Ufafanuzi kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu

Umesema MTU huwa a apewa pesa zote hiyo 30 na 50 mwisho wa formula zina maana gani?
 
Msilete huruma hewa. Watu wapewe fedha zao zote. Atakaechezea ataishi kama wazee wengine ambao hawakuwaikuwa kwenye mfumo wa ajira.
 
Una uhakika gani ana warithi na kama anao umejuaje anataka kuwaachia urithi wa fedha. Hicho kikokotoo kwanini hakiwahusu wabunge na mawaziri au wenyewe wanaishi milele
 
Kama wewe ulishindwa kuhandle pesa zako ni wewe, usigenerelize.
 
Akili za hivi ndo zinaua Taifa. Laana hsitawaacha kwa uwongo wenu huo.
1. Kama waliokuwa kwenye Mashirika walipunjika,ni nini kiliwafanya msiwarekebishie wao tuu ili walingane na wengine kwenye kikokotoo cha zamani?
2. Ni kwa nini mnapochukua pesa za wanachama kuwekeza kwenye miradi hamtoi taari za faida anayotarajia kupata mwanachama? Huo siyo ufisadi na uuwaji wa mifuko?
3.
 
Msilete huruma hewa. Watu wapewe fedha zao zote. Atakaechezea ataishi kama wazee wengine ambao hawakuwaikuwa kwenye mfumo wa ajira.
Dhima ya hifadhi ya jamii ni kukupa income security pale unapo patwa na janga mfano, Uzee, kupoteza ajira, kifo etc. Kupunguza dependency ratio, ukimfata mtu aliye staafu 2005 - 2018 kilio chao kikubwa waongezewe Monthly pension wamesahau kabisa kama walilipwa kikubwa mwanzoni.. Hifadhi ya jamii haipo kukupa wewe utajiri wala pesa za kujengea nyumba ipo kwaajiri ya kukupa income security.

Hiki kiinua Mgongo kuna baazi ya nchi hakipo mtu anapo staafu, anaanza kupata Monthly pension moja kwa moja.

Nyongeza tu, ukilipwa kiinua mgongo hakuna pesa unayo bakiza kwenye mfuko kwani kiinua mgongo ni zaidi ya kile ulicho changia.
 
Kama wewe ulishindwa kuhandle pesa zako ni wewe, usigenerelize.
😀😀! Mnaweka hisia.. Kifupi kama umeshindwa kuinvest 90%+ ya mshaara unao upata, unakuja kutegemea asilimia 5% ulio changia ndio utimize ndoto zako utakuwa ni Mpumbavu tu.
 
Nimekuja kugundua kuna umuhimu wa kuanzishwa somo la uhifadhi ya wajamii kwenye elimu yetu.

Sasa ulicho andika siwezi hata kukujibu, Embu pitia dhima za hifadhi ya jamii na nchi zingine huu mfumo uko vipi..!? Labda utajifunza uko.

Simply, Hifadhi ya jamii Haipo kwaajili ya kukupa utajiri, pesa ya kujengea nyumba kununua gari n.k hifadhi ya jamii ipo kwaajiri ya kukupa income security pale unapo poteza kazi/kipato iwe kustaafu, kuondolewa kazini, kuugua nk

Unacho takiwa kupambania ni serikali kuboresha maslahi na mishaara ya watumishi wake..
 
Huu ni ubinafsi Wa Hali ya juu, kwanini waajiriwa wapya ndo waumie almradi nyie mmetoka na kitita chenu kwa kikokotoo cha zamani? Kama kitu hakifai, tuseme hakifai siyo kusema kundi flani lianze na hii mpya. No.
 
Huu ni ubinafsi Wa Hali ya juu, kwanini waajiriwa wapya ndo waumie almradi nyie mmetoka na kitita chenu kwa kikokotoo cha zamani? Kama kitu hakifai, tuseme hakifai siyo kusema kundi flani lianze na hii mpya. No.
Jaribu kusoma kwa ufahamu. Kwanza mimi sihusiki kwenye kulipwa pension. Nilichosema nikuwa kama wanataka waanze mikataba mipya badala ya kubadilisha njiani. Ikianza mikataba mipya wale waajiriwa wapya watakuwa na nafasi ya kukubali mfumo wa pension ili waajiriwe au kukataa na kutoajiriwa. BTW, the way foward sidhani kama utaratibu utakuja kubadilika tena watu wawe wanalipwa fedha zote kwa mkupuo. Jaribu kufanya uchunguzi, nchi nyingi kabisa pension hulipwa kila mwezi kama mshahara. Cha kuzingatia ni kuwa malipo ya kila mwezi huwa yanakidhi mahitaji ya walipwaji kwa kiasi kikubwa
 
Kama wewe ulishindwa kuhandle pesa zako ni wewe, usigenerelize.
Akili za wanao Dai walipwe pesa zao kwa mkupuo tu, kusiwepo na pension ya kila mwezi hawana Tofauti na akili za MWANA MPOTEVU, kisa hiki kipo kwenye biblia kwenye kitabu cha Luka 15 11 - 24, nitanukuu hapo chini, Ndugu zangu kuna watu wanastaafu na mishaara ya 700k hawa ukisema uwape Full pension, pension yao haiwezi zidi hata Million 50. haya wapewe hizo million wakajifie mbele pesa zikiwaishia wa-anze kuwa tegemezi..!? tuongeze dependency ratio

( FORMULA YA FULL PENSION : 1/580 × APE × MPS )

Nukuu ya mwana mpotevu :

Luka 15:11-24
Neno: Bibilia Takatifu
Mwana Mpotevu

11 Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu aliyekuwa na watoto wawili wa kiume. 12 Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Basi huyo baba akagawanya mali yake kati yao.

13 “Baada ya muda mfupi yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo akaenda nchi ya mbali akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa. 14 Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote naye akawa hana cho chote. 15 Kwa hiyo akaomba kibarua kwa raia mmoja wa nchi hiyo aliyemtuma shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Akatamani kujish ibisha kwa maganda waliyokuwa wanakula nguruwe, wala hakuna mtu aliyempa cho chote cha kula.

17 “Hatimaye akili zikamrudia, akasema, ‘Ni watumishi wan gapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza nami hapa nakufa kwa njaa! 18 Nitaondoka nirudi kwa baba yangu nikamwambie, ‘Baba, nimetenda dhambi mbele ya Mungu na mbele yako. 19 Sistahili kuitwa mwanao tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’ 20 Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanae, akamkumbatia na kumbusu. 21 Yule mtoto akasema, ‘Baba, nimekosa mbele ya Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.’ 22 Lakini baba yake aka waambia watumishi, ‘Leteni upesi kanzu iliyo bora mumvalishe. Pia mvalisheni pete na viatu. 23 Kisha mleteni yule ndama aliyenona mkamchinje; ili tule tusherehekee. 24 Kwa maana huyu mwanangu alikuwa amekufa, na sasa yu hai tena; alikuwa amepotea na sasa amepatikana.’ Basi wakaanza sherehe.
 
Ukisha lipwa kiinua mgongo hakuna pesa yako inayo baki kwenye mfuko.
kama hakuna pesa inayobaki, kuna haja gani ya kucalculate kwa hizo formula wakati inajulikana umechangia 20% kwa miaka kadhaa??? balance si inaonekana?
 
miezi ya uchangiaji inajibu swali lako
 
ambacho hufafanui ni kuwa hicho kiinua mgongo unalipwa ASILIMIA 33 unapostaafu na ASILIMIA 67 inalipwa ndani ya miaka 12.5 baada ya hapo.. Ikipita miaka 12.5 unakuwa ushamaliza kiinua mgongo chako. baada ya hapo kama utakuwa bado hujafa, mfuko wa jamii itaendelea kukulipa ingawa pesa yako inakuwa imekwisha
 
Wanajeshi si nao ni watumishi wa umma mbona mmewatoa kwenye hiki kikokotoo kipya tokea mwanzo.... mpaka na ndugu zetu polisi wanaomba kutolewa kama ni kizuri.
Ibara ya 13(2) ya Katiba ya 1977 inasomeka “Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yeyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
 
Eti waulize waliostaafu miaka 10 iliyopita kama Wana hela yoyote!? Kwa hiyo kama wanazo au hawana mi inanihusu nini!? Nmeishia hapo kusoma upuuzi
 
maelezo, uchambuzi, ufafanuzi na elimu mujarabu sana hii, dhidi ya upotoshaji wa makusudi wa watu wachache wasioelewa vema dhima na lengo la kikokotoo hiki.....

thank you very much gentleman DOMINGO THOMAS
 
Mtoa mada wewe Ni mpumbavu
NB: mpumbavu sio tusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…