Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu ukinisaidia namba zako itakua poa me nipo mjini mbeya nahitaji mzigoKaribu Tunduma utapata bidhaa nyingi za vupodozi kwa beii nafuu upande was Zambia eneo maarufu kama bkack
Kwa kusema kweli biashara ya vipodozi inalipa vizuri tu ukiielewa vizuri na kucheza vizuri na soko lako na biashara yenyewe kwa ujumla.
1. Nikiasi gani cha mtaji kinahitajika(minimum amount of capital) = Inategemea na msuli wako. Ila minimum uwe na kama Tsh Millioni Saba Hivi (7,000,000/=) Hivi kwa maeneo ya mjini; i.e.
- Kukodi fremu = Tsh 100,000/= kwa mwezi, miezi 6 >> 600,000/=; dalali utajuana naye mwenyewe
- Kusajili TFDA = 150,000/=
- Leseni halmashauri = 80,000/=
- Kodi TRA kama Tsh 150,000/= hivi kwa mwaka, quarter 1 utalipia Tsh 37,500/=
- Kuweka mashelfu ya aluminium na vioo = 1,000,000/=
- Kabati la chini la aluminium na vioo = 400,000/=
- Vipodozi angalau vya kuanzia = 4,000,000/=
- Pesa ya kukaa standby kwa ajili ya kuongezea vipodozi watakavyokosa wateja = 1,000,000/=
- Pia uwe na akiba ya kuendelea kuishi na kuhudumia familia yako bila kudokoa pesa kutoka kwenye duka lako kwa angalau miezi 3 hivi
View attachment 1078393
2.Ni vipodozi vya aina gani vyenye uhitaji mkubwa sana sokoni(consumer needs) = Soko la vipodozi mara zote ni dynamic; leo wateja wako wanatumia Rinju, baada ya miezi 6 watakuwa wanatumia kitu kingine. Pia inategemea sana na eneo utakaloweka duka lako, kuna maeneo wananunua bei na kuna maeneo wananunua brand. Ukitaka kufanikiwa hapa ngoja wakati ukiwa tayari kufungua duka basi fanya survey maduka ya wenzako wamestock nini kisha nenda kwa duka la jumla la eneo lako mwambie unataka ufungue duka la rejareja na ununue vipodozi kwake, muombe akuambie vipodozi vinavyotembea kwa wakati huo na vipodozi gani vya kuwa navyo anyway. Kwa hiyo ukiwa tayari kuingia sokoni ndo utafiti hili
3.Ni vipodozi gani vina faida kubwa sana = Vipodozi vyote vina faida kubwa sana. Faida inatokana na kasi ya kutoka kwa kipodozi husika na tofauti kati ya bei ya kununulia na kuuzia (profit margin). Kwa ushauri wangu ni bora uangalie mahitaji ya wateja wako kuliko faida. Unaweza kuweka vipodozi vyenye faida kubwa halafu vikawa havina movement kwenye location yako - utaangukia pua. Au unaweza kuweka vipodozi vya bei ya chini ambavyo wateja wako hawaviamini na wala hawavitumii.
View attachment 1078397
4.Hasara ambazo unaweza pata = Hili nimekuwa nikiwafundisha sana watu wanaokuja kujifunza kwetu biashara ya vipodozi A-Z. Zipo nyingi, ila karibia zote zinaepukika. Muuzaji kukuibia, adhabu za TFDA, adhabu za TRA, adhabu za halmashauri, vipodozi kuharibika, gharama za uendeshaji kuwa kubwa kuliko faida ghafi (gross profit) na kadhalika.
List ya vipodozi vilivyoruhusiwa kuuzwa na vilivyokatazwa kuuzwa zote zinapatikana kwenye tovuti ya TFDA: www. tfda. go. tz (Toa hizo space)
5.Sehemu ya kuweka duka(Matter of location) = Location kama kawaida, wewe tu na ubavu wako; ila ukipata mtaa wenye wakazi wengi au sehemu yenye movement nzuri ya watu - hususan akina dada basi umewin. Iwe ni njia ya kwenda university, mtaa wenye biashara ambazo wateja wake wengi ni wanawake, mtaani wanakokaa hao akina mama, mjini, sokoni nk. Zingatia sheria za TFDA, kuna baadhi ya maeneo hutakiwi kuweka duka la vipodozi (mfano karibu na kituo cha mafuta) hata kama kibiashara ni strategic location (Please kabla ya kulipia fremu kaonane na TFDA, eneo lako lisije kukataliwa wakati umeshalipia)!
6.Sehemu nzuri ambayo naweza fungasha mzigo kwa bei rahisi sana( iwe nje au hata ndani ya nchi hapa mkoa wowote ule) = Kariakoo is the best (ila usipokuwa makini inawezakuwa the worst)! Siku za kwanza nenda na mwenyeji tu hadi utakapomaster, vinginevyo utanunua kwa walionunua na hivyo kupata vipodozi kwa bei mbaya na kuuza kwa bei mbaya - kumbuka akina mama ni very sensitive kwenye suala la bei kwa hiyo ukiuza bei juu hata kwa tofauti ya Tsh 500/= tu basi watapita duka lako na kwenda kununua kwa jirani yako au hata mbali sana; unaweza kuhisi umerogwa, ila 500/= mwenzako anapata vocha!
Ila kitu kimoja - changieni maduka ya jumla ya mikoani kwenu. Kwa hiyo kama haupo Dar es salaam basi usinunue kutoka Kariakoo, tafuta maduka ya jumla hukohuko mkoani kwenu.
I am done & Out!
Ukihitaji kujua zaidi ya hayo basi karibu ..... nitakupa darasa zaidi maana kuna mambo kama 21 hivi ambayo nitakufundisha kwa wiki 1 (Kila siku nitakufundisha mambo matatu makubwa) kuhusu kuanzisha, kusimamia na kuendeleza duka lako la vipodozi ..... (Ila utanipodha soda mbili 😂😂😂 maana ni consultancy eti 🙂🙂🙂)
Viva JF!
AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS
0719326693 | 0743422883 | afyazaidi@gmail.com
WAMESHAKUJA KULETA MWONGOZO!!!
Kwa ushauri wangu. Usiende kariakoo kichwa kichwa utaumia. Tafuta mtu ambaye ameshawahi au anafanya hiyo biashara ongea nae kwa uzuri mweleze shida yako mpe hela ya soda kidogo, muombe muda wake kidogo uongozane nae mpaka kariakoo ili kununua mahitaji yako kwa usalama zaidi. Ukienda mwenyewe kariakoo basi jiandae kuuziwa bidhaa feki kama vile vipodozi fake au vilivyokwisha muda wa matumizi(expire) ambao unaweza kuja kukutia matatizoni iwapo watapita wakaguzi wa TFDA. Zaidi ya yote hongera kwa kuthubutu na Mungu akutangulie. Kila la kheri.Wakuu habar za weekend
Ndugu zangu naomben msaada kwa wale mliopitia kwenye biashara ya vipodoz.
Nina M5 ya mtaji nikatoa kodi na vibali na kila kitu nimebakiwa na pesa taslim M3 ndo nataka nianze kununulia mzigo.
Je kwa pesa hii naweza pata mzigo wa kueleweka yaan hata nikifungua duka likaonekana Lina hadhi yaan vile vipodoz muhimu nisivikose.
Pia naomben mnisaidie maduka ya jumla kwa k,koo yapo sehemu gan na kwa vile ndo mala yangu ya kwanza naenda na pesa zote taslm au nafanyaje maana naogopa kuibiwa pesa yenyewe ya kuchanga changa sna, na je ile list ya vipodoz watanipa wenyewe nikiwaambia nataka kufungua duka LA vipodoz maana wao wanajua vipodoz vyote vinavyotoka.
Au niende na list yangu mkononi nikifika nawatajia wananiuzia.
Naomben msaada jaman kwa waliopitia kwenye hii biashara.
Nawapenda
Kwa ushauri wangu. Usiende kariakoo kichwa kichwa utaumia. Tafuta mtu ambaye ameshawahi au anafanya hiyo biashara ongea nae kwa uzuri mweleze shida yako mpe hela ya soda kidogo, muombe muda wake kidogo uongozane nae mpaka kariakoo ili kununua mahitaji yako kwa usalama zaidi. Ukienda mwenyewe kariakoo basi jiandae kuuziwa bidhaa feki kama vile vipodozi fake au vilivyokwisha muda wa matumizi(expire) ambao unaweza kuja kukutia matatizoni iwapo watapita wakaguzi wa TFDA. Zaidi ya yote hongera kwa kuthubutu na Mungu akutangulie. Kila la kheri.
Mimi nasema kila siku kuwa haya mambo yawe yanafundishwa mashuleni na vyuoni huko. Tena liwe somo la lazima. Basic Entrepreneurship skills, Financial skills 101 na stadi zingine za lazima katika maisha ya sasa. Kweli mtu unaingia gharama za kuanzisha biashara ambayo hata hujui bidhaa utazipata wapi? Wateja je? Washindani wako? Gharama zingine? Angeweza kuandika ka business plan hata ka uongo na kweli au kufanya ka utafiti kuhusu mambo ya muhimu ya biashara hii angepata majibu yote ya maswali ya msingi.Maswali mengi hapa ulitakiwa uwe na majibu kabla hujafanya maamuzi ya kodi na vingine
Btw wanakuja wajuzi
AhsanteMimi nasema kila siku kuwa haya mambo yawe yanafundishwa mashuleni na vyuoni huko. Tena liwe somo la lazima. Basic Entrepreneurship skills, Financial skills 101 na stadi zingine za lazima katika maisha ya sasa. Kweli mtu unaingia gharama za kuanzisha biashara ambayo hata hujui bidhaa utazipata wapi? Wateja je? Washindani wako? Angeweza kuandika ka business plan hata ka uongo na kweli angepata majibu yote ya maswali ya msingi.
Nimemuelewa sana mdau hapo juu ntatumia hii ideaChukua ushauri huu simple wa huyu mdau.
Binafsi si deal na business za namna hii lakini njia rahisi ya kuanza biashara yoyote ni kuwa karibu na anayefanya hiyo biashara kabla yako.
Kama alivyosema mdau usisite kumpatia pesa ya soda (consultation) utajifunza mengi. Pia utaokoa muda na pesa yako.
Ahsante sna nimekupata vzr snaKwa ushauri wangu. Usiende kariakoo kichwa kichwa utaumia. Tafuta mtu ambaye ameshawahi au anafanya hiyo biashara ongea nae kwa uzuri mweleze shida yako mpe hela ya soda kidogo, muombe muda wake kidogo uongozane nae mpaka kariakoo ili kununua mahitaji yako kwa usalama zaidi. Ukienda mwenyewe kariakoo basi jiandae kuuziwa bidhaa feki kama vile vipodozi fake au vilivyokwisha muda wa matumizi(expire) ambao unaweza kuja kukutia matatizoni iwapo watapita wakaguzi wa TFDA. Zaidi ya yote hongera kwa kuthubutu na Mungu akutangulie. Kila la kheri.
Fata ushauri wa mdau ,pia fanya analysis uwatambue wateja wako,soko,faida , changamoto za hiyo biasharaKwa ushauri wangu. Usiende kariakoo kichwa kichwa utaumia. Tafuta mtu ambaye ameshawahi au anafanya hiyo biashara ongea nae kwa uzuri mweleze shida yako mpe hela ya soda kidogo, muombe muda wake kidogo uongozane nae mpaka kariakoo ili kununua mahitaji yako kwa usalama zaidi. Ukienda mwenyewe kariakoo basi jiandae kuuziwa bidhaa feki kama vile vipodozi fake au vilivyokwisha muda wa matumizi(expire) ambao unaweza kuja kukutia matatizoni iwapo watapita wakaguzi wa TFDA. Zaidi ya yote hongera kwa kuthubutu na Mungu akutangulie. Kila la kheri.
Humu ndani kila MTU mwalimu na amefanikiwa wala hakuna mbumbumbu, mm pekeangu ndo mbumbumbu niliekuja kuuliza sasa cjui huyo ndugu yangu alitaka nitapeliwe au niibiwe ndo niulize maana sioni kosa hapo bado Nina nafasi ya kufanya chochote nikipata mawazo kwa wadau walipitia humu.Tusipende sana kukosoa au kuongea ili uonekane umetoa point.. Mdau kauliza ajibiwe na sio kukosolewa. Toa ushauri baada ya ushauri toa changamoto na mrekebishe alipokosea. Ujasiria mali haupo darasani ni more practical than theory. Ndio maana hao wanaofundsha hawana hata genge la nyanya...
Tusipende sana kukosoa au kuongea ili uonekane umetoa point.. Mdau kauliza ajibiwe na sio kukosolewa. Toa ushauri baada ya ushauri toa changamoto na mrekebishe alipokosea. Ujasiria mali haupo darasani ni more practical than theory. Ndio maana hao wanaofundsha hawana hata genge la nyanya...
Anaona kama umeshalipa fremu na pia hujui lolote lile. Kila mtu na uandshi wake na pia kila mtu anazo njia za kutafuta information ya kupata kile anachoitaji..Humu ndani kila MTU mwalimu na amefanikiwa wala hakuna mbumbumbu, mm pekeangu ndo mbumbumbu niliekuja kuuliza sasa cjui huyo ndugu yangu alitaka nitapeliwe au niibiwe ndo niulize maana sioni kosa hapo bado Nina nafasi ya kufanya chochote nikipata mawazo kwa wadau walipitia humu.