Nchi zenye sera hii zimejikuta zikikuza ile tabia ya watu kujitambulisha kwa majimbo yao na hivyo utaifa unakuwa shakani.
Ni rahisi sana watu kupata sababu za kuchukiana kuliko zile za kutaka kuwa kitu kimoja.
Mnapokubaliana kwamba udhaifu wa kila mmoja wenu unamezwa na umoja wenu maana yale ni rahisi hata huo udhaifu kupatiwa suluhisho ndani ya kuamini kwenu kwamba mpo salama mnapokuwa ni wamoja.
Ni kitu kipya kabisa, ni sawa na kuufanyia majaribio mfumo huo kwenye maisha ya watanzania.Hakuna kitu rahisi ni kujituma na kutumia vichwa ambavyo tunavyo. Mfumo tuliokua nao hautusaidii kwa kweli. Swala sio uhusiano wa jimbo na jimbo bali ni kwa kiasi gani serikali kuu itaziwezesha serikali za majimbo kupumua na kujiamulia mambo yao.
Hivi USA huwa unawatambuaje kwa majimbo yao, je ujerumani je Zambia au unaongea bila kufanya utafiti
Hebu tazama hatua kubwa za maendeleo kiuchumi waliyofikia hadi sasa! ...tuanze na hao iliyowataka.MIsingi ya hao uliowataja ni tofauti na ya kwetu, Wajerumani na Wamarekani ni watawala wenye historia fulani iliyowalazimisha wakubaliane na hali zao.
Tazama vipindi vya tv za China utaona wanavyosisitiza katika umoja. Tazama vikao vyao kila mwaka vinavyoongozwa na rais wao utaelewa maana ya umoja.
Nyerere aliua uchifu kwa makusudi ili tuwe kitu kimoja, Nigeria wanajitambulisha kwa majimbo na uchifu tazama jamii yao ilivyojaa hulka za kubaguana.
Haya mawazo yataishi hadi pale Tanzania tutakapobadili mfumo wetu. Tuombe Mungu hili like kufanikiwa.Hebu tazama hatua kubwa za maendeleo kiuchumi waliyofikia hadi sasa! ...tuanze na hao iliyowataka.