UDOM na PhD kwa wanasiasa. Nini chanzo cha mchezo huu katika elimu ya nchi hii?

UDOM na PhD kwa wanasiasa. Nini chanzo cha mchezo huu katika elimu ya nchi hii?

Hii nchi hua nasema..viongozi wake wanalaana..wanaitia unajisi hii nchi.

#MaendeleoHayanaChama
Wanacheza na kitu sensitive Cha elimu, hafu PhD wengi ni wabovu kiutendaji, wanazidiwa uwezo Hadi na bachelor, PhD with zero impacts in society's ni useless kabisa, Sasa wanasiasa wanaitumia hyo ka ngazi huku ni vilaza wa kutupwa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hafu huyo shingongo Kuna siku alikuwa anahutubia first year na kuwaambia yeye ni la saba ila Sasa hivi anasoma Masters yake Tumaini, hivi huyu mfano wake si una discourage elimu sahihi na sio hyo yake ya mchongo, no wonder udsm walimnyima admission ya master's.
 
Kwa kweli inasikitisha sana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Shigongo kuruka toka la saba hadi kupata degree...na ajabu chuo kilimtunuku ubest student[emoji119],,hapa ndipo ninapoishangaa elimu yetu watanzania[emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Hawabebi watu hovyo hovyo, Sasa madilu yenyewe alifanyiwa yake udsm na aliyemfanyia haja malizia kumlipa hela yake
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wee khaaaah sasa ndo nn iv lol
 
Walioanza siyo tu UDOM, ni UDSM na OUT. SUA sijawahi kuwasikia wakitoa digrii za kisiasa kwa wanasiasa. Kwa ufupi wanasiasa wanaharibu elimu ya nchi hii kwa kushirikiana na viongozi wa vyuo ambao wanapewa kuviongoza kisiasa. Cheo cha Vice Chancellor (VC) ni muhimu sana ktk uongozi wa chuo cha kitaaluma, bahati mbaya nafasi hiyo sasa wanapewa kutokana na uhusiano wao na wanasiasa. Hii ni kwa vyuo vyote vya serikali; ARDHI, UDSM, SUA, MUHAS, NM-AIST, Mzumbe pamoja na colleges zote! Nasema zote! Watu wanateuliwa hata bila uwezo na kupewa kwa sababu ya kupendana na wanasiasa. wengine hata uhusiano wao na wananchi mitaani ni kama 'wahuni' anaowasma ndg. Polepole. Cheo cha juu ni Chancellor ambacho pia kinashikiliwa na wanasiasa kwa vyuo vyote;
UD - Jakaya Kikwete
SUA - Sinde Warioba
Mzumbe -Mohammed Shein
MUHAS -Ali Hassan Mwinyi
ARDHI -Cleopa Msuya, sasa ni Othman Chande

Sasa wanasiasa wantaka PhD! Vyuo vinawasaidia kwa nguvu zote ili wapate Ph.D. Bahati mbaya sana UDOM imekuwa ni kinara wa kutoa digrii hizi. Nini Sababu kubwa?

Maoni yangu ni kwamba UDOM imekuwa ni chuo cha kufurahisha wanasiasa badala ya taaluma. UDOM ilianza vibaya na sasa inaendelea vibaya. ilianza na viongozi kutoka UD, waliokuwa wameshindikana kuishi na wenzao kijamii, wakapewa nafasi kirafiki, kisiasa. Hata wanafunzi wa digrii ya kwanza wanafundishwa kwa ubora wa matatizo tu, halafu tunashangaa kusikia wakiwa bize na ngono na waalimu wao. Kwa Ph.D Wanakiuka hata sheraia zao za ki-taaluma.

Jafo na Biteko wamepewa Ph.D bila kutimiza vigezo vya kitaaluma. Hawajafanya tafiti za kuwawezesha kupata Ph.D. pia hawajatoa machapisho kutokana na tafiti zao kama zilivyo taratibu za chuo. Mbaya zaidi, Ph.D zao zimeandikwa na wanataaluma hao hao wanaotakiwa kuwasimamia na wataandika machapisho kwamba ni ya wanafunzi wao wanasiasa, kumbe ni wao wenyewe waalimu. Hii ni aibu ya kitaaluma na ni aibu ya kisiasa.
Mwinyi ambaye hata kuongea amesahau anamuduje kuongoza baraza la chuo? Mabadiliko yanahitajika, SASHA nakuomba unisikie.
 
Hafu huyo shingongo Kuna siku alikuwa anahutubia first year na kuwaambia yeye ni la saba ila Sasa hivi anasoma Masters yake Tumaini, hivi huyu mfano wake si una discourage elimu sahihi na sio hyo yake ya mchongo, no wonder udsm walimnyima admission ya master's.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] std 7, ghafla degree? Sasa ordinary na advance level kasoma mda gan?
 
Mwinyi ambaye hata kuongea amesahau anamuduje kuongoza baraza la chuo? Mabadiliko yanahitajika, SASHA nakuomba unisikie.
Tena ktk chuo kilichobeba idara muhimu (afya) muhimbili, hii nchii ina futuhi hadi bas lol, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi jamani hawa wastaafu huwa hawachoki? Sinde Warioba, Cleopa Msuya JK na wengine, kwa nini msikatae hizo nafasi? Kwani hakuna maprofesa waliostaafu toka vyuoni kama kina Mwandosya, na wengine wakapewa hizo nafasi jamani?? Wanasiasa hawa sijui kama wanasaidia hivi vyuo sana
Just think of Ali H. Mwinyi, a person in his 90's; can't even remember his name yet still leads the university!! 'Wonders shall never end'
 
Back
Top Bottom