Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Hapana, Dar es Salaam kumbuka ni mkoa. Kwa maana ya Mkoa, ina idadi ile ile ya watu, kwa maana ya Jiji la Dar es Salaam ( Urban Proper eneo la Ilala) kweli itakua na watu wachache. Kwa sasa kama watu wanaoboresha taarifa za Google inatakiwa ukiingia uone hivi:
Dar es Salaam City
Capital- Ilala
Population- Itapaswa iwekwe watu wote wakaazi wa iliyokua Manispaa ya Ilala. Metro- Inatakiwa idadi ya watu wote wa Manispaa zilizobaki zinazounda mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa ziko kwenye mji mmoja(tofauti na kama Mbeya, Dodoma, Arusha na Tanga)

Hapo nyuma kimuundo, google iliweka watu wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni wakazi wa jiji bila Metropolitan Areas.
Ukiingia google miji mingi duniani hata kama ulipaswa uwe na Manispaa zaidi ya 2, 3 na kuendelea, wanatenganisha eneo moja kuwa jiji na mengine kufanya Metro Area(kwa pamoja).

Angalia Kinshasa City na Kinshansa Province, Paris na Andorissment(Municipalities) London na Gretar London, Lagos na Metro kuifanya Corbunation, Los Angeles na Greater Los Angeles kutaja mifano michache. Ingia google utajifunza miji wenzetu walivyoitofautisha ingawa ni eneo moja ila lililo kubwa.
 
Kuhusu faida na hasara. Kimsingi mimi sioni faida, ila naona hasara, kwa sababu
1. Lazimakutakuwa na wafanyakazi pale jiji la dsm (ilala) ambao watanya shughuli za uratibu zilizo kuwa zinafanywa na jiji lililovunjwa. Kama kuratibu miradi. Gharama za uratibu lazima zitakuwepo.

2. Kwa kuwa meya wa ilala ndo anakuwa meya wa jiji ikiwa ni pamoja na mkurugenzi, kuna uwezekano mkubwa wakapendelea ilala kuliko manispaa zingine kwa miradi ambayo ni ya "jiji".

3. Vikao vya madiwani wote wa halmashauri zote au wawakirishi wao kukaa na kujadili na kukubaliana mambo ya jiji bado vitakuwepo. Maana huwezi kuratibu bila vikao. Posho na matumizi mengine ya uratibu itakuwa pale pale.
4. Ilala itaanza kuelemewa na majukumu ya uratibu ambayo nayo yanahitaji fedha. Je watapata wapi fedha za uratibu?

Kimsingi tumetengeneza tatizo lingine badala ya kusolve tatizo.
 
Kweli wajiandae kisaikologia...maana Hadi ..askari wa jiji wataishia magomeni tuu maana huku kwetu ni manispaa
.
 
Ndio kusema matukio yatakayotokea kinondoni, mwenge, magomeni, waandishi watasema "nje kidogo mwa jiji la daressalaam"
 
Kuhusu faida na hasara. Kimsingi mimi sioni faida, ila naona hasara, kwa sababu
1. Lazimakutakuwa na wafanyakazi pale jiji la dsm (ilala) ambao watanya shughuli za uratibu zilizo kuwa zinafanywa na jiji lililovunjwa...
#2 ulivoiandika Inaonyesha wazi huu muundo hujauelewa.

Hakuna Halmashauri itakayosimamia eneo jingine. Ilala ni kwa ajili ya Ilala tu.
 
Nashukuru kama umeona naropoka. Lakini kama ungekuwa unajua jinsi mifumo inavyofanya kazi usingeona naropoka. Kwa mfano huu mradi Mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Metropolitan Development Project- DMDP) ulikuwa chini ya jiji, kwa sasa utachini ya ilala (jiji jipya). Una cover halmashauri zote.
 
Sahihi kabisa
 
Kuna watu mazoba sana
Ni vyema ukachukua muda kusoma, kufanya utafiti kidogo na kutafakari. Jiji kama jiji la dar es salaamu kama jiji halijavunjwa. Ila majukumu yake yanahamishwa kwenda iliyokuwa manispaa ya ilala.
 
Dar es salaam ingebaki kuwa jiji lenye manispaa zake tano tu na mameya kwenye hizo manispaa bila kuwa na meya wa jiji au kinachoitwa halmashauri ya jiji.Over.
 
KAMA UKO NJE YA KATA HIZI BASI KUNZIA 24.02.2021 JIHESABU UPO NJE YA JIJI LA DAR

1 Kisukuru
2. Jangwani...
Ilala imekuwa Dar city, kinondoni ikifikia viwango vya jiji itaitwaje? Inamaana ndani ya mkoa wa Dar kutakuwa Dar city, kino city, Tmk City etc itapofikia maeneo yote hayo yana viwango vya kuwa Jiji.
 
Hizo ofisi za jiji zilizoenda ilala zitasimamia eneo gani la kiutawala?
Dar es Salaam in its whole is still a city.
Ilala zimeenda ofisi za jiji tuu. Acheni Ujinga.
 
Ilala inakuwa makao makuu ya nini?
Na kwakuongezea Dar inabaki kuwa mkoa wenye halamshauri ulizotaja hapo lakini ilala ikiwandio makao makuu yake. Watu wengi imewachanganya .
 
Tangu Rais Dr. John Pombe Magufuli kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji la Dar es Salaam, kumekuwa na mijadala kemkem kuhusu jambo hilo runingani, redioni na hata mitandaoni....
Wape watu tofauti ya mkoa na jiji.

Kimkoa maeneo yote yapo mkoa wa Dar es salaam ila halmashauri moja ya kati ya tano za mkoa wa Dar es salaam imepewa hadhi ya jiji.

Hivyo Ilala kuwa Jiji haimaanishi kino na ubungo na halmashauri zingine sio sehemu ya Dar es salaam.
 
Hili si hata Jafo alisema palepale baada ya kupewa nafasi ya kuongea kuwa ubungo itabaki kuwa ubungo, kinondoni itabaki kuwa kinondoni jiji Sasa ni Ilala. Kwakukazia akasema jiji ni kuanzia international airport, bandari na Ikulu hiyo ndio mipaka ya jiji la Dar.
 
Huu uzi ndiyo njia pekee ya kutambua watanzania ni wazito sana kuelewa.
 
Moja ya manufaa yake ni kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa na sehemu yake mahsusi ya kiutawala tofauti na ilivyokuwa awali. Awali, jiji la Dar es Salaam ni kama lilikuwa likielea kuhusu eneo hasa la kiutawala.

Je matatizo vya Daresalaam ni kwasababu ya jiji kukosa sehemu mahususi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…