Ufafanuzi kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu

Huu ndio ukweli ambao srikalu haijakiri. Inabaki tuu kutumia maneno kama sustainability ya mfuko na mengine ja kufichaficha lakini hawasemi chochote juu ya ubadhirifu, mikopo ya hovyo na uwekezaji usioleta tija kwa mifuko
 
Mzee kama huna Uwezo wa kujibu Hoja usicopy na kupaste ulichokijibu nyuma na nikakupa jibh hilo
 
Safi🤝🏿
 
Mzee kama huna Uwezo wa kujibu Hoja usicopy na kupaste ulichokijibu nyuma na nikakupa jibh hilo
Tafuta waliolipwa 50 kwa 50.


Then waulize wangerudi kwenye utumishi wangetamani kulipwa vipi?

Mimi nadhani changamoto tumeshindwa kubalance story,kati ya Watumishi na wastaafu waliokwishalipwa.


Wapo wastaafu wanatamani hata wasingelipwa mkupuo, pesa yote iende kwenye montly pensheni na iwe kubwa.

Sisi tumeamua kuwa kwenye kelele za Watumishi na wanasiasa.

Tumeamua kuweka taaluma pembeni, sijui na sitaki kuamini wakati tunasoma principles za Hifadhi ya jamii kuna mtu aliwahi kupingana na kile tulichokuwa tunafundishwa.

Leo hii tumeanza kupingana nacho either kwa sababu njia zetu hazijafunguka kuiona na fani yetu kuwa na msaada kwetu direct.


Kuna nchi hata mkupuo hazina kabisa,mtu akistaafu anaunganisha na pensheni ya kila mwezi.


Kuna nchi ukistaafu wanakupa pesa yako yote lakini wao kiuchumi wako vizuri walishakufanyia kila kitu.

Wazee wakishapewa wananunua Annuity ili kila Mwaka walipwe pesa nzuri.


Mnaosema wastaafu wapewe pesa zao zote naombeni leteni mifano ya waliolipwa na wakawekeza na kuwa vizuri kifedha hadi sasa.

Hata watatu tu!
 
Monthly pension ndio maisha.. Wengi wanao waza wapewe pesa zao zote, akili zao ni kuwa wakistaafu tu watakufa.. Wanaona walipwe 100% ili wafe nazo.
 
sio nitafute Nimekuambia ninao wengi sana na wanafurahi kulipwa hivyo..

By the way kuna rafiki zangu mwaka 2020 mpaka 2022 kabla kikokotoo hakijaanza kufanya kazi waliomba kustaafu haraka kabla hakjjaanza..

Kiukweli hakuna Mtumishi narudia Tena hakuna Mtumishi anayefurahia Hiki kikokotooo..

SIo polisi sio Afya,Sio elimu wala sio Kada yoyote..
Nilikuwa miongoni mwa waliokusanya maoni na tuliyapeleka TuCTA ili yawasilishwe Bungeni na Pia Kwa Rais na mengine mtayasikia SIKU YA Mei mosi..

Nimezunguka Mikoa 20 nikiwa mwenyekiti wa Chama fulani cha wafanyakazi kwa Mkoa Fulani na yote hiyo asilimia 99 hawataki Kikokotoo..
Nyie hao mliowauliza mliwauliza wapi..

Report Ya kuzunguka huko Ipo kwa Rais wa TUCTA
 
kwani kiongozi iyo ela ni ya kwenu au wan

Ni asilimia 19% ya watumishi ndio walikuwa wanalipwa hicho kikokotoo unacho semea niwa PSPF na LAPF.. unawajua walio kuwepo PPF, NSSF na GEPF walitumia kikokotoo kipi...!?
 
kwani kiongozi iyo ela ni ya kwenu au wan

Ni asilimia 19% ya watumishi ndio walikuwa wanalipwa hicho kikokotoo unacho semea niwa PSPF na LAPF.. unawajua walio kuwepo PPF, NSSF na GEPF walitumia kikokotoo kipi...
Vipi kuhusu Wabunge wao hawakupenda Kupewa Hio ya kila mwezi??
Kwanza utambue wabunge, RAS, DAS hawalipwi na PSSSF wala NSSF wana mfumo wao wa ulipaji na sio wanachama wa NSSF wala PSSSF.
 
Vipi kuhusu Wabunge wao hawakupenda Kupewa Hio ya kila mwezi??
Ubunge ni kazi ya mkataba wa miaka 5. Hawakatwi fedha za mifuko ya pensheni. Kwa hiyo kisheria hahusiki na mifuko hiyo. Hata hiyo kupata pensheni mpaka uwe umechangia miaka 15.
 
umeeleza mno kwa kujaribu kutetea!!
ila huwa najiuliza Wabunge wetu ni wapuuzi kiasi gani
wanatengeneza tatizo wenyewe halafu baadae wanapigia kelele kitu fulani si sawa wakati wao wenyewe walipitisha kwa sauti kubwa NDIOOOOOO
kitu nnachotamani nchi hii ya watanganyika tungalikuwa na uwezo wa kupiga kura kuwatoa (wabunge,wakurugenzi,DAS) pale ambapo hawaendi kama tunavyohitaji
nadhani utendaji unetukuka kidogo kwenye hizi nafasi za kisiasa
 
Ubunge ni kazi ya mkataba wa miaka 5. Hawakatwi fedha za mifuko ya pensheni. Kwa hiyo kisheria hahusiki na mifuko hiyo. Hata hiyo kupata pensheni mpaka uwe umechangia miaka 15.
lakini mbona mimi nafanya kazi kwa mkataba 5 years kampuni X na nakatwa NSSF na Paye
wao wana exclussion gani ya kutokukatwa hivyo!
 
Kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, kinacho fuatwa ni sheria na misingi ya hifafhi ya jamii.. Sio kauli za Mbunge au DAS.
 
Kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, kinacho fuatwa ni sheria na misingi ya hifafhi ya jamii.. Sio kauli za Mbunge au DAS.
hii ndo kauli ambayo huwa inanifikirisha sana
ukweli ni kwamba siasa inaendesha maisha yetu ya kila siku
leo unaambiwa unchukua hela zako
kesho unaambiwa mara unalipwa asilimia ya mshahara wako kwa miezi sita
ukisema tunaendeshwa na sheria za hifadhi ya jamii pekee bila siasa si kweli
 
Ni asilimia 19% ya watumishi ndio walikuwa wanalipwa hicho kikokotoo unacho semea niwa PSPF na LAPF.. unawajua walio kuwepo PPF, NSSF na GEPF walitumia kikokotoo kipi...!?
PPF na GEPF zilikuwa na wanachama Wachache sana Kulinganisha na PSPF na LAPF japp LAPF ilikuwa na wanachama wengi kuliko Hivyo vyote..

Na ndo maana LAPF na PSPF ndo zilikuwa zinafuatwa na watumishi wengi..

Kuhusu NSSF sio mfuko wa watumishi wa serkali So haituhusu
 
Siasa ipo kila kona, hili sijapinga.
Na point yangu ipo palepale, tusibadilishe maada kwenda kwenye siasa tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…