Udini: Mwalimu Mkuu na wanafunzi wa Kikristo wakimbia shule Bagamoyo kuhofia maisha

Udini: Mwalimu Mkuu na wanafunzi wa Kikristo wakimbia shule Bagamoyo kuhofia maisha

Status
Not open for further replies.


“Kama kweli Mkuu wa Shule amekimbia shuleni atakuwa amefanya vizuri kwa sababu alikuwa hatakiwi na wanafunzi,” alisema Mbaga ambaye hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi chanzo cha mgogoro huo.

Dah!! Huyo ndiyo kamanda wa Polisi anayeongea hayo!!!
 
Nchi inaelekea kubaya sana, vita hii ya kidini sasa itaanza kupiganwa kimya kimya ndani ya nyumba mlizopanga, ndani ya mashule, masokoni nk, huko sio Polisi wala JWTZ watakaoweza kupiga mabomu, JK and CCM hamkwepi laana hii.
 
huku tunakokwenda sasa naona itakua wanafunzi wa kikristo wana shule zao na waislam wana shule zao itakua vigumu kuwaweka shule moja...kazi ipo...
 
Labda hilo tatizo liwe siku hizi, miaka hii.
Nakumbuka wakati nasoma O-level pale Azania secondary(early 90's), Head master, second master, displini master na academic master walikuwa ni Wakristo.
Kulikuwa na chumba maalumu ambacho kilitengwa kuwa ni sehemu ya kusalia waislamu na kilikuwa kinatumika exactly kama msikiti. kutokana na ibada za waislamu kuwa ni mara tano kwa siku so chumba kile kilikuwa hakitumiwi na watu wengine na palikuwa panaitwa msikitini.
Kwa Wakristo walikuwa wakitumia madarasa kuendesha ibada ambazo zilikuwa zinafanyika kila siku nyakati za jioni na sometimes hall la shule lilikuwa linatumika kuendeshea ibada za kikristo.
Lakini hakukuwa na maneno wala tatizo lolote kama leo hii.
Mkuu kile chumba Bado Kipo pale kama msikiti....Juhudi kubwa zimefanywa na baadhi ya walimu Kuwanyang'nya waislamu Kile chumba.....
Mimi mwenyewe nilimla mitama Ticha mmoja aliengia na viatu katika kile chumba...
Mzee Kwayu alikuwa Mtu mzuri sana alikuwa hana matatizo yoyote ila kuna Vidampa vina chukiza ajabu sana
 
Hilo swali lako ni muhimu kujibiwa ili tuchangie tukiwa na uelewa mzuri.

Lakin jambo la msingi hapa ni funzo gani tunapata hapa; Hakuna umuhimu wa kuwa na haya makanisa ama misikiti kwenye taasisi za serikali kama shule!

Uvaaji wa miwani ya mbao kwenye mambo kama haya tutajuta uko tuendako!
Kweli kabisa mkuu, leo ndiyo tunasituka juu ya mambo haya.

Tunaanza kusituka kutokana na kukosa siasa bora za kuongoza nchi kama wamoja.
Mshikamano hakuna tena au ndio unazidi kutetereka.

Nimepita hapo Bagamoyo mara nyingi, na najua huo msikiti upo siku nyingi sana, we took ourselves for gtranted.
Leo vijana/walimu wanafarakana kutokana na udini.
Walimu/wanafunzi wanafikia hatua ya kukimbia academic campuses kutokana na mifarakano ya kidini.

Sasa ndo tunatatambua kuwa ile amani tuliyodhani tunayo kumbe sisi wenyewe ndio kuni za moto unaokuja.

Msikiti au Kanisa NDANI ya serikali ilikuwa kitu positive kwa miaka mingi,lakini leo ni source of conflict.

Inabidi tusali sana, kama hatujajua ni wapi tumepotoka.
La sivyo laana ya makosa tuliyofanya itatuhukumu kwa maka mingi ijayo.
 
Binafsi sioni tatizo na pia sio islamu. Shule niliyosoma ambayo awali ilikuwa shule ya mission na baadaye kutaifishwa na serikali enzi za mwalimu ina kanisa katikati ya shule. Lakini pia kama shule ya Bagamoyo imejengwa na serikali kwa ajili ya wanafunzi wote na ikajenga msikiti katika eneo la shule hilo ni TATIZO!


Nimesoma Tosamaganga Sekondary, kuna Kanisa zuri sana katikati ya Shule na wala halijawahi kuwa tatizo. Nachojua ni kuwa ikiwa shule ilitaifishwa kutoka ktk taasisi ya kidini basi wasingetaifisha hadi imani za waliokuwepo kwa maana kubadili kanisa au msikiti kuwa darasa au ukumbi wa mikutan au starehe. Ikiwa tunaaimini kuwa lengo la Dini ni Amani na utulivu basi hapo shida hamna. Labda kama Kanisa hilo au msikiti umejengwa na Serikali wakati wa ujenzi wa shule au baada. Na huo msikiti unaonekana ni mkongwe sana. Hivyo ulikuwepo toka kitambo.
 
Liko wapi tatizo la Msikiti ndani ya Shule ya Bagamoyo? Nani asiyejua kwamba PUGU SEKONDARI kuna kanisa kubwa la Roma? Mbona MARA Sekondari kuna Kanisa Kubwa la ROMA lakini hakuna Msikiti? Je umeshawahi kusikia mgogoro toka katika Shule hizi za Serikali.
MISIKITI na MAKANISA kwenye Shule za Sekondari wala si tatizo...Tatizo ni sisi tunaotumia muda wetu vibaya kwa kuzungumzia juu ya vitu hivyo bila ya kufanya tafiti za kutosha na kujiridhisha juu ya kile tunachokizungumza.
TAFAKARI.
 
wanaoandika habari kuhusu udini wawe makini sana. hata sisi tuaochangia humu tuwe makini ama sivyo tunaweza kuwa tunachochea moto katika tanuru la udini. madhara yake yatakuwa kwetu sote waliomo na wasiokuwepo.
 
Masyopakindi wa Magamba anaendelea kuchochea udini JF!
 
Mnanikumbusha kisanga cha shule ya sekondari ya Ndanda kule Mtwara!
 
ni vizuri majengo ya ibada yajengwe karibu na shule...kwa dunia hii ya leo wanafunzi wetu wanahitaji sana kumjua Mungu iwe ni dini yoyote ile
 
Hapo kwenye bold. Pole sana kwa kutoyajua maandiko matakatifu. Yaani tatizo lenu ninyi wakristo maandiko hamyajui, na hata kama mkifundishwa hamtaki kuukubali ukweli. Tukubaliane kitu kimoja.... Kwamba huwezi kuwa mkristo kamili bila kwanza kubatizwa (jibu ni ndiyo). Je, ubatizo maana yake ni nini? Jibu, ni kuzaliwa upya ama wengine watasema ni ondoleo la dhambi.... Tuanze na kuzaliwa upya. Hapa inamaana unaingizwa kwenye ulimwengu mwingine wa dini nyingine unakuwa mpya yaani unakuwa mkristo. Tuje na ondoleo la dhambi. Mtoto mdogo anapobatizwa maana yake tunamnwondolea dhambi...? Lakini mbona Yesu anasema watoto hawana dhambi? Maana yake hapa si kumwondolea dhambi bali tunampa dini mpya. Sasa tujiulize dini yake ya awali kabla ilikuwa inaitwaje? Jibu ni uislamu!!!! Kwa kawaida mtu anapozaliwa hutanguliza kichwa (anasujudu-means anakuwa muslim!!!). Na ndio maana mtoto akizaliwa kwa kutanguliza miguu inakuwaga hekaheka kweli mpaka madaktari huwa wanachanganyikiwa. kwa nini wanachanganyikiwa? Au kwa nini mila zingine hufanya tambiko mtu akizaliwa katanguliza miguu???
Ila kwa chuki ya uislamu ama kutopenda kujifunza maandiko watu watabisha mpaka mwaka mpya utaingia. lakini huo ndio ukweli. kwamba binadamu woooooote huzaliwa wakiwa waislamu na ndio maana huwa wanabatizwa ili kuwatoa kwenye dini yao (ya uislamu) kwenda dini hiyo ya ukristo.

Huo ndio ujinga wa Waislamu wengi, wanaamini wao wanaujua Ukristo kuliko Wakristo wenyewe lakini papo hapo wanamkashifu huyo Yesu anayeaminiwa na Wakristo. Chakushangaza, Mkristo au mwingine akizungumzia Uislamu au Muhammad kinyume na wanavyoamini basi ni vita na vurugu na kuharibu mali za Wakristo.

Najiuliza; kama Wakristo wangekuwa na tabia kama Waislamu hali ingekuwaje?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom