GE2025 UDSM yailaani UDASA kwa kukosa “Maadili ya Umma” baada ya kulaani uvunjifu wa haki nchini

GE2025 UDSM yailaani UDASA kwa kukosa “Maadili ya Umma” baada ya kulaani uvunjifu wa haki nchini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tamko la UDASA lilikuwa na rejea ya vifungu vya Katiba juu ya Serikali kuwa na wajibu wa kutunza na kudumisha ustawi wa wa wananchi kitu ambacho ni kweli! Sasa kukiwa na matukio ya utekaji Lukuki nchini na Serikali haioneshi jitihada zozote za kuwajibika kwa watu unasemaje limekiuka misingi ya kiutu tamko lao? Mbona UDSM halina ata kifungu kimoja cha KaTIBA au sheria kinachopingana na vifungu vya UDASA? Tamko la UD ni sawa na karatasi la kufungia maandazi.
 
Profesa kuwa chawa ni mbaya sana elimu aliyonayo haijamsaidia chochote...

Poor me!
 
UDSM ina mdomo ? Na hao UDASA sio UDSM ? Naona tumekuwa wepesi sana wa kupinga kilichosemwa badala ya kupinga issues na je UDASA walichosema kina makosa au kina uongo...;

Haya ni majibu mepesi sana kwa Taasisi ya Elimu kila mpingaji angeweza points zake kwanini kilichosemwa hakifai na upande mwingine kutetea walichosema na sio kuanza kupinga kwa aliyesema sio sisi wakati nyie hamjesema mnasema nini na Je nyie ndio NYIE au nyie ndio SISI wakati wao SIO ?
 
Yaani sasa hivi mtu ukikemea utekaji na mauaji na matukio mengine ya kuogofya yanayoendelea hapa nchini unaambiwa unasababisha taharuki au kuhatarisha amani?

Kwa hiyo kumbe kuilinda amani ni kutokukemea kabisa hali mbaya ya kiusalama iliyipo nchini sio?

Aisee nafikiri tunakoelekea ni pabaya zaidi ya ilipo Uganda...

....miezi sio mingi Tanzania itakuwa "pariah state".
 
Mapro"pesa" wa kibongo hata huwezi kujua wana amini nini yani? Mijoga hata isiyojua maana ya ku"profess" wanajua ni cheo tu kama cha koplo wa magereza majukumu yanawahusu hawajui

Ni bongo tu ndio utakuta Doctori wa "Philosophy" asiyekua na "Philosophy" yoyote bali makaratasi tu ya kumuongeshea mama na kujibandika majina makubwa ya kisomi baada ya kudesa miaka yote ya ujana wao! Wanahara hata kabla mtawala fomfoo hajaongea :RGBcheese: :RGBcheese:
 
Udasa wametumia uhuru wao

Uongozi wa udsm wametumia uhuru wao..

Sasa mbona mnapanua vidole badala ya kupanua ubongo!
Uongoz wa Udsm wamekosea maana wanasema wanafuata katiba , sheria za nchi na maadili ya taifa ila sidhan kama hayao wanayoyafuata yanaruhusu watu kutekwa au kuzuia watu kukemea uhalifu
 
Back
Top Bottom