Ufafanuzi kuhusu kanisa Katoliki kutokuwafanyia maziko ya kikanisa baadhi ya waamini wake

Ni hatari sana kwani viongozi wa dini husika wengi wao kanuni na taratibu za kwao hawataki kuziboresha kuendana na wakati husika wengi wamebaki kuwa"dogmatic and pre-emptive to all canonical laws and rules"
Mungu atusamehe......
Mmh! Lakini ukumbuke Kristu ni yule yule juzi, jana, leo na hata milele.Habadiliki-badiliki kama sie leo ni analogia kesho Digitali na kadhalika. Mungu au Yesu Kristu hafungwi na Wakati kwa sababu yeye ni mwanzo na mwisho - Alfa na Omega.
 
Kuna ule utaratibu wa kuwahimiza waumini wanapokuwa wamefiwa na wapendwa wao kwamba wawe wanatoa sadaka kila mara au kwa wingi ili mpendwa wao aliyetangulia mbele ya haki aweze kusamehewa dhambi zake na kupunguziwa adhabu huko aliko (?!).

Swali: Kama kanisa linaloundwa na wanadamu wameshindwa hata kumsamehe marehemu au wameshindwa kabisa kuwasikiliza ndugu na marafiki wa marehemu waliobembeleza viongozi wa kanisa ili mpendwa wao azikwe na kanisa, vipi sadaka zitakazokuwa zinatolewa kila mara na hao hao ndugu na marafiki ili mpendwa wao asameheme na kupunguziwa adhabu zitakuwa zinapokelewa na kanisa au la? Na kama zitapokelewa zitafanya kazi iliyokusudiwa kwa marehemu?

Pia kanisa kama kanisa bila kujali kama ni Roman Catholic au la, kwa nini liwe na utaratibu unaokinzana na hitaji la kusameheana unaopelekea kumsusa hadi maiti na hata kutokuwa tayari kusikia kilio cha ndugu na marafiki wanaobembeleza ndugu azikwe na kanisa?

Kwa mtazamo wangu huu utaratibu wa kanisa (RC na hata makanisa mengine yenye uraratibu wa aina hiyo) ungetazamwa upya na kufanya marekebisho yatakayoakisi dhana nzima ya kusameheana kama wanadamu.
 
Mmh! Lakini ukumbuke Kristu ni yule yule juzi, jana, leo na hata milele.Habadiliki-badiliki kama sie leo ni analogia kesho Digitali na kadhalika. Mungu au Yesu Kristu hafungwi na Wakati kwa sababu yeye ni mwanzo na mwisho - Alfa na Omega.
Yesu aliwahi kubadilika pale alipokuwa katika umbile la mwanadamu na kuzaliwa na bikira Maria.

Lakini pia kwani huyu Yesu alitoa maagizo hayo ya kususia marehemu aliyekuwa hasali au kutofanyia marekebisho katika miongozo ya kanisa iliyowekwa na wanadamu wenzetu miaka ya nyuma?
 
Umesema matarajio yako. Naomba nuulize hvi: Kwa nini hao ndugu wa marehemu hawakuona umuhimu wa kumshauri marehemu wakati wa uhai wake? Kusameheana au tuseme msamaha katika kanisa upo wazi siku zote na bila ubaguzi. Ni juu yako wewe unayehitaji kusamehewa kuuendea huo msamaha au kuufuata huo msamaha.Tusingoje mambo yakisha haribika halafu tunalalamika na kulaumu eti hatukupata msamaha. After all pengine kama marehemu angejaliwa kuzungumza angeweza kusema hauhitaji huo msamaha Marehemu ni ngangari achana na mambo ya kusamehe.
 
Ni Yesu huyo huyo ambaye alitoa mamlaka ya "Nendeni mkawabatize kwa jina la ...na lolote mtakalofunga duniani litafungwa hata mbinguni" samahani sina bible hapa ningekupa ni mistari gani nimenukuu inayotamka hivyo.
 
*_Anaandika Bernard Mukasa_*

UFAFANUZI KUHUSU KANISA KATOLIKI KUTOKUWAFANYIA MAZIKO YA KIKANISA BAADHI YA WAAMINI WAKE:

Jana mitandao ya kijamii nchini ilienea habari za kanisa kutokumzika tajiri mmoja kwa sababu alikufa katika hali ya "kinyumba" bila ndoa takatifu, na kwamba hakuwa mshiriki hai wa masuala ya kanisa.

Baada ya hapo kukatokea maneno mengi sana baadhi ya watu wakilishanbulia kanisa katoliki kwamba limekosea na linakosea kwa utaratibu huo, kwa maelezo mepesi kwamba suala la mtu kwenda mbinguni ni wajibu wa Mungu na siyo kazi ya kanisa kuhukumu (huenda wamesahau kwamba kanisa halijaihukumu roho ya marehemu bali limekataa kuuzika mwili wake tu ardhini).

Basi nimewiwa kufafanua kidogo niwezavyo kuhusu suala hili.

Karibu.......

Maziko ya kikanisa hayamfanyi mmoja aliyefariki aende mbinguni wala Jehanamu, bali yanamkumbusha mwombolezaji aliyebaki hai wajibu wake wa kuishi katika ushirika na kanisa ambalo ni mwili wa Kristo.

Kumzika au kutokumzika mtu kikanisa siyo jambo la kubeza ingawa ni kweli siyo linalompeleka marehemu mbinguni au motoni. Tukumbuke mwili wa marehemu unabaki ardhini. Kinachoenda mbinguni au motoni ni roho.

Lakini maziko ya kikanisa ni jambo lenye maana kubwa kutukumbusha tunaobaki duniani kwamba Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo na ambalo Kristo mwenyewe ndiye kichwa chake *(Waefeso 5:23)* linataka waamini tuige mfano wa mwenzetu aliyeishi na kumaliza maisha yake akiwa na ushirika na kanisa, ndiyo maana linafanya maziko ya kikanisa kama sherehe ya kumpongeza, kumuaga na kutuonesha mfano wake ili tuufuate. Na kama ameishi na kumaliza maisha yake bila shirika kamili na Kristo kwa njia ya kanisa ambalo ni mwili wa huyo Kristo, kanisa linakataa kumzika ili kutuambia kwamba mfano wake siyo ufaao kuigwa.

*Kwa nini ni muhimu Mkristo ashiriki maisha ya kanisa badala ya kuishi kivyakevyake tu?*

Kwa sababu Kristo alitaka hivyo. Wakati anawaaga mitume wake na wanafunzi wake aliwataka WABAKI KATIKA UMOJA, NA WAKAE HIVYO HATA ROHO MTAKATIFU MZINDUZI RASMI WA KANISA AKIJA AWAKUTE WAKIWA PAMOJA NA WAMOJA.

Tutakumbuka hata sala ya Mwisho ya Bwana wetu Yesu Kristo kabla hajatiwa mikononi mwa wauaji aliwaombea wanafunzi wake WABAKI WAMOJA kama yeye na Baba walivyo MMOJA *(Yohane 17:11)*.

Hivyo maisha ya ukristo ya kivyakovyako kwa kujitenga na kanisa Siyo mpango wa Kristo bali mpango wako binafsi. Siyo mfano tunaopaswa kuuiga wala kuuendekeza.

Kungia mbinguni kuurithi uzima wa milele kunamdai mtu atimize masharti makuu mawili (Luka 10:25-28):

1. Mapendo kwa Mungu
2. Mapendo kwa jirani.

Lakini huwezi kumpenda Mungu nusunusu. Yaani ukampenda kichwa na ukamchukia mwili. Kama kanisa ni mwili wa Kristo, wawezaje kusema unampenda Yesu (Mungu nafsi ya pili) na bado huna muda na mwili wake yaani kanisa lake? Mnafiki wewe.....!

Na kama hukumpenda Mungu (kichwa na mwili) na hukumpenda jirani, utawezaje kuurithi uzima wa milele? Ni vigumu.

Ni vema kujitahidi kuiepuka njia hiyo, ndiyo maana kanisa linautumia msiba kutukumbusha njia njema na kutuonya juu ya njia isiyo njema.

Kumbuka Yesu alisema atakayemkiri yeye Yesu (ambaye kanisa ni mwili wake) mbele za watu, Yesu pia atamkiri mbele ya baba, na atakayemkana Yesu mbele za watu Yesu pia atamkana yeye mbele ya Baba yake wa Mbinguni atakapofika mbele ya kiti cha utukufu wa Mungu (Mathayo 10:32-33).


*Mfano wa taratibu za ki-kanisa ambazo ukijitenga nazo siyo rahisi kuupata uzima wa milele ni huu:*

Ukiuishi ukristo wako peke yako nyumbani mwako huna nafasi ya kushiriki EKARISTI TAKATIFU au kwa maneno mengine KOMUNYO au wengine wanaita CHAKULA CHA BWANA au wengine wanaita MKATE WA BWANA.

Lakini Yesu mwenyewe alisema:

" *Kweli nawaambieni,* Msipokula huu mwili wangu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho"

*Yohane 6:53-54*

Zingatia vizuri hayo maneno ya mwanzo niliyoya-bold. Yesu anaanza kwa kusisitiza akisema *"Kweli nawaambieni,..*

Kwa nini Yesu alisisitiza?

Kwa sababu alijua kuna wengi watapuuzia suala la kukomunika (kushiriki chakula cha Bwana) wakidhani watakuwa na uzima wa milele kwa kuishi tu majumbani kwao bila kuja kanisani ambako ndiko chakula hicho hutolewa, wakijidanganya kwamba maadam waliishabatizwa (na wengine walibatizwa kwa maji mengi ya mto wote au bahari nzima) basi hiyo inatosha kwa wao kuurithi uzima wa milele.

Pia alijua wapo ambao wanaweza kuwa wanasali na kutoa sadaka kubwakubwa lakini wanaishi maisha yanayowafanya wasistahili kushiriki chakula cha Bwana, wakidhani ni rahisi kuupata uzima wa milele bila chakula hicho.

By the way..., hatuokolewi kwa matendo yetu. Tunaokolewa kwa neema (Waefeso 5:2).

Neema ya Mungu (yaani uwepo wa Yesu Kristo katika maisha na mazingira ya mwanadamu) haipatikani katika kujitenga wewe binafsi, bali inapatikana kwa kuungana na wenzako kwa jina la Yesu.

Yeye mwenyewe alisema:

"Wakutanikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao"

Mathayo. 18:20.

Na kama Yesu yupo katikati ya walio na umoja/ushirika katika yeye, basi neema ya Mungu inapatikana katika ushirika huo na siyo katika ubinafsi na kujitenga. Na kwa kuwa tunaokolewa kwa neema, ni rahisi zaidi kuokolewa tukiwa ndani ya kanisa kuliko kuokolewa tukiwa tumejitenga na mambo ya kanisa.

Kwa hiyo ndugu yangu..., ni muhimu sana kushiriki mambo ya kanisa. Na ni muhimu sana kwa kanisa kuonesha shukrani nanpongezi (appreciation) kwa yule anayekufa katika ushirika na kanisa, na kuonesha kuhuzunishwa na yule anayekufa akiwa hana shirika na kanisa.

Neno la Mungu linasema "Heri watu ambao wanakufa wakiwa wameungana na Bwana. Naam, watapumzika kutoka katika taabu zao, maana matunda ya jasho lao yatawafuata" (Ufunuo 14:13).

Mstari huo wa mwisho kunukuu ni muhimu sana kwako ndugu yangu. Kwamba ukifa umetengana na Bwana kwa matendo yoyote ikiwemo kutengana na mwili wa Bwana Yesu (Kanisa lake) una ole. Na ukifa ukiwa umeungana naye kwa matendo yoyote ikiwemo kuungana na mwili wa Bwama Yesu (Kanisa lake) una heri. Na amemalizia kwa kusema "matendo yako yataambatana nawe" hata baada ya kufa. Ndiyo maana umekufa, lakini sifa za jitihada za jasho lako tunazihubiri hata wakati wa mazishi yako. Na kinyume chake, sifa mbaya ulizoacha tunazikana hata baada ya kufa kwako kwa kuyakana mazishi yako.

Tumsifu Yesu Kristo.


Ben Mukasa.
 
Ni Yesu huyo huyo ambaye alitoa mamlaka ya "Nendeni mkawabatize kwa jina la ...na lolote mtakalofunga duniani litafungwa hata mbinguni" samahani sina bible hapa ningekupa ni mistari gani nimenukuu inayotamka hivyo.
Sawa mkuu. "....lolote mtakalofunga duniani litafungwa mbinguni....". Kuna mambo mengi sana yamekuwa yakifanyiwa review na kanisa na kuyabadilisha. Kumbe kuna uwezekano wa kanisa kuangalia upya msimamo huo na kuwa na msamaha "wa kibinadamu" kwa waliokufa na hivyo "kufungua" jambo hilo na hatimaye jambo hilo "kufunguliwa" mbinguni. Ni mtazamo wangu.
 
mbona una kichwa kigumu km jiwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…