UEFA Zamani, sasa ni mfano tu.

UEFA Zamani, sasa ni mfano tu.

Daa kweli aise nikikumbuka mechi ya mtoano mwaka 2003, Manchester United ya akina Rio Ferdinand, Wes brown, David Beckham, Van Nestroooy, nevel brothers, Nick Batt, Fabian Bathez dhidi ya Real Madrid ya kina Claude Makele, Ronald9, Zinedine Zidane, Ruis Figo, Raul Gonzalenz, Roberto Carlos, Ika Casilas, kwa kweli nauona usiku wa Ulaya ukiwa unapoteza radha, Sasa tunaenda kumuangalia Mason Mount badala ya Frank Lampard, Jesse Lingard badala ya Ricardo Kaka, Jordan Henderson badala ya Genarro Gatuso, Michael Ballack Lucas Versques Karim Benzema badala Van Nestroooy, Andre Shevchenko, Didier Drogba, De Lima. Eti Leo Erick Bailly, Fikayo Tomori wanacheza UEFA wakati sisi tulizoea kuwaona Lucio, Ferdinand, Vidic, Soul Camplel, Allesandro Nesta, Jap Stam, John Terry, Ricardo Cavalho e.tc unaweza kuona hapa tulikuwa tunaenda kuangalia vitu viwili, kwanza Mpira wenyewe kwa ujumla, lakini pia Battle ya mtu mmoja na mwingine, yaani Zidane anavotoana jasho na Paul Scholes, au Genarro Gatusso( kaangalie mechi ya Nusu fainali 2003 Juventus anakufa 3-0 Santiago Bernabeu, halafu Madrid anakuja kufa 4-0 pale Turin), Rio Ferdinand anavokabana koo na Ronald9, nyie acheni bana, Sasa hivi unaweza ukawa unaangalia mpira ukajikuta hata hunconcertrate kwa sababu tu ya mbwembwe za Kidukulilo, miaka hiyo mpira unapigwa kika sekunde lazima ukoncerntrate!
Sahivi tunaangalia magic za Tammy Abraham, Marcus Rashford,Saka n.k
 
kumbe unajua kwamba ronaldinho kamzidi vyenga messi!!!...santiago bernabeu ni gaucho ndiye aliyepata standing ovation,messi mwenyewe anamkubali gaucho,kama gaucho hajamzidi chochote messi barcelona sasa messi anamzidi nini mume wa shakira!?
Nilivoanza kusoma nikawa naelewaelewa mwishoni nimegundua una matatizo
 
Mabeki wakazi washoka walimalizikia hapa
%2B255%20688%20550%20904%2020191016_175108.jpeg
 
kumbe unajua kwamba ronaldinho kamzidi vyenga messi!!!...santiago bernabeu ni gaucho ndiye aliyepata standing ovation,messi mwenyewe anamkubali gaucho,kama gaucho hajamzidi chochote messi barcelona sasa messi anamzidi nini mume wa shakira!?
Pia mwambie huyo kuwa mpaka sasa ni Ronaldinho ni Mchezaji pekee aliepata standing ovation pasipokucheza match.
 
Great robbery in football history ni Final Kati ya Chelsea na Barcelona from that moment I hate Barça dogs
Ile ndo ilikuwa uefa mkuu ..yani nguvu nguvu ..yule referee aliyechezesha ile gemu alikuwa anaichukia sana Chelsea..
 
Na ile ya Liverpool na Real Madrid?

Mwanzoni kabisa M.Salah anafanyiwa ukatili na Ramos
Ile final mbna ilikuwa nyepesi sana mkuu... ile kivyovyote Liver ilikuwa lazima afe tu ...hata Salah angecheza
 
Chotora ni sisi tunawaita hivyo, ila kwa wazungu hao ni blacks, hujiulizi Obama alikuwa anahesabika ni raisi mweusi??
Si ndio sasa ...Dihno atabaki kuwa Nabii wa mwisho kwenye soka, huyu messi ni balaa ila ni white basi lazima abwebwe tu..
 
Sahivi tunaangalia magic za Tammy Abraham, Marcus Rashford,Saka n.k
Aaah wapi, Marcos Rashford enzo hizo sidhani Kama angeweza hata kucheza EPL achilia mbali MANU, japo Tammy akipewa nafasi ya kutosha hapo Chelsea anaweza kuja kuwa bonge la mshambuliaji mwenye vinasaba vya washambuliaji wale wakatili!
Just imagine, Vidic yule, Ferdnand yule, Soul Cample yule, Cavalho yule, hawa madogo wangechezaje. Ulihitaji wanaume kwelikweli Kama kina Van Nestroooy, Emily Heskey, Drogba, Carlos Teves N.K kupambana nao. Soyo kina Fikayo Tomori!
 
Naunga mkono hoja. Mpira ulikuwa zamani siku hizi uhondo hakuna sana. Zamani hata timu ndogo zilikuwa zinaweza kugeuza matokeo mbele ya vigogo. Ngoja niwape mfano.

Usiku wa April 7 mwaka 2004, Katika mechi ya marudiano ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kati ya Deportivo La Coruna Vs Ac Milan katika uwanja wa Riazor nchini Hispania.

Mechi ya kwanza San Siro, Ac Milan bingwa mtetezi wa taji, alishinda 4-1.

Sasa mechi ya marudiano, Ac Milan ikiwa imetimia haswa, Dida, Cafu, Nesta, Stam, Maldini, Pirlo, Ambrossini,Gattuso, Shevchenko, Inzaghi na wengineo.

Deportivo aliishangaza dunia baada ya kuibuka na ushindi wa goli 4-0. Akina Diego Tristan na Walter Pandiani wakapeleka msiba jijini Milan. Ulipigwa mpira mwingi sana.

Siku hizi habari ni tofauti sana, ni nadra sana kwa timu ndogo kumkazia timu kubwa hasa kwa bingwa mtetezi.
 
Achana na hizo street football free style ambazo hata yule Dada wa hapa bongo anazifanya. Messi ni mwanaume kwenye mpira wa kileo labda kidogo na CR7 huwa anapambana. Shida ya gaucho ni kwamba alikaa kipindi kifupi sana kwenye peak ila jamaa alikuwa ni magitician. Hao wengine ni vijivulana.
 
Messi hata kina gatusso wawili wasingeweza. By the way sijui ni kwa nini huwa mnamsifia sana Genaro wakati alikuwa Wa kawaida. CR7 ndio alimpa ujiko huyo mchezaji
Kama messi hawezekaniki barca wasingekua wanatolewa kifala uefa consecutive, NB usiwasingizie wenzake (teammates) kwani wao wana zuilika
 
Madrid kachukua UEFA triple mara mbili.
Sema hiyo Real madrid yenu ya kina Ronaldo ilikuwa nyanya tu haikutamba Ulaya kama ya kina CR7
Madrid ya kina De Lima ilikuwa ya wanaume haswa. Na kipindi hicho timu pinzani hasa hizi kubwa zilikuwa ni za kiume haswa,so isingekuwa easy kuwika kama hii ya kina cr7 ambapo Madrid wao waliwekeza kisawasawa ilihali wapinzani wapo kawaida tu
 
Back
Top Bottom