GE2025 UDSM yailaani UDASA kwa kukosa “Maadili ya Umma” baada ya kulaani uvunjifu wa haki nchini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hahahah bongo bila uchawa haiendi, ndio wasomi wa nchi ya kengez wanalisifia lichuo lao kila siku yani

Sijuagi hata lina msaada gani zaidi ya kuunda mafisadi wachanga wakakomae sisieme wakitoka
 
Hakuna Profesa hapa! Nikimlinganisha na Makamu mkuu wangu wa chuo Mathew Luhanga, na Mkuu wake wa taaluma Profesa Mayunga Nkunya (wote ni marehemu), nadhani ni mbingu na nchi.
 

Naona Jalalani kunawaka moto.

Baada ya tarehe 29, UDASA itaonfoka na wengi.
 
Masikini hana msimamo,
Na kipindi cha hivi katibuni wanapenda kutumia neno amani kama mwamvuli wa uovu, kila kitu tuna amani,
Amani wanaijua? Probably hatupo hata katika nchi hamsini zenye amani duniani
Njaa mbaya sana
 
Siku za huko nyuma, UDSM ilikiwa ni taasisi ya elimu hasa, iliyokuwa mstari wa mbele kutetea haki na kusimama kwenye misingi ya kitaaluma bila kupindisha.

Lakini siku hizi kwenye nafasi za utawala, yamejazwa machawa ambayo yamekigeuza chuo kikuu kuwa kama genge la machawa wanaosubiria teuzi. Kwa aina ya watawala wa hizi taasisi za elimu ya juu, elimu yetu itazidi kudidimia, kwa sababu wanaoongoza hivyo vyuo, wao wenyewe elimu haijawakomboa. Unajiita msomi, halafu unakuwa chawa. Hao ndio wanajiona kuwa wapo jalalani, na wanaamini uchawa ndio utakaowachomoa kutoka jalalani. Hawa wanadhalilidha sana taasisi za elimu ya juu.
 
Pale unapoambiwa profesa mzima msomi Anangisye aweka uprofesa mfukoni pale aliambiwa nje ya mlango wa UDSM kumewekwa madumu mawili ya asali, moja ya Tabora na ingine ya Katavi.

Profesa Anangisye kachagua asali ya Tabora.

What a pathetic academic.

Unbelievable.
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…