MLETA maada unawazo zuri lakini wazo lako limekosa ushahidi/research ya kisomi. Chuo kikuu cha Dodoma ni kweli kimekusanya watu wenye elimu ya kiwango cha juu sana na wenye upeo wa hali ya juu katika kutizama mambo kwa upana wake na urefu. Wapo ma Professer, madoctor, maphd holders,n.k na hawa wote wanashiriki kwa nafasi zao katika kuzungumzia mambo mbalimbali inayohusu taifa letu kwa ujumla. Wanatoa maoni yao sehemu mbalimbali ikiwemo Makongamano, warsha,seminars, vyombo vya habari vingi tu vyakutosha Tanzania. Sasa wewe kama huwasikii ni bora ungejisemea nafsi yako kuliko kufanya inference without any scientific research for your argument. Unaporukia kwenye conclusion bila research ni dalili pia za kuonyesha wewe ni msomi/uelewana wako ni wa aina gani. Dhana ya Dodoma University kuwa chuo cha kata ni dhana ambayo wengi mnaimba kila siku bila kujua what are you saying. Kwakuwa hata nikikuhoji ni nini kinaifanya Udom kuwa chuo cha kata na ili chuo kiwe cha kata kina sifa gani wengi hamna majibu zaidi ya kurukaruka kama mmekanyaga siafu. DHANA ya kuwa Udom ni chuo cha kata imejengwa na watu wenye akili zao hasa kwa malengo ya kupotosha wasiochukua muda wao kufikiria yasemwayo hasa vijana wanaohitimu A level na collegus mbalimbali na wanaoitaji kujiunga na elimu ya juu. Lengo ni kutengeneza soko la vyuo vyao ambavyo kimsingi kusoma katika vyuo hivyo hata ukiwa 100% ya mkopo still maisha yako kama mwanafunzi yatakuwa tofauti na mwanafunzi wa udom. Hii ni kwasababu hasa ya miundombinu mizuri iliyopo chuo kikuu cha Dodoma. Pia intake ya chuo kile kwa taarifa tu kikikamilika uzuri per year kinaweza kupokea wanafunzi elfu kumi natano 15000 na chuo kizima kuwa na jumla ya wanafunzi elfu arubaini (40000) wote wakiwa wanapata kila mmoja malazi palepale. Takwimu hii ni hatari sana kwa ustawi wa vyuo vingine hasa vya private kwani kuna uwezekana wanao apply wasiombe kabisa vyuo hivyo. Mimi hii kwangu ni hoja dhaifu kwani Tcu kwa sasa andio taasisi inayowajibika kupangia vyuo wanafunzi na sio matakwa pekee ya wanafunzi. Kifupi chuo kile kama hujuma hazitoendelea kufanyika ili kisifanikiwe malengo yake few years ahead kitakuwa si kuwa ni bora tu Tanzania bali na Afrika kwa ujumla. Kuna hujuma nyingi sana nazijua kinafanyiwa UDOM lakini leo nadhani itatosha. Nawakumbusha tu kwamba Udom before 2015 Hospitali bora zaidi ya muhimbili itakuwa imefunguliwa ndani ya chuo hicho. Magonjwa yanayotibiwa India km Moyo yatatolewa huduma zako chuo kikuu cha dodoma. Nalo hili lina maelezo yake yanayopelekea kupakwa matope yasiostahili.