DeepPond
JF-Expert Member
- Nov 18, 2017
- 41,728
- 103,997
Mtoa mada kaandika pumba, na nadhan kaileta kusudi kuelekea Mei mosi.Kulichoandikwa Mpaka Mwisho ni Upuuzi tu na wala sijasoma mpaka mwisho nimeishia katikati tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtoa mada kaandika pumba, na nadhan kaileta kusudi kuelekea Mei mosi.Kulichoandikwa Mpaka Mwisho ni Upuuzi tu na wala sijasoma mpaka mwisho nimeishia katikati tu
Sustainable kivipi wakati mifuko inakopwa na kujenga miradi hewa isiyorudisha pesa? Wee jamaa mzima kweli?Hio sio Pensheni waweke pesa Benki na hapo kutakuwa wala hakuna ulazima kwenye Sheria mwajiri wako kukuongezea hizo asilimia za ziada...
Narudia tena pensheni zilianzishwa kama Social Security na Sio Mtaji kwahio hawa unaosema wapo kwenye ajira na wanafanya biashara kuna mifuko tofauti ambayo wanaweza kuweka ambao wakitaka pesa zao wanaweza kupewa zote bila mfuko kuharibika / kufa...
Cha maana na kigezo ambacho kina-make sense ni watu kulalamika kwamba mtu anachopata kila mwezi hakikidhi mahitaji na wengine watakaokuja kesho watakuwa sio pensionable...; lakini issue ya kila mtu apewe chake chote sio sustainable
Mstaafu mwenzio mwenye Cheo sawa na weww alikula milion 80 wew leo unaenda kuambulia mil 20 alafua anatokea mbwa mmoja anakwambia usenge wa calculator.... kunaa mtu atakulaa chumaa wazi waziii watu wa machungu sanaa na huu upuuzi unaoendeleaa.
Serikali imewageuza wastaaf mbuzi wa kafalaHuu ndio ukweli ambao srikalu haijakiri. Inabaki tuu kutumia maneno kama sustainability ya mfuko na mengine ja kufichaficha lakini hawasemi chochote juu ya ubadhirifu, mikopo ya hovyo na uwekezaji usioleta tija kwa mifuko
Nimesema mifuko ni sustainable ? Moja nimeongelea Dhima ya Pension ni Insurance / Security, na kwa muktadha huo pensheni funds hazitakiwi kujiingiza kwenye volatile investments.....Sustainable kivipi wakati mifuko inakopwa na kujenga miradi hewa isiyorudisha pesa? Wee jamaa mzima kweli?
Nimesha kujibu, kuwa ukilipwa kiinua mgongo hakuna pesa unayo acha kwenye mfuko, kwaio kama wewe unataka pesa zako zote, baada ya kulipwa kiinua mgongo unakuwa umelipwa pesa yako yote, ile ya kila mwezi achana nayo, maana inatoka kwenye mfuko sio ambayo umechangia.
Wabunge sio wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii, PSSSF/NSSF na hawalipwi na NSSF/PSSSF..
Wabunge sio wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii, PSSSF/NSSF na hawalipwi na NSSF/PSSSF..
Hizi ndio naita Vioja na kwa bahati mbaya sana ndio kifo cha mijadala hapa JF..., does it matter hata kama mimi nigekuwa ni Robot au AI ? Cha muhimu au cha kuangalia ni kama nachoongea kina mashiko au ni Pumba na kiwe weighed kwa uzito huo....Jambo liko wazi, Logikos na DOMINGO THOMAS Ni I'd za mtu mmoja.
Acha janja janja,Hizi ndio naita Vioja na kwa bahati mbaya sana ndio kifo cha mijadala hapa JF..., does it matter hata kama mimi nigekuwa ni Robot au AI ? Cha muhimu au cha kuangalia ni kama nachoongea kina mashiko au ni Pumba na kiwe weighed kwa uzito huo....
Pili sidhani kama mimi na mleta uzi tuna perceptive moja per se...., mimi perception yangu ni umuhimu wa pension na ukweli kwamba mtu kupewa pesa zake (so called zake) zote pindi anapotaka sio dhima ya pension wala sio sustainable... Point yangu kubwa ni kwamba monthly pension iboreshwe na ihakikishwe kila mtu anakuwa na monthly pension kwa kuhakikisha ustawi wa jamii...., Sababu duniani kote mtaji mkubwa wa pension ni wachangiaji (wanaofanya kazi) kuwachangia waliostaafu... Kama ukitaka returns kubwa au kuchukua pindi unapotaka kuna investments funds nyingi tu.., ila usijeshangaa hizo investment funds zinakenda belly-up na usipate kitu (sababu hazina guarantee)....
Tena hapa kuna opportunity ya wapigaji leo hii mtu anaweza ku-lobby watunga sera na kuanzisha pension funds zao zenye returns kubwa balaa na kuhakikisha mtu akiacha kazi tu anapewa chake maradufu (ila usishangae yakatokea ya kina Bernie Madoff)
In conclusion kama taifa we need Security ya kuwa-protect wazee wetu..., kustaafu means kustaafu na sio kubadilisha kazi au kuanza biashara...
Aisee sasa nitumie huo muda ili niku-convince wewe ili iweje ? Ndipo bapo sasa ume-confirm nilichosema hapo mwanzo badala ya kuzungumzia mapungufu au lack of Pension Funds tunaongelea identity yangu (which is immaterial as long as mjadala unavyohusika) mjadala umetoka kwenye issues mpaka individual... which I have to say ni matumizi mabovu ya rasilimali muda as far as am concerned....Acha janja janja,
Uandishi, Maelezo,comand na upangiliaji Hadi uwekaji wa nukta mnafanana. We are not that fool
Jaribu kusoma kwa ufahamu. Kwanza mimi sihusiki kwenye kulipwa pension. Nilichosema nikuwa kama wanataka waanze mikataba mipya badala ya kubadilisha njiani. Ikianza mikataba mipya wale waajiriwa wapya watakuwa na nafasi ya kukubali mfumo wa pension ili waajiriwe au kukataa na kutoajiriwa. BTW, the way foward sidhani kama utaratibu utakuja kubadilika tena watu wawe wanalipwa fedha zote kwa mkupuo. Jaribu kufanya uchunguzi, nchi nyingi kabisa pension hulipwa kila mwezi kama mshahara. Cha kuzingatia ni kuwa malipo ya kila mwezi huwa yanakidhi mahitaji ya walipwaji kwa kiasi kikubwa
Unachangia asilimia 5%, 15% ni kutoka kwa mwajirikama hakuna pesa inayobaki, kuna haja gani ya kucalculate kwa hizo formula wakati inajulikana umechangia 20% kwa miaka kadhaa??? balance si inaonekana?
Malipo ya kila mwezi yanalipwa mpaka pale unapo fariki, na ukifariki tegemezi watachukua ×36 ya kile unacho lipwa kwamwezi.ambacho hufafanui ni kuwa hicho kiinua mgongo unalipwa ASILIMIA 33 unapostaafu na ASILIMIA 67 inalipwa ndani ya miaka 12.5 baada ya hapo.. Ikipita miaka 12.5 unakuwa ushamaliza kiinua mgongo chako. baada ya hapo kama utakuwa bado hujafa, mfuko wa jamii itaendelea kukulipa ingawa pesa yako inakuwa imekwisha
Asante.🤝🏿maelezo, uchambuzi, ufafanuzi na elimu mujarabu sana hii, dhidi ya upotoshaji wa makusudi wa watu wachache wasioelewa vema dhima na lengo la kikokotoo hiki.....
thank you very much gentleman DOMINGO THOMAS