Ufafanuzi: Je, kuna Majimbo yatashindwa kujiendesha kwenye mfumo wa Majimbo?

Ufafanuzi: Je, kuna Majimbo yatashindwa kujiendesha kwenye mfumo wa Majimbo?

Nchi zenye sera hii zimejikuta zikikuza ile tabia ya watu kujitambulisha kwa majimbo yao na hivyo utaifa unakuwa shakani.

Ni rahisi sana watu kupata sababu za kuchukiana kuliko zile za kutaka kuwa kitu kimoja.

Mnapokubaliana kwamba udhaifu wa kila mmoja wenu unamezwa na umoja wenu maana yale ni rahisi hata huo udhaifu kupatiwa suluhisho ndani ya kuamini kwenu kwamba mpo salama mnapokuwa ni wamoja.

Hivi USA huwa unawatambuaje kwa majimbo yao, je ujerumani je Zambia au unaongea bila kufanya utafiti
 
Hakuna kitu rahisi ni kujituma na kutumia vichwa ambavyo tunavyo. Mfumo tuliokua nao hautusaidii kwa kweli. Swala sio uhusiano wa jimbo na jimbo bali ni kwa kiasi gani serikali kuu itaziwezesha serikali za majimbo kupumua na kujiamulia mambo yao.
Ni kitu kipya kabisa, ni sawa na kuufanyia majaribio mfumo huo kwenye maisha ya watanzania.
 
Hivi USA huwa unawatambuaje kwa majimbo yao, je ujerumani je Zambia au unaongea bila kufanya utafiti

USA nadhani unaijua historia yao na nadhani unajua hatufanani nao.

Hata wajerumani wapo kama walivyo kwa gharama ya vita na shida walizopitia zamani.

Msingi wa taifa letu upo katika umoja wa kitaifa tangu kabla ya muingereza kutupatia uhuru.

Muwe mnaisoma historia ya Mama Tanzania (kwa sauti ya Mbatia).
 
Kila kitu kinasababu na mazingira yake. Mfumo wa majimbo sio mbaya lakini kwa mazingira ya Tanzania ya sasa haufai. Sijui huko mbeleni.

Tanzania ni moja Kati ya nchi chache sana za kiafrika ambazo zimeweza kudhibiti kwa kiasi kikubwa suala la ukabila, ukanda na udini. Serikali ya majimbo inaweza kutupelekea huko.

Kwa jinsi lilivyowekwa hapa, watu wa Jimbo fulani watakuwa na utamaduni na dini zinazofanana. Hii ni mbaya Sana kwenye kufanya maamuzi maana yanaweza kuelemea kwenye mila na utaratibu wa watu hao.

Isitoshe, msingi wa CHADEMA kuanzisha serikali ya majimbo hauna mashiko. Je, changamoto za kiuchumi zinazolikabili taifa letu zimetokana na kutokuwa na majimbo? La hasha. CHADEMA wangesema watatilia mkazo usimamizi wa bajeti inayopitishwa na bunge.

Nchi za Marekani, Uchina na nyinginezo, zilikuwa na mazingira na sababu tofauti na hizi za CHADEMA. Mathalani Marekani yale majimbo 51 yalikuwa ni mataifa au mamlaka zilizojitegemea kabla ya kuunganishia kuwa taifa moja. Kila jimbo linajiamulia mambo yake na lina sheria zake.

Sisi hapa bado tunabaguana (kimyakimya) kuhusu makabila na dini zetu. Umajimbo utachagiza hali hiyo kwa uwazi zaidi.

Tuikatae CHADEMA
Tuukatae ubaguzi

Amani Msumari
Tanga (kwasasa Arusha kwa kazi maalumu)
 
MIsingi ya hao uliowataja ni tofauti na ya kwetu, Wajerumani na Wamarekani ni watawala wenye historia fulani iliyowalazimisha wakubaliane na hali zao.

Tazama vipindi vya tv za China utaona wanavyosisitiza katika umoja. Tazama vikao vyao kila mwaka vinavyoongozwa na rais wao utaelewa maana ya umoja.

Nyerere aliua uchifu kwa makusudi ili tuwe kitu kimoja, Nigeria wanajitambulisha kwa majimbo na uchifu tazama jamii yao ilivyojaa hulka za kubaguana.
Hebu tazama hatua kubwa za maendeleo kiuchumi waliyofikia hadi sasa! ...tuanze na hao iliyowataka.
 
Baada ya Kubadili Katiba, Nitapenda tuelekee huku ili kuharakisha maendeleo ya maeneo yetu nchini.
 
Hebu tazama hatua kubwa za maendeleo kiuchumi waliyofikia hadi sasa! ...tuanze na hao iliyowataka.
Haya mawazo yataishi hadi pale Tanzania tutakapobadili mfumo wetu. Tuombe Mungu hili like kufanikiwa.
 
Back
Top Bottom