Mnafiki Wa Kujitegemea
JF-Expert Member
- Dec 30, 2022
- 3,751
- 6,337
TatiZo wewe sio rais sasa na huwezi kuwa hasa hasa utaishia kuwa mke wa boda bodaKisheria wapo wenye mamlaka ya kukamata lakini kwa kitendo cha watu kujichukulia sheria na kuharibu mali ya umma Ningekua Rais kitu ningefanya kwanza polisi wangepiga msako wa maana hicho kijiji kilicho changamka cha dasilam wote mngekaa mahabusu
Wanabeba na silaha??Hii ni ngeni kwako? Fatilia vizuri hao jamaa wana operations zao, wapelelezi, intelejensia yao na wanakamata vilevile, haijalishi siku wala masaa.
Wasiojulikana baada ya mission kufeli mnajifanya watumushi wa TRA na ngojeni wananchi waendelee kuamkia watakula nyie sahani mmoja hamtoamini macho yenu.View attachment 3170012
UFAFANUZI KUHUSU SHAMBULIO LA GARI NA WATUMISHI WA TRA KATIKA ENEO LA TEGETA (Kwa Ndevu)
Dar es Salaam, 06 Desemba, 2024:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inasikitika kuutarifu Umma kwamba gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za Forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, tarehe 05 Disemba, 2024, usiku.
Kadhia hii imetokea baada ya watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ilioingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.
Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa.
Mamlaka ya Mapato Tanzania, inawapa pole watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone kwa haraka.
Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.
"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"
Imetolewa na;
IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO
Pia Soma: Tegeta, Dar: ‘Wasiojulikana’ washambuliwa na wananchi kwa mawe
Huwa kiutaratibu wanapaswa kuongozana na polisi lakini deals zao za 'kipigaji' huwa wanaenda peke yao ili wanachovuna kusiwepo watu wengi wa kugawana.Nilikua sifahamu kama officer wa TRA ana mamalaka ya kukamata mtu? Sio kazi ya polisi hiyo wajameni!
Kwanini msingeongozana na polisi?
Wewe mjinga hujui tra inavyofanya kazi kaa kimya funga domo lakoKama gari mnaijua na ina usajili kwanini msimuite mwenye nayo atoe nyaraka za gari yake? Inakuwaje mnaanza kufuatilia mtu tena usiku?
Nyie ni polisi?
Je mna mamlaka ya kumfuatilia mtu na kumkamata au kukamata mali yake bila kushirikisha vyombo vya ulinzi na usalama?
Hayo yote mmeyataka kwakuwa hali ya usalama wa raia nchini imedhoofu kiasi kwamba sasa raia ni lazima kuwa vigilant la sivyo ni kutekwa na kuuwawa tu.
Wafanyakazi wenu mnatakiwa muwape barua ya onyo kwa kuwa negligent. Wameshindwa kusoma alama za nyakati.
Sasa hivi hatuaminiani mkuu. Polisi imeshindwa kuwalinda raia sasa raia wanaanza kulindana na hapo effects ndipo zinaanza kuchomoza. Now ukija kamatwa unakuwa huna uhakika kama unakamatwa unapelekwa polisi au mabwepande maana wanakuja wakidai ni polisi na wakati mwingine na gari la polisi au tra ila baadaye polisi wanakana kuwa hawajakukamata.mpaka wanaplate namba ni kinyemela kweli? au kuna jambo lililojificha
Sasa hiyo ni red alert, wakiendelea hivyo watakufa sana.Hii ni ngeni kwako? Fatilia vizuri hao jamaa wana operations zao, wapelelezi, intelejensia yao na wanakamata vilevile, haijalishi siku wala masaa.
Kwa mujibu wa sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki,Customs Officer amepewa nguvu ya polisi awapo katika majukumu yake.Hii ni ngeni kwako? Fatilia vizuri hao jamaa wana operations zao, wapelelezi, intelejensia yao na wanakamata vilevile, haijalishi siku wala masaa.
Na kaxi yao itqzifi kuwa ngumu, hakuna raia atakubali kukamatwaTRA poleni sana kwa yaliyowakuta kupigwa mawe kama vibaka.Hii nchi ni yetu sote nawalaum sana polisi wetu kwa kupuuzia vitendo vya utekaji,raia wameanza kuamka.Bila kuwekana Sawa wengi wataumizwa sana kwa kigezo cha Utekaji.Taratibu zifuatwe.
Hapo hapo wahalifu ndo watatumia upenyo wa kufanya tukio na kutoroka.Hata kama watakuwa wanakamatwa kihalali.Na kaxi yao itqzifi kuwa ngumu, hakuna raia atakubali kukamatwa