UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

Spain ina wachezaii mafundi sana aisee, sio viungo, sio Mabeki, sio Forwards...wote wanajua kucheza na mpira
Goli la dogo hatari kweli kweli...wenzetu wanawekeza mwenye youth hamna magumashi. Unaambiwa dogo 16 ukiamgalia sura unaona kabisa huyu mtoto. Njoo kwetu sasa mchezaji u20 anacheza mashinda manne 🤣🤣🤣🤣
 
Kawaida wale wabaguzi wa ufaransa walioshabikia yule mama kigagula ndio huwa washabiki wakubwa wa mpira, na hii ni ulaya yote huwa wako hivi, sasa hawa wa ufaransa walisahau kuwa timu nzima ni zaidi ya nusu wageni au weusi
Ndio maana hata Mbappe aliingilia na kuwaasa wananchi wasimpe serikali yule mama kigagula
Kwahiyo baada ya kushindwa uchaguzi, na sasa wamepewa makusudi msongo mwingine wa ufaransa kutolewa
 
SPAIN akili nyingi.

Kocha anajua nani anastahili kuingia na wapi, na ukizingatia wana wachezaji wanaojua kutulia na mpira, sio kubutua butua tu 🤣

Wanastahili kuchukua ubingwa hawa mafundi
 
Sio kweli, Final ni Final tu, wakikutana na Netherlands kazi ipo, ila wakikutana na England Spain itafunga magoli sio chini ya 4 na Fainali itaboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…