguliwa na pia hawataki walimu Wakristo shuleni hapo.

Habari zaidi zinasema kuwa vitisho viliendelea na kuwa nyakati za usiku watu wasiofahamika walikuwa wakipita na pikipiki kuzunguka mabweni na shule.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi wa Kikristo waliamua kuondoka shuleni hapo kurejea majumbani hadi sasa kuhofia usalama wa maisha yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Samuel Saliyanga, alipoulizwa alisema bodi ya shule hiyo ilikuwa inakutana jana kutoa maamuzi ya suala hilo na kwamba yeye atapata taarifa kupitia kwa Afisa Elimu ya Sekondari.

CHANZO: NIPASHE
 
tatizo hapo kura za hapana zilikuwa nyingi kushinda za ndio, haya ndio yale yale ya chadema 2010 na sasa waislam wameamka.
 
Mgogoro mkubwa umeibuka katika Shule ya Sekondari ya Bagamoyo mkoani Pwani katiya wanafunzi wa Kiislamu na Kikristo na kusababisha Mkuu wa Shule hiyo, Bonus Ndimbo, kuikimbia shule na familia yake kuhofia usalama wa maisha yake.

Pia, baadhi ya wanafunzi wa Kikristo wamekimbia shule hiyo na kurejea majumbani mwao kutokana na vitisho wanavyopewa. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salehe Mbaga, akizungumza na NIPASHE jana kwa simu, alithibisha kuwepo kwa mgogoro huo, lakini alisema hajapata taarifa za kukimbia kwa Mkuu wa Shule.

"Kama kweli Mkuu wa Shule amekimbia shuleni atakuwa amefanya vizuri kwa sababu alikuwa hatakiwi na wanafunzi," alisema Mbaga ambaye hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi chanzo cha mgogoro huo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alipotafutwa, alisema mgogoro huo upo, lakini alikataa kutoa maelezo zaidi na hatua zilizochukuliwa yatolewe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Hata hivyo habari zilizopatikana shule hapo zinaeleza kuwa mgogoro huo ulianza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa serikali ya wanafunzi.

Wakati wa uchaguzi huo walijitokeza wagombea wawili wa nafasi ya Kilanja Mkuu wa Shule, Answal Abdul na Emmanuel Mmari ambao walikuwa wakichuana nafasi hiyo. Wote ni wanasoma kidato cha tano.

Chanzo cha habari kinaeleza kuwa kampeni zilipoanza wanafunzi wa Kiislamu ambao baadhi yao ni viongozi wa msikiti uliopo shuleni hapo, walianza kumpigia kampeni mgombea wa dini yao na wa dini ya Kikristo walianza kufanya hivyo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa wakati kampeni zikiendelea, inadaiwa Mkuu wa Shule
aliwasihi wanafunzi wa Kiislamu waache kupiga kampeni kwa kufuata misingi ya dini.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Shule inadaiwa iliwakera wanafunzi wa Kiislamu ambao walichukua uamuzi wa kumuondoa katika kinyang'anyiro mgombea wa waliyekuwa wakimpigia kampeni, Answal Abdul na kubakia mgombea pekee Emmanuel Mmari.

Habari zinaeleza kuwa siku ya uchaguzi wanafunzi wote walishiriki, lakini wanafunzi wa Kiislamu licha kupewa karatasi za kupigia kura hawakuandika chochote katika karatasi hizo huku wanafunzi wa Kikristo wakipiga kura.

Baada ya uchaguzi huo, Mmari alichaguliwa kuwa Kiranja Mkuu wa shule hiyo. Mkuu wa Shule hiyo, Ndimbo baada ya kukamilika uchaguzi huo alitangaza siku ya kuapisha viongozi wa serikali ya wanafunzi waliochaguliwa na ndipo mgogoro ulioanza.

Siku ya kuapisha viongozi hao, wanafunzi wa Kiislamu inadaiwa walimvamia Mkuu wa Shule na kumnyang'anya karatasi zilizokuwa zimeandika majina ya viongozi waliopangwa kuapishwa, hali iliyozua vurugu ambazo hata hivyo, baadaye zilitulia.

Mtoa habari watu amesematangu siku hiyo wanafunzi wa Kiislamu walianza kushinikiza Mkuu wa Shule ahamishwe na kwamba hawautambui uongozi wa shule uliochaguliwa na pia hawataki walimu Wakristo shuleni hapo.

Habari zaidi zinasema kuwa vitisho viliendelea na kuwa nyakati za usiku watuwasiofahamika walikuwa wakipita na pikipiki kuzunguka mabweni na shule.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi wa Kikristo waliamua kuondoka shuleni hapo kurejea majumbani hadi sasa kuhofia usalama wa maisha yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Samuel Saliyanga, alipoulizwa alisema bodi ya shule hiyo ilikuwa inakutana jana kutoa maamuzi ya suala hilo na kwamba yeye atapata taarifa kupitia kwa Afisa Elimu ya Sekondari.

CHANZO: NIPASHE
Sasa kwa mtazamo wangu hakuna wa kuuzima huu moto ndani ya serikali hii kwa maana kwa njia moja au nyingine inawasaidia watawala katika divide and rule..........

Mkuu wa Wilaya na OCD wanajua lilotokea na kupangwa. Hata hivyo haya ndio matokeo ya kuacha udini wa kijinga uendelee nchini.
Shule hiyo naifahamu na sasa inaelekea mwishoni mwa umaarufu wake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom