Labda hilo tatizo liwe siku hizi, miaka hii.
Nakumbuka wakati nasoma O-level pale Azania secondary(early 90's), Head master, second master, displini master na academic master walikuwa ni Wakristo.
Kulikuwa na chumba maalumu ambacho kilitengwa kuwa ni sehemu ya kusalia waislamu na kilikuwa kinatumika exactly kama msikiti. kutokana na ibada za waislamu kuwa ni mara tano kwa siku so chumba kile kilikuwa hakitumiwi na watu wengine na palikuwa panaitwa msikitini.
Kwa Wakristo walikuwa wakitumia madarasa kuendesha ibada ambazo zilikuwa zinafanyika kila siku nyakati za jioni na sometimes hall la shule lilikuwa linatumika kuendeshea ibada za kikristo.
Lakini hakukuwa na maneno wala tatizo lolote kama leo hii.