Mzee kama huna Uwezo wa kujibu Hoja usicopy na kupaste ulichokijibu nyuma na nikakupa jibh hilo
Tafuta waliolipwa 50 kwa 50.
Then waulize wangerudi kwenye utumishi wangetamani kulipwa vipi?
Mimi nadhani changamoto tumeshindwa kubalance story,kati ya Watumishi na wastaafu waliokwishalipwa.
Wapo wastaafu wanatamani hata wasingelipwa mkupuo, pesa yote iende kwenye montly pensheni na iwe kubwa.
Sisi tumeamua kuwa kwenye kelele za Watumishi na wanasiasa.
Tumeamua kuweka taaluma pembeni, sijui na sitaki kuamini wakati tunasoma principles za Hifadhi ya jamii kuna mtu aliwahi kupingana na kile tulichokuwa tunafundishwa.
Leo hii tumeanza kupingana nacho either kwa sababu njia zetu hazijafunguka kuiona na fani yetu kuwa na msaada kwetu direct.
Kuna nchi hata mkupuo hazina kabisa,mtu akistaafu anaunganisha na pensheni ya kila mwezi.
Kuna nchi ukistaafu wanakupa pesa yako yote lakini wao kiuchumi wako vizuri walishakufanyia kila kitu.
Wazee wakishapewa wananunua Annuity ili kila Mwaka walipwe pesa nzuri.
Mnaosema wastaafu wapewe pesa zao zote naombeni leteni mifano ya waliolipwa na wakawekeza na kuwa vizuri kifedha hadi sasa.
Hata watatu tu!