Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Muda mfupi baada ya Mwananchi aliyejitambulisha kuwa ni mmoja wa Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia JamiiForums.com kudai kuna changamoto ya hosteli katika chuo hicho, ufafanuzi umetolewa kutoka kwa Uongozi wa UDOM.
Awali Mdau huyo alisema baadhi ya Wanafunzi hasa wanaoendelea na masomo wamekutana na kadhia ya kulipia hostel lakini wanapokamilisha usajili wanaambiwa vyumba vimejaa na tayari fedha hairudishwi, hali inayowafanya wengi wao kuanza kubebana kwenye vyumba.
Pia Mwanafunzi huyo aligusia kuwa kuna baadhi ya michezo ya wasimamizi wa majengo kuonesha upendeleo au kwa maslahi binafsi kuwapa vyumba baadhi ya wanafunzi huku wengine wakikosa nafasi hiyo.
Kusoma hoja ya awali bofya hapa ~ Wanafunzi UDOM tunalipia gharama ya hosteli lakini ukikamilisha usajili unaambiwa vyumba vimejaa, tunalazimika kubebana
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Mdami amesema: “Hatujapata malalamiko kuhusu wanafunzi kukosa vyumba baada ya kuwa wamekamilisha usajili lakini kwa hayo yaliyosemwa kuhusu Wanafunzi kubebana ni wazi wametushtua kumbe michezo hiyo ipo! Nasi tutaanza ukaguzi kwenye mabweni yetu yote kujua kama Wanafunzi wanabebana.
“Tulichokuwa tunafanya ni kuwaruhusu wale ambao wanalipa ada kidogokidogo waweze kupata nafasi ya kupata vyumba, lakini kama hiyo michezo ya kubebana ipo basi tutakagua kwa kuwa kubebana kwenye mabweni ni kinyume nataratibu za chuo.
“Wao (Wanafunzi) kama wana changamoto yoyote walitakiwa kuiwasilisha kwenye Kurugenzi yao ya Wanafunzi ya hapa chuoni ili wasaidiwe. Idadi ya Wanafunzi waliojisajili haijazidi idadi ya nafasi za bweni zilizopo.
“Pamoja na hivyo kuna majengo ambayo yanafanyiwa ukarabati ili yaweze kutumikwa na Wanafunzi, awali majengo hayo yalitumiwa kama ofisi kutokana na sababu kadhaa lakini sasa ukarabati utafanyika ili yawe sehemu ya mabweni ya Wanafunzi.”