Ufafanuzi kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu


Kama huyo ni Director afukuzwe kazi haraka sana..!!

1: Nothing kaelezea zaidi ya formula tu

2: Hiyo formula ya PSPF na LAPF ilikuwa kwa watumishi wa Serikali kuu, ilikuwa kizuri sana kwani kina 50% sio 33% kwa mkupuo, na kina 15.5 yrs na sio 12.5 yrs, na kina 1/540 sio 1/580 na kina LAS sio APE, so ukiangalia formula mpya imepunguza kila sehemu katika formula, yaani wamekata, maana yake ukichukua formula mpya na ya zamani mafao ya mstaafu unapata nusu kwa formula mpya ukilinganisha na formula ya zamani, yaani mstaafu atapata nusu tu ya mafao yake kwa mkupuo, hii mbaya sana

3: Huyo Director kazi yake anatetea tumbo na kazi yake tu, hana lolote na hawezi saidia chochote kwa watumishi wa Umma.

Mh. Rais wetu Mama Samia ndio mkombozi pekee aliyebakia kuwafuta machozi watumishi wa Umma.
 
kwani ukiteseka ni wewe au wao. walipe pesa watu pesa zao zote wakapambane mbele huko. kwan unazani wabunge pension zao wanachukua kidogo kidogo
 
kwani ukiteseka ni wewe au wao. walipe pesa watu pesa zao zote wakapambane mbele huko. kwan unazani wabunge pension zao wanachukua kidogo kidogo
Kama ni kulipwa pesa zao zote walizo changia, Pesa zao zote wamesha lipwa kwenye kiinua mgongo.
 
Mapungufu ya hiyo formula ndio imefanywa ifutwe ( Iondolewe ). Ilikuwa inaua mifuko.

2014 - 2018 wastaafu walio kuwa wakistaafu PSPF na LAPF walikuwa wakisubiri zaidi ya mwaka kulipwa CP kwasababu mifuko ilikuwa haina pesa na kilicho sababisha mifuko hiyo kushindwa kujiendesha 70% ilikuwa ni formula ya kikokotoo wanacho tumia.
 
Acha porojo nyingi,
Wewe ungekuwa mtumishi ungependa ulipwe pensheni yako kwa kikokotoo kipi?
 
Nilimpigia hesabu mstaafu mmoja mtarajiwa, najuta kufanya hivyo toka leo pressure na sukari haijawahi kushuka nalaumika na familia nzima, naumia leo nimetoka Muhimbili kumuona.
Daaah pole yake kiongozi. Na huu ndio ukweli wenyewe kabisaa.wengi kwa sasa hali zao na kiafya sio nzuri wastafu watarajiwa. Alafu anatokea chawa mmoja uko kuleta ngenye zake hapa.
 
Sijaona utafanuzi zaidi ya matusi.
Mwandishi atakua ni kada wa chama chakavu. Ametumwa.
 
Mimi NATAKA UJIBU HILI SWALI RAHISI ILI TWENDE SAWA Ingawa huko mwanzo umelikimbia ila nitaomba mods wakulazimishe kujibu,

Mfanyakazi aliyestaafu na mshahara wa basic 1,500,000 alipata kiinua mgongo kiasi gani na pensheni ya mwezi kiasi gani kwenye kikokotoo Cha zamani,

Na mfanyakazi huyu huyu atapata kiasi gani na kwa mwezi kiasi gani kwenye kikokotoo kipya,

Endapo kama amefanya kazi miaka 25


Naomba ujibu
 
Na hoja ya muhimu zaidi ni tunafanye kuhusu kesho ya hawa wengi ambao sio pensionable ?
 
Ok..so hapo kastaafu july 2018, na kwa document hiyo nitajuaje kama ni kipya au cha zamani
 
Ass hole, kuna ubaya kulipwa pesa yako yote?wewe utakuwa umerogwa! Yaani kulipwa mkwanja wako wote ni jambo baya!
 
Bora wewe unaeleweka siyo huyu mleta uzi, hamna anachoelezea akaeleweka. Anapayuka tu.
 
Sasa unataka kiinua mgongo ndio kikujengee nyumba, ununue gari, uongeze mke kwanini ulishindwa kufanya ukiwa na asilimia 95% ya mshaara wako wote, unataka hii uliyo kuwa unachangia 5% ndio ifanye hayo yote...!?
hela yoyote unaweza kufanya jambo lolote,kama mshahara ambao haujaandikwa popote mtumishi ajengee kibanda cha vyumba viwili umeona ni sawa mtu kujengea hata pension inawezatumika tu.
 
Hiyo APE inakokotolewa vipi?
 
Ukisikia mtumishi wa umma anadai hataki pensheni ya kila mwezi anaomba alipwe pesa zake zote aendelee na maisha yake ujue kuwa huyo siyo mtumishi wa umma. Ni Mjasiriamali
Kwani ujasiliamali ni kosa kisheria?
Kuna ubaya gani kuwa mjasiliamali?
Maisha hayafanani, wengine walishawekeza kidogokidogo, serikali haipaswi kuwapangia namna ya kuishi au kutumia haki zao, mbona wabunge hawapangiwi maisha? Kwanini kuwe na double standards?
 
Hii habari ya mfuko uweze kujiendesha ndiyo inawaumiza watu, fedha zinawekezwa kwenye madude yasiyo na maslahi kwa wanachama mwisho wa siku wanaishia kuumia na kufa kwakuwa kuna genge la wahuni wanacheza kamari na hayo mafao ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…