Leo ndio leo ni draw ya kombe la mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali.
TUMU ZILIZOFAULU KUINGIA HATUA YA ROBO FAINAL UEFA NI
-FC BARCELONA
-ATLETICO MADRID
-REAL MADRID
-FC BAYERN MUNCHEN
-DORTMUND
-JUVENTUS
-MONACO
-LEICESTER
Draw itafanyika majira ya saa 8 mchana e.a.t
Huku dondoo zikionesha timu pendwa na UEFA au timu mlungula Real Madrid kubebwa kwa kupewa Leicester ambao ndio timu dhaifu kutokana na kufanya vibaya msimu huu.
Kuhusu Barcelona wao wanataka kupangiwa na timu mbili kati ya mahasimu zao R. Madrid au Bayern ili kulipiza kisasi kwa Arsenal ila la kusikitisha timu hizo zote hazitaki kukutana na FC Barcelona haswa R. Madrid
Na ile kauli ya Blatter kuwa kuna vimpira vyenye joto kwenye draw za UEFA naona inatimia tena
Tukitoka huko macho na masikio yote ya wapenda michezo Tanzania yapo kwa mchezaji wetu anayetuwakilisha vizuri nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta aliyeisaidia timu yake kuingia hatua ya robo fainali tukitaka kujua atapangiwa na timu gani maoni yangu ni heri akutane na Manchester United ili awaoneshe kuwa Tanzania tunaweza.