Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo


Safi sana kwa muongozo wako mzuri.


Cc: mahondaw
 
Wakuu habari za muda huu kwanza natanguliza shukrani kwa wote wanaochangia kwenye jukwaa na kuzidi kupeana detail mbalimbali za biashara.

Naomba kujua kuhusu hii biashara ya urembo nikiwa na maana duka la kuuza bidhaa za urembo hasa vitu hivi:

1. Ukiwa Dodoma mzigo unaweza pata wapi au ni mpaka uagize kutoka Dar es salaam

2. Kwa anaefanya biashara hii ni mtaji kiasi gani unaweza husika kuanzia frem mpaka mzigo.

3. Na kuhusu taratibu za vibari ni vipi vinavyohitajika katika biashara hii.

NB: Biashara itafanyika Dodoma na sitaki iwe duka kubwa sana nahitaji la kawaida tu litakuwa jinsi Mungu atakavyo jaalia.
 
Wakuu habar za weekend
Ndugu zangu naomben msaada kwa wale mliopitia kwenye biashara ya vipodoz.

Nina M5 ya mtaji nikatoa kodi na vibali na kila kitu nimebakiwa na pesa taslim M3 ndo nataka nianze kununulia mzigo.

Je kwa pesa hii naweza pata mzigo wa kueleweka yaan hata nikifungua duka likaonekana Lina hadhi yaan vile vipodoz muhimu nisivikose.

Pia naomben mnisaidie maduka ya jumla kwa k,koo yapo sehemu gan na kwa vile ndo mala yangu ya kwanza naenda na pesa zote taslm au nafanyaje maana naogopa kuibiwa pesa yenyewe ya kuchanga changa sna, na je ile list ya vipodoz watanipa wenyewe nikiwaambia nataka kufungua duka LA vipodoz maana wao wanajua vipodoz vyote vinavyotoka.

Au niende na list yangu mkononi nikifika nawatajia wananiuzia.

Naomben msaada jaman kwa waliopitia kwenye hii biashara.
Nawapenda
 
Kwa ushauri wangu. Usiende kariakoo kichwa kichwa utaumia. Tafuta mtu ambaye ameshawahi au anafanya hiyo biashara ongea nae kwa uzuri mweleze shida yako mpe hela ya soda kidogo, muombe muda wake kidogo uongozane nae mpaka kariakoo ili kununua mahitaji yako kwa usalama zaidi. Ukienda mwenyewe kariakoo basi jiandae kuuziwa bidhaa feki kama vile vipodozi fake au vilivyokwisha muda wa matumizi(expire) ambao unaweza kuja kukutia matatizoni iwapo watapita wakaguzi wa TFDA. Zaidi ya yote hongera kwa kuthubutu na Mungu akutangulie. Kila la kheri.
 

Chukua ushauri huu simple wa huyu mdau.

Binafsi si deal na business za namna hii lakini njia rahisi ya kuanza biashara yoyote ni kuwa karibu na anayefanya hiyo biashara kabla yako.

Kama alivyosema mdau usisite kumpatia pesa ya soda (consultation) utajifunza mengi. Pia utaokoa muda na pesa yako.
 
Maswali mengi hapa ulitakiwa uwe na majibu kabla hujafanya maamuzi ya kodi na vingine

Btw wanakuja wajuzi
Mimi nasema kila siku kuwa haya mambo yawe yanafundishwa mashuleni na vyuoni huko. Tena liwe somo la lazima. Basic Entrepreneurship skills, Financial skills 101 na stadi zingine za lazima katika maisha ya sasa. Kweli mtu unaingia gharama za kuanzisha biashara ambayo hata hujui bidhaa utazipata wapi? Wateja je? Washindani wako? Gharama zingine? Angeweza kuandika ka business plan hata ka uongo na kweli au kufanya ka utafiti kuhusu mambo ya muhimu ya biashara hii angepata majibu yote ya maswali ya msingi.
 
Ahsante
 
Nimemuelewa sana mdau hapo juu ntatumia hii idea
 
Tusipende sana kukosoa au kuongea ili uonekane umetoa point.. Mdau kauliza ajibiwe na sio kukosolewa. Toa ushauri baada ya ushauri toa changamoto na mrekebishe alipokosea. Ujasiria mali haupo darasani ni more practical than theory. Ndio maana hao wanaofundsha hawana hata genge la nyanya...
 
Ahsante sna nimekupata vzr sna
 
Fata ushauri wa mdau ,pia fanya analysis uwatambue wateja wako,soko,faida , changamoto za hiyo biashara
 
Humu ndani kila MTU mwalimu na amefanikiwa wala hakuna mbumbumbu, mm pekeangu ndo mbumbumbu niliekuja kuuliza sasa cjui huyo ndugu yangu alitaka nitapeliwe au niibiwe ndo niulize maana sioni kosa hapo bado Nina nafasi ya kufanya chochote nikipata mawazo kwa wadau walipitia humu.
 

Ukileta jambo hapa hadharani tegemea cho chote mkuu. Unachukua kinachokufaa na kisichokufaa unakiacha. Ndo maana halisi ya uhuru na demokrasia tunayoililia kila siku; na wote hatuwezi kufanana kimawazo na kimtazamo. Ila kuanzisha biashara hata hujui bidhaa utazipata wapi, wateja wako wakoje, ushindani ulivyo na mambo mengine ya msingi siyo njia sahihi ya kuanzisha biashara !!!
 
Napenda pia kufanya hii biashara ila mtaji bado natafuta,Cha msingi tafuta location nzuri haswa kwa dsm,pia tafuta mfanyakaji wa dukan mwenye customer care nzuri coz wateja wako wengi ni wanawake,ndio maana maduka mengi ya vipodozi kwa dar wanaouza ni wanaume
 
Anaona kama umeshalipa fremu na pia hujui lolote lile. Kila mtu na uandshi wake na pia kila mtu anazo njia za kutafuta information ya kupata kile anachoitaji..

Na kweli unaeza kuta mtu kakosea ila toa ushauri na umuulize ikiwa na ulazima ili umrekebishe alipokosea. Ila moja kwa moja una mu attack kama mjinga sio poa..

Mwerevu ni yule anaejifanya mjinga kupata analoitaji..

Na kama umelipa fremu na kila kitu ni mambo yanayorekebishika.. Tafuta mtu aliewah kufanya biashara kaa nae chini. Na kama hujui bei zikiwa dukani kwa bei ya reja reja tafuta mdada au mkaka aliewahi kuajiriwa kaa nae hata mwez utapata idea na kurekebishA ulipokesea..

Watu wajibu ulilouliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…