Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Msilete huruma hewa. Watu wapewe fedha zao zote. Atakaechezea ataishi kama wazee wengine ambao hawakuwaikuwa kwenye mfumo wa ajira.Kuna makundi makuu mawili kwa sasa hapa nchini
1.Kuna watumishi (Wastaafu watarajiwa)
2.Kuna wastaafu waliokwishalipwa Mkupuo na sasa wanapokea monthly pension
Tafuteni makundi yote mawili mtaona hoja zao ni tofauti.
Kundi la Kwanza linataka mkupuo mkubwa.
Kundi la pili ambalo walipokea mkupuo mkubwa wanalalamika kuhusu udogo wa monthly pension.
Kila siku wanasema walau pensheni ya kila mwezi iongezeke.
Ukiamua kwa hisia,utajikuta unatengeneza kundi kubwa la ombaomba siku za baadaye!
Una uhakika gani ana warithi na kama anao umejuaje anataka kuwaachia urithi wa fedha. Hicho kikokotoo kwanini hakiwahusu wabunge na mawaziri au wenyewe wanaishi mileleBosi nchi hii ina wajinga wengi sana. Badala ya kutafuta ufumbuzi kwenye kuhakikisha watanzania wanapata elimu ya fedha na uwekezaji mapema minitu unakuta ina midevu inasema kikokotoo kibaya. Ukiuliza ubaya wake nini eti apewe hela zote, ukiuliza ukipewa eti nikifa niwe nimechukua hela yako, ukiukiliza je kwani ukiwa unapata kila mwezi ukifa hela yako si watapewa warithi yanasema oh mi nataka hela yangu yaani ni full ujinga mno.
Hakuna sehemu kwenye formula kuna 30 na 50.Umesema MTU huwa a apewa pesa zote hiyo 30 na 50 mwisho wa formula zina maana gani?
Kama wewe ulishindwa kuhandle pesa zako ni wewe, usigenerelize.Mie huwa nashangaa watu wanachanganya mada. Baada ya kukusoma unachozungumzia ni umuhimu wa ama kulipwa fedha zote au kubakiza upewe pension.
Kwa uelewa wangu mifuko ya jamii iko kwenye kundi la bima. Unawekeza ili baadaye upate mpaka hapo maisha yatakapokuchukua.
Najiuliza, kama mtu amefanya kazi miaka 30 hakuje nga, hana shamba, hana biashara. Anawezaje kupewa fedha za mkupuo ndio aanzishe mambo hayo akiwa hana ujuzi wowote? Nadhani ni ngumu. Watu wanapewa fedha wanakuwa wehu (sio wehu wa kurukwa na akili). Wakishtuka zimeisha. Au wanaazisha tu miradi ambayo haidumu maana matumizi yanabaki yaleyale na hana usimamizi bora. Hakuna mradi watakaoanzisha utakaopata faida zaidi ya pensheni ya kila mwezi.
Ni heri pensheni wangepigania pensheni kuongezwa kuliko kulipwa fedha zote ili zikiisha wasibaki na kitu.
Jamani, nayaona nina miaka 5 baada ya kustaafu. Pensheni nzuri jamani.
Nalipongeza andiko lako.
Akili za hivi ndo zinaua Taifa. Laana hsitawaacha kwa uwongo wenu huo.Watumishi wa umma wengi sasa hivi wanafuatilia issue ya kikokotoo cha mafao yao ya baadaye.
Hata hivyo wapo watumishi wa umma ambao wapo kimya kuhusu kikokotoo labda kwa kuwa miaka yao ya kustaafu bado iko mbali saaana.
Wapo wengine wanaoongea kwa kuwa kikokotoo kipya kimewagusa kwa namna moja ama nyingine.
Kama Mwanazuoni wa Hifadhi ya Jamii, Naomba nifafanue baadhi ya mambo kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu.
Kikokotoo kipya cha:
1/580 × APE x PoS x 12.5 x 33%
Na kikokotoo cha zamani cha LAPF na PSPF yaani
1/540 × LAS x PoS x 15.5 x 50%
(LAS = Last Annual Salary na PoS = Period of Service)
APE = Annual Pensionable Emoluments
1/540 = Acrual factor
15.5=Commutation Factor
50%=Commutation Rate
Usipojifunza jinsi ya vikokotoo hivyo viliundwa utashindwa kuishawishi Serikali kipi kirekebishwe na kwa nini. Ni kama unakuwa unaongea kitu usichojua.
Kusema Serikali ikulipe pesa yako yote ni ujinga ujinga mkubwa saaana ambao watumishi wa umma wenye ujinga ndiyo watapromoti hoja hii.
Vikokotoo vyote hivyo vina uzuri na ubaya wake. Kama wewe siyo mchambuzi utashabikia tu lolote bila kujua vizuri matokeo yake.
Sheria za Kikokotoo cha PSPF na LAPF kilikuwa na mapungufu meengi sana. Bahati mbaya mapungufu hayo hakuna watalaam wanaoyadadavua sasa hivi.
Wanachama waliokuwa PSPF na LAPF kikokotoo chao kilikuwa na mapungufu kibao ukiacha upande wa Kiinua mgongo tu vipengere vingine vyote havikuwa vizuri.
Kikokotoo cha wanachama waliokuwa PPF, GEPF na NSSF kilikuwa hiki hapa:
1/580 × APE x PoS x 12.5 x 25%.
(APE = Annual Pensionable Emoluments na PoS = Period of Service/Contribution)
Makundi haya ya wanachama ambao ni zaidi ya 81% ya wanachama wote wa mifuko iliyokuwepo kwao kikokotoo kipya kimewaongezea mkupuo wa mafao waliokuwa wanapata kwa 8%. Yaani iko hivi:
1/580 × APE x PoS x 12.5 x 25%
Hapo kwenye asilimia 25 kwa kikokotoo kipya wao imekuwa 33% ambayo ni ongezeko la 8%.
Sasa watumishi wa umma wote wamepewa kikokotoo kimoja bila kujali wako idara ipi.
Zamani (2004 hadi 2018) waliokuwa Serikali kuu na serikali za mitaa yaa LAPF na PSPF walikuwa wakilipwa Mkupuo Mkubwa saaana kwa Kikokotoo hiki hapa cha 1/540 × LAS x PoS x 15.5 × 50% kwa sababu kikokotoo hicho cha Serikali Kuu kilizingatia Last Month Salary
Na wale wa sekta binafsi chini ya NSSF na PPF walitumia kikokotoo kilichozingatia Wastani wa Mshahara wa miaka mitatu.
Kwa hiyo tunafanyaje? Tuchukue kikokotoo cha serikali Kuu kiwe cha wanachama wote wa sekta binafsi na umma halafu mfuko uishiwe nguvu kulipa mafao baada ya miaka 5???
Au tuchukue kikokotoo cha sekta binafsi kilichokuwa kinatumika NSSF, PPF na GEPF kiwe cha wote na kiboreshwe kidogo from 25% to 33% na mfuko uweze kujiendesha kwa miaka mingi???? Kipi bora??
Maamuzi yaliyochukuliwa na serikali mwaka 2018 yalikuwa ya kuwatazama wanachama 81% waliokuwa mifuko ya NSSF, PPF, na GEPF ili wafanyakazi wote wafanane kwenye mafao ya uzeeni.
Yaani serikali ililenga kufanya pensheni ya kila mwezi na malipo ya Mkupuo yawe na usawa pamoja na watumishi wa umma waliokuwa na kikokotoo kikubwa kwa kutazama factors za uendelevu wa mfuko mpya wa PSSSF.
Mwaka 2014 hadi 2018 wastaafu wa serikali Kuu waliokuwa chini ya PSPF walikuwa wamefikia mahali Papaya sana hadi mafao yao yalikuwa hayapatikani tena kutokana na PSPF kushindwa kujiendesha kwa sababu ya madeni makubwa ambayo serikali ilikuwa inadaiwa tangu 1999.
Watu waliokuwa wanastaafu miaka hiyo 2014 hadi 2018 walikuwa wanaambiwa wasubiri. Walisubiri saaana mpaka Mwaka 2018 December mifuko ilipounganishwa zikachukuliwa fedha za LAPF na PPF kuwalipa wastaafu waliokuwa wamekaa mtaani bila mafao kwa zaidi ya miaka 2 hadi 3 bila mafao.
Ni bahati mbaya saaana kwamba tuna wanasiasa na wanachama wanaosahau mapema tulipotoka.
USHAURI MBAYA NI HUU
Kudai Kwamba wastaafu walipwe pesa zote (100%) na waendelee na maisha yao. Huu ni ushauri mbaya saaana kuishauri serikali.
Kwamba kwa nini wastaafu wawekewe pesa za kulipwa kila mwezi kidogo kidogo? Hili ni swali la kitoto litokanalo na kutojua maana ya Society Protection
Ukisikia mtumishi wa umma anadai hataki pensheni ya kila mwezi anaomba alipwe pesa zake zote aendelee na maisha yake ujue kuwa huyo siyo mtumishi wa umma. Ni Mjasiriamali.
Na Bahati mbaya watumishi wa umma asilimia 95 siyo wajasiriamali. Ni wategemezi wa mishahara ya kila mwezi.
Akilipwa pesa yote halafu ikaisha social economic crisis itakayotokea katika jamii ya wazee itazidi ile ya wazee wa East Africa Community waliovua nguo barabarani wakidai Pension ya kila mwezi.
Ukitaka kujua utamu wa pension ya kila mwezi kabla hujashauri utaratibu wa pension ufutwe, nakuomba ukawaulize waliostaafu miaka 10 iliyopita.
Waulize kama pesa kubwa ya kikokotoo kikubwa walicholipwa 2010 mpaka leo pesa ipo?
Kawaulize Tegemeo lao kuu la pesa ya kila mwezi ni wapi? Hawa wazee ukitaka ukosane nao ondoa utaratibu wa pension ya kila mwezi.
Waulize utamu wa pension na utamu wa kiinua mgongo ni kipi kitamu zaidi.
Kawaulize wazee waliostaafu 2010 kati ya Pension na Burungutu la pesa unayopewa ukistaafu ni kipi kiongezwe kiwe kikubwa?
Waulize kati ya Pension ya kila mwezi na kiinua mgongo(gratuity) wanashauri kipi kiongezwe?.
Ukiwauliza waliostaafu miaka 10 iliyopita wao wanaomba pension iongezeke iwe kubwa saaana.
Ukiwauliza wazee wastaafu Watarajiwa kipi kiongezwe, wao wataomba kiinua mgongo ndicho kiongezwe.
Hii inatokana na kwamba ni vigumu sana mstaafu mwenyewe tarajiwa kupendekeza alipwe nini kama hajafika huko uzeeni.
Wazee waliolipwa mafao kwa kikokotoo cha LAPF na PSPF miaka 5 iliyopita asilimia 90 yao tegemeo lao kuu kwa sasa ni pension ya kila mwezi pamoja na kwamba walilipwa kikokotoo kikubwa.
Hoja nyingine inayopotoshwa ni hii kwamba mstaafu analipwa pesa fulani na nyingine inabakia kwenye Mfuko kwa ajili ya kulipwa kidogo kidogo kama pension.
Huu nao ni uongo wa Mtaani umeshageuzwa kuwa kama ukweli.
Ukweli ni kwamba Hakuna pesa inayobakia kwenye Mfuko.
Mstaafu huwa analipwa pesa zote alizochangia yeye na Mwajiri wake (5% na 15%) halafu Mfuko unaongeza nyingine kutoka kwenye uwekezaji na kisha anaanza kulipwa pension kila mwezi. Hapo unasemaje kuna pesa imebakia PSSSF au NSSF.
Ukweli ni kwamba Mstaafu akishalipwa kiinua mgongo ambacho huwa mara nyingi ni zaidi ya hata michango yake yote anaanza kulipwa Monthly Pension ambayo mara nyingi huwa ni zaidi ya 40% hadi 50% ya mshahara wake (Net pay) aliyokuwa analipwa akiwa kazini.
Ukweli ni kwamba Pension hiyo atalipwa maisha yake yote yaliyoko mbele Hata kama akiishi miaka 50 au zaidi baada ya kustaafu.
Ndugu wafanyakazi wenzangu kama tunaomba mafao makubwa tuwe tayari kuongeza uchangiaji yaani badala ya kuchangia 5% au 10% ya mishahara yetu tukubaliane kiasi kiongezwe kiwe 10% au 15% na Mwajiri atuongezee 15% au 20%
Au pia kama tukitaka mafao makubwa tukubaliane mfumo wa pension ya kila mwezi uondolewe ili kila mtu akistaafu alipwe Kiinua mgongo kama wabunge na Madiwani halafu pension isiwepo.
Au tuchague mfumo wa pension kwa wote ambapo hakuna kuchangia chochote kila mwezi na kila mwananchi akitimiza miaka 55 au 60 anaenda HAZINA kuu ya Serikali kuchukua Kiinua mgongo chake bila kujali alikuwa mwajiriwa au Mjasiriamali.
Au tuchague kuwa na Mifuko mingi ya pension na kila mfuko ujipangie mafao utakayotoa chini ya Sheria za ushindani na serikali isiingilie lolote zaidi ya kuweka Sheria na sera za kuwalinda wateja wa Skimu hizo.
Imeandikwa na
FADEMO DIRECTOR.
Social Security Practioner with 19 years of Field Experience
Dhima ya hifadhi ya jamii ni kukupa income security pale unapo patwa na janga mfano, Uzee, kupoteza ajira, kifo etc. Kupunguza dependency ratio, ukimfata mtu aliye staafu 2005 - 2018 kilio chao kikubwa waongezewe Monthly pension wamesahau kabisa kama walilipwa kikubwa mwanzoni.. Hifadhi ya jamii haipo kukupa wewe utajiri wala pesa za kujengea nyumba ipo kwaajiri ya kukupa income security.Msilete huruma hewa. Watu wapewe fedha zao zote. Atakaechezea ataishi kama wazee wengine ambao hawakuwaikuwa kwenye mfumo wa ajira.
😀😀! Mnaweka hisia.. Kifupi kama umeshindwa kuinvest 90%+ ya mshaara unao upata, unakuja kutegemea asilimia 5% ulio changia ndio utimize ndoto zako utakuwa ni Mpumbavu tu.Kama wewe ulishindwa kuhandle pesa zako ni wewe, usigenerelize.
Nimekuja kugundua kuna umuhimu wa kuanzishwa somo la uhifadhi ya wajamii kwenye elimu yetu.Akili za hivi ndo zinaua Taifa. Laana hsitawaacha kwa uwongo wenu huo.
1. Kama waliokuwa kwenye Mashirika walipunjika,ni nini kiliwafanya msiwarekebishie wao tuu ili walingane na wengine kwenye kikokotoo cha zamani?
2. Ni kwa nini mnapochukua pesa za wanachama kuwekeza kwenye miradi hamtoi taari za faida anayotarajia kupata mwanachama? Huo siyo ufisadi na uuwaji wa mifuko?
3.
Huu ni ubinafsi Wa Hali ya juu, kwanini waajiriwa wapya ndo waumie almradi nyie mmetoka na kitita chenu kwa kikokotoo cha zamani? Kama kitu hakifai, tuseme hakifai siyo kusema kundi flani lianze na hii mpya. No.Maelezo ni mengi sana lakini huna nguvu ya ku-convince watu. Sijui kama mwanzisha thread ndiye mwandishi lakini swali langu ni hili: Kwa nini utaratibu ubadilishwe ghafla? Mtu anapo-saini mkataba wa kuanza ajira, huwa mwajiri na mwajiriwa wanakubaliana mambo mengi, moja wapo likiwa ni ukatwaji wa malipo ya pension na ulipaji wakati wa kustaafu. Kwa wafanyakazi ambao tayari wako kwenye ajira, huoni kuwa serikali ni kama imekiuka mkataba waliwekeana wakati wa kuajiriwa? Kwa nini serikali haikuendelea ku-honor mkataba waliokubalina kuhusu makato na malipo ya pension na kuanza utaratibu mpya kwa watumishi wanaoajiwa sasa hivi?
Jaribu kusoma kwa ufahamu. Kwanza mimi sihusiki kwenye kulipwa pension. Nilichosema nikuwa kama wanataka waanze mikataba mipya badala ya kubadilisha njiani. Ikianza mikataba mipya wale waajiriwa wapya watakuwa na nafasi ya kukubali mfumo wa pension ili waajiriwe au kukataa na kutoajiriwa. BTW, the way foward sidhani kama utaratibu utakuja kubadilika tena watu wawe wanalipwa fedha zote kwa mkupuo. Jaribu kufanya uchunguzi, nchi nyingi kabisa pension hulipwa kila mwezi kama mshahara. Cha kuzingatia ni kuwa malipo ya kila mwezi huwa yanakidhi mahitaji ya walipwaji kwa kiasi kikubwaHuu ni ubinafsi Wa Hali ya juu, kwanini waajiriwa wapya ndo waumie almradi nyie mmetoka na kitita chenu kwa kikokotoo cha zamani? Kama kitu hakifai, tuseme hakifai siyo kusema kundi flani lianze na hii mpya. No.
Akili za wanao Dai walipwe pesa zao kwa mkupuo tu, kusiwepo na pension ya kila mwezi hawana Tofauti na akili za MWANA MPOTEVU, kisa hiki kipo kwenye biblia kwenye kitabu cha Luka 15 11 - 24, nitanukuu hapo chini, Ndugu zangu kuna watu wanastaafu na mishaara ya 700k hawa ukisema uwape Full pension, pension yao haiwezi zidi hata Million 50. haya wapewe hizo million wakajifie mbele pesa zikiwaishia wa-anze kuwa tegemezi..!? tuongeze dependency ratioKama wewe ulishindwa kuhandle pesa zako ni wewe, usigenerelize.
kama hakuna pesa inayobaki, kuna haja gani ya kucalculate kwa hizo formula wakati inajulikana umechangia 20% kwa miaka kadhaa??? balance si inaonekana?Ukisha lipwa kiinua mgongo hakuna pesa yako inayo baki kwenye mfuko.
miezi ya uchangiaji inajibu swali lakona jingine mbona hiyo formula haizingatii umri wa mtu kwenye ajira. maana inaangalia wastani wa mishahara ya miaka 10 tu ambayo maana yake mtu aliyefanya kazi kwa miaka 30 atakuwa hana tofauti ya maslahi yake ya mwisho na yule alifanya kazi kwa miaka 15 na pengine kama huyu wa miaka 15 alikuwa na mshahara mkubwa basi atamwacha mbali sana huyo wa miaka 30 au hilo likoje? nini kitakachowatofautisha hao watu wawili kwenye maslahi watakayopata?
ambacho hufafanui ni kuwa hicho kiinua mgongo unalipwa ASILIMIA 33 unapostaafu na ASILIMIA 67 inalipwa ndani ya miaka 12.5 baada ya hapo.. Ikipita miaka 12.5 unakuwa ushamaliza kiinua mgongo chako. baada ya hapo kama utakuwa bado hujafa, mfuko wa jamii itaendelea kukulipa ingawa pesa yako inakuwa imekwisha- Kiinua Mgongo ni zaidi ya kile ulicho changia kwenye mfuko, simply mtu akisha lipwa kiinua mgongo inakuwa hakuna pesa ambayo umebakiza kwenye mfuko.
- Ni ngumu kuielewa zana ya Hifadhi ya jamii, kama unalengo la kupinga na kukosao sio kujifunza mfumo wa hifadhi ya jamii unafanya kazi vipi.
maelezo, uchambuzi, ufafanuzi na elimu mujarabu sana hii, dhidi ya upotoshaji wa makusudi wa watu wachache wasioelewa vema dhima na lengo la kikokotoo hiki.....Watumishi wa umma wengi sasa hivi wanafuatilia issue ya kikokotoo cha mafao yao ya baadaye.