Ufafanuzi kwanini Yanga akimfunga Mc Alger anaweza kuingia top 5 kwenye CAF 5 years ranking

Makolo wanakuja kwa hasira sana japo umejitahidi vizuri sana kuelezea. Nadhani ni ile hasira kwamba vichaka vinafyekwa
 
Zinashuka kwasababu kuna msimu mmoja nyuma umefutwa na msimu mmoja mbele umeongezeka na huo msimu uliongezeka Simba imejikuta wapo kwenye mashindano ya akina mama
Umeteleza hapo,,, mwaka 2019/2020 SIMBA alikuwa na POINT O kwahiyo hakuna point atakayokatwa ila zile COEFFICIENT ndo zitabadilika kwa POINT husika...


 
Wazee wa calculator hadi kwenye rankings
 
Zinashuka kwasababu kuna msimu mmoja nyuma umefutwa na msimu mmoja mbele umeongezeka na huo msimu uliongezeka Simba imejikuta wapo kwenye mashindano ya akina mama
ivi akina mama mnatuchukuliaje lakini kwenye hilo swala🤣
 
Kwahiyo Simba akishinda point zake haziongezeki?
Akishinda nini labda? Point zake zishajumlishwa baada ya kufuzu robo sasa unataka ashinde point Gani Tena,,labda akifika nusu ndio litaongezeka Tena na yanga point zake bado azijajumlishwa ni mpaka aingie robo kwasasa anazo 34 akiingia robo atafikisha 39, na kitu ambacho amkielewi walio wengi ni kwamba point za klabu bingwa ni tofauti na za kombe la ushirikishwaji mlijue hilo!
 
Kwahiyo Simba akishinda point zake haziongezeki?
Waliofuzu robo fainali tayari point zao zimeshaongezewa na Yanga kawekea point zake kwa jinsi msimamo wa kundi lake lilivyo, hivyo ana nafasi ya kuongeza point kama itafuzu robo fainali
 
Yaani wewe hesabu zako zinawezekana tu kama points za Simba zitakua haziongezeki, kitu ambacho si kweli kwan Simba nayo imeshavuzu kuingia robo
 
Yaani wewe hesabu zako zinawezekana tu kama points za Simba zitakua haziongezeki, kitu ambacho si kweli kwan Simba nayo imeshavuzu kuingia robo
Tatizo umesoma bila kuelewa, Simba na timu zingine zote zilizo juu ya Yanga zimeshajumlishiwa point zao za kufuzu robo fainali hivyo hakutakuwa na mabadiliko mpaka pale watakapofuzu kucheza nusu fainali, ila Yanga hajafuzu ndio maana point zake ni 34 ila akifuzu tarehe 18 inamaana ataongeza point 5 na kuwa na point 39 na kupanda hadi nafasi ya 5 kwenye rank
 
Hizi point za yanga bado sielewi zinapanda vipi hizi rank mnatumia ni za wapi?
Duh kuna watu mna vichwa vigumu balaa! Hapo usichokielewa ni kipi? Au haupp tayari kuelewa? Yanga kabla ya msimu alikuwa na 24, mpaka sasa hata akitolewa robo fainali ataishia nafasi ya tatu ambayo ni alama 2 ukizidisha kwa 5 ni 10, ukijumlisha na ile 24 ni 34. Endapo atafuzu robo ni alama 3 ukizidisha kwa 5 ni 15, ukijumlisha na 24 alizonazo inakuwa 39
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…