UDSM kuwekeza kwenye Kumbi za Mikutano na Flemu Mlimani City kuna tija ya Msingi?

UDSM kuwekeza kwenye Kumbi za Mikutano na Flemu Mlimani City kuna tija ya Msingi?

Inaitwa "Framenomics" hii ndiyo imekuwa bishara pendwa ya watanzia wa kada zote, wasomi wa PhD na wasiosoma, wakulima kwa wafanyakazi, maprofesa wa vyuo vikuu kwa walimu wa vidudu na hata makanisa na misikiti.

Si ajabu hata hata maeneo kama haya nayo tayari wana frame ili kuchanganyikiwa uchumi wa fremu
1. Msimbazi Centre
2. Magomeni Usharika KKKT
3. Magomeni Msikiti wa Kichangani
4. Lugalo Military base
5. Navy Kigamboni
6. Chuo cha Uhasibu Arusha

Inaonekana uchumi wa frame ndiyo ujuzi pekee ambao watanzania wanaupata na kuuelewa sana wanapotoka vyuoni
Sasa hivi kuna petro station inafungukiwa soon.
 
UDSM kuwekeza kwenye kumbi za mikutano na frame Mlimani City kuna tija ya msingi?

Nawasilisha kama Swali

Ahsanteni sana 😄
Hakuna chuo chenye udhahifu katika mipango kama UDSM. Jamaa wana maeneo mpaka huko bahari beac, ukiona miradi yao mpaka aibu. Pili kule bahari beach wana majengo hopeless kabisa na yasiyo na tija. Hawa wanyimwe ruzuku ndo akili itakaa sawa
 
UDSM kuwekeza kwenye kumbi za mikutano na frame Mlimani City kuna tija ya msingi?

Nawasilisha kama Swali

Ahsanteni sana 😄
Tija ya Mlimani City ni kubwa sana. Usiangalie kodi ambayo UDSM wanakusanya au wanapaswa kukusanya. Angalia kitu kinaitwa 'multiplier efect" ya uwekezaji wa Mlimani City.

Kabla ya 1990 pale palikuwa na petrol staion ya Agip tu. Huku eneo la Savei likiwa na Mlimani Park bar na upande wa Sinza na vijumba vidogo vya kupanga na wakazi wachache.

wa miaka zaidi ya 25 Mlimani City imezaa Mji wa Biashara pembezoni. Biashara nyingi zimeibuka, majengo makubwa mengine yamejengwa na atu wengine, ofisi za Serikali nazo ziko jirani yote yale pale ukitathmini mapato au mzunguko wa hela, itabidi umsifie developer wa hiyo idea ya Mlimani City.

Kama huwezi kunielewa kwa maelezo haya machache basi inabidi ukaombewe kwa akina Mwamposa
 
Back
Top Bottom