UDOM yazindua rasmi kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi (UDOSO 2026/27)

UDOM yazindua rasmi kampeni za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi (UDOSO 2026/27)

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
WhatsApp Image 2026-05-23 at 00.07.15.jpeg


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, leo Ijumaa tarehe 22 Mei 2026 katika ukumbi wa CIVE Auditorium, amezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO) katika hafla iliyowakutanisha viongozi wa chuo, Tume ya Uchaguzi, wagombea pamoja na wanafunzi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Prof. Kusiluka amesema uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi ni sehemu muhimu katika kujenga viongozi wa baadaye wenye maadili, uwajibikaji na uwezo wa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu. Aidha, amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha amani, ustaarabu na demokrasia vinaendelea kudumishwa ndani ya chuo.

WhatsApp Image 2026-05-23 at 00.07.14.jpeg


“Tunatarajia kuona kampeni zinazojengwa katika hoja na sera zitakazochangia maendeleo ya wanafunzi pamoja na ustawi wa mazingira ya kujifunzia chuoni.Vilevile, ni muhimu kutunza heshima ya chuo kwa kuzingatia sheria na katiba za uchaguzi ili kupata serikali bora itakayokiwakilisha vyema chuo,” amesema Prof. Kusiluka.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Serikali ya Wanafunzi, Bi. Najma Mdee, amesema tume hiyo imejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, haki na usawa kwa wagombea wote bila upendeleo wowote.

WhatsApp Image 2026-05-23 at 00.07.14 (1).jpeg


Aidha, Bi. Mdee ametoa shukrani za dhati kwa wagombea wote waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo na kuwataka kuzingatia umoja, amani na ushirikiano katika kipindi chote cha kampeni. Pia amewataka wagombea pamoja na wanafunzi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zote za uchaguzi.

Uzinduzi wa kampeni hizo umeambatana na hamasa kubwa kutoka kwa wanafunzi waliojitokeza kushuhudia mwanzo wa kampeni hizo, huku wengi wakieleza matarajio yao ya kupata viongozi wenye maono, uwajibikaji na uwezo wa kuwasemea wanafunzi katika kipindi kijacho.

WhatsApp Image 2026-05-23 at 00.07.13.jpeg
 
Back
Top Bottom