Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Binafsi nadhani kuna haja ya jambo kufanyika ili kuongeza uelewa wa masuala ya kisheria baina ya watanzania. Najua sheria ni noble professional lakini hii haimaanishi ni wale waliosoma sheria tu ndiyo wanapaswa kuijua sheria, NO kila raia anatakiwa awe japo na uelewa wa msingi kuhusu masuala ya sheria (legal besic understanding).
Tukizingatia sheria ipo katika maisha yetu ya kila siku, Mfano; Makazini (kunasheria za kazi), Masuala ya ndoa (kuna sheria za ndoa), migogoro mbalimbali kama vile ya aridhi (kuna sheria za aridhi), mirathi (kuna sheria za mirathi) na masuala ya mikataba (kuna sheria za mikataba) n.k, hivi vyote ni maisha yetu ya kila siku kwaio ni muhimu japo kuelewa sheria ya masuala muhimu katika maisha yetu.
Kuongeza uelewa wa sheria kutasaidia watanzania kujua wajibu na haki zao, lakini pia itasaidia kuwafanya watanzania kuelewa pale haki zao zitakapovunjwa na nini wafanye na wapi waende na ndani ya muda gani ili kuweza kupata haki zao.
Ni aibu kuona watanzania wanashindwa japo kujua mpangilio wa mahakma (court hierarchy system) za Tanzania kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka ya rufaa, wanashindwa hata kujua mamlaka tofautitofauti (Jurisdictions) za mahakama izo, isitoshe wengi hudhani Kisutu ndio Mahaka kuu ya Tanzania (what a shame).
Pia asilimia kubwa ya watanzania hudhani kuwa sheria ni katiba, watu hudhani katiba ndiyo iliyosema kuua ni kosa, hudhani katiba ndiyo iliyosema wizi ni kosa n.k. Na, wengine hushindwa hata kutofautisha kati ya kesi za madai na jinai (unakuta mtu anadai ila anapeleka kesi polisi badala ya mahakamani) ,pia hushindwa kutofautisha kati ya mwanasheria na wakili ama jaji na hakimu na haya yote yana ashiria jamii yenye uelewa mdogo wa masuala ya sheria.
Nadhani kuna haja kubwa kwa majukwaa kama haya kufufua na kupanua wigo wa majadiliano kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria. Kwa kuwa dunia inaelekea kwenye teknolojia, hakuna haja tena ya mikutano ya kawaida ya kisheria kutoa elimu ya sheria. Badala yake, majukwaa kama haya yanapaswa kutumika zaidi ili kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi na kwa haraka.
Ni wazo tu lakini wadau