pia swala la vyoo hali ni mbaya sana kwa college ya Ualimu inasikitisha sana..Muda mfupi baada ya Mwananchi aliyejitambulisha kuwa ni mmoja wa Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia JamiiForums.com kudai kuna changamoto ya hosteli katika chuo hicho, ufafanuzi umetolewa kutoka kwa Uongozi wa UDOM.
Awali Mdau huyo alisema baadhi ya Wanafunzi hasa wanaoendelea na masomo wamekutana na kadhia ya kulipia hostel lakini wanapokamilisha usajili wanaambiwa vyumba vimejaa na tayari fedha hairudishwi, hali inayowafanya wengi wao kuanza kubebana kwenye vyumba.
Pia Mwanafunzi huyo aligusia kuwa kuna baadhi ya michezo ya wasimamizi wa majengo kuonesha upendeleo au kwa maslahi binafsi kuwapa vyumba baadhi ya wanafunzi huku wengine wakikosa nafasi hiyo.
Kusoma hoja ya awali bofya hapa ~ Wanafunzi UDOM tunalipia gharama ya hosteli lakini ukikamilisha usajili unaambiwa vyumba vimejaa, tunalazimika kubebana
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Mdami amesema: “Hatujapata malalamiko kuhusu wanafunzi kukosa vyumba baada ya kuwa wamekamilisha usajili lakini kwa hayo yaliyosemwa kuhusu Wanafunzi kubebana ni wazi wametushtua kumbe michezo hiyo ipo! Nasi tutaanza ukaguzi kwenye mabweni yetu yote kujua kama Wanafunzi wanabebana.
“Tulichokuwa tunafanya ni kuwaruhusu wale ambao wanalipa ada kidogokidogo waweze kupata nafasi ya kupata vyumba, lakini kama hiyo michezo ya kubebana ipo basi tutakagua kwa kuwa kubebana kwenye mabweni ni kinyume nataratibu za chuo.
“Wao (Wanafunzi) kama wana changamoto yoyote walitakiwa kuiwasilisha kwenye Kurugenzi yao ya Wanafunzi ya hapa chuoni ili wasaidiwe. Idadi ya Wanafunzi waliojisajili haijazidi idadi ya nafasi za bweni zilizopo.
“Pamoja na hivyo kuna majengo ambayo yanafanyiwa ukarabati ili yaweze kutumikwa na Wanafunzi, awali majengo hayo yalitumiwa kama ofisi kutokana na sababu kadhaa lakini sasa ukarabati utafanyika ili yawe sehemu ya mabweni ya Wanafunzi.”
Unaweza soma chuo cha kata ukapata ajira yenye mshara mkubwa halafu wewe ukiyesoma chuo cha international unazunguka na mabahasha yako miaka kibao unabaki kuwa winga tu.Chuo cha KATA.
mama yao aliwaambia wale kwa urefu wa kamba zao! Sasa hawajali hata wakilalamika!Kama wanafanyia kazi taarifa za wanafunzi kubebana kwanini wasifanyie kazi taarifa za kuwa kuna dhuluma katika utoaji wa vyumba, chanzo cha taarifa si kile kile ?
Mh! mpaka mabweni ya UDOM yanajaa maana yake kwa sasa chuo kinachukua wanafunzi wengi sana? Mana tulielezwa miaka hiyo kwamba chuo kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi elfu 40!Muda mfupi baada ya Mwananchi aliyejitambulisha kuwa ni mmoja wa Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia JamiiForums.com kudai kuna changamoto ya hosteli katika chuo hicho, ufafanuzi umetolewa kutoka kwa Uongozi wa UDOM.