Ufafanuzi: Nafuu ya kodi unapoagiza/kununua gari za Afrika Kusini

Ufafanuzi: Nafuu ya kodi unapoagiza/kununua gari za Afrika Kusini

Tafuta wateja tuu Mkuu gari yeyote inakuja iwe Lori mpaka hizi gari ndogo...gari za Friedge Truck zilifutwa Kodi mwaka huu huyo jamaa mwenye uzi huu atakua ajui pia tukimwambia na hiyo ni fursa ataikataa...iwe tani moja pick up walitoa nadhani VAT utalipia vitu vingine...
Nitaomba nikutafuta nikuombe mawazo kwenye hilo jambo
 
Nitaomba nikutafuta nikuombe mawazo kwenye hilo jambo
Nimefungua Kampuni ya utalii Arusha muda mwingi ntakua Arusha, Tanzania mwezi wa December ntakuwepo free hapo karibu kwa lolote magari nayafahamu maana mengine tunatengeneza kuanzia kuunga Chassis na likija Tanzania utakataa maana SA kila bati sijui fender na takataka zingine zipo madukani ni vitu vipya havibondwi kunyoosha...
 
Tafuta wateja tuu Mkuu gari yeyote inakuja iwe Lori mpaka hizi gari ndogo...gari za Friedge Truck zilifutwa Kodi mwaka huu huyo jamaa mwenye uzi huu atakua ajui pia tukimwambia na hiyo ni fursa ataikataa...iwe tani moja pick up walitoa nadhani VAT utalipia vitu vingine...
Nirushie namba inbox tuyajenge kaka
 
Isanga family msamaha wa Kodi ni kiasi gani kwa magari mapya toka SA?
Kipindi cha nyuma ilikua VAT 50% off miaka ya nyuma sema sijafatilia hivi karibuni ingawaje pana dogo alinunua hapo hapo Toyota alidai haikua na VAT % kabisa ingawaje sijafatilia kuhusu hilo maana ukinunua SA ukiendesha mpaka hapo naona Zakayo anaweza akagoma kuwa sio jipya nikamshauri aagize hapo hapo Toyota...
 
Huu uzoefu umeupata wapi mkuu gari za SA hata maroli ni imara sana kwa nini mnapenda kupotosha jamii ili iweje humu nikituma Gari za SA ukiambiwa ni used utakataa na pia ili upate huo unafuu wa kodi ni lazima uwe na karatasi za export za SA ambazo wanatoa Sunnyside pale...
Mleta uzi ana uzoefu kutoka kwenye Story za Vijiwe vya kahawa🤣
 
Website gani naweza browse kupata hizo used cars for SA?
Angalia tuu zipo nyingi ila Wasenegal wameingilia kati mifumo ya malipo imekua risk nina documents karibu mbili vijana walinunua tractor kwa kuwalipa hao jamaa nimeenda Interpol wapi Polisi wanasema tukio limefanyika Tanzania sio SA maana crime imefanyika mlipaji akiwa Tanzania na jamaa hao wezi wanaendelea kutangaza matrekta yao...SA ukienda trip moja ukapata taarifa za bank kutoka kwao zingine zote unaweza usiende au mtu alieko SA anauliza switf code za hiyo kampuni na akaunti yao basi...mimi huwa sipendi kurusha hizo site maana zimeingiliwa na wahuni wengi...
 
Habari wakuu.

Naomba kutoa angalizo ama ufafanuzi kidogo kuhusu nafuu ya kodi pale utakapoagiza gari zilizotengwa South Afrika.

Nimeona mijadala mingi humu watu wakisema kuna unafuu mkubwa wa kodi ukiagiza gari South Afrika kuliko Japan.

Hilo jambo linaweza kua sahihi ama linaweza kua na ukweli ndani yake ila kuna masharti magumu ya kufanya ili kupata hiyo nafuu.

Ni kweli South Afrika wanatengeneza baadhi ya models za magari 'exclusively' ya makampuni makubwa Duniani, kuna assembly plants za magari kama Toyota, Ford, Hammer, Benz, BMW, Nissan nk.

Ni kweli pia kwamba kuna makubaliano ya nchi za kusini mwa Afrika ama SADC kupeana nafuu ya kodi iwapo hicho kitu kimetengenezwa ndani ya nchi wanachama. Tanzania na South Afrika ni wanachama hivyo mikataba hiyo iko halali kabisa.

Pamoja na hayo, sharti la kupata nafuu ya kodi ni iwapo tu gari utakayoiagiza ni brand new zero kilometers, haijawahi kutumika mahala popote.

Iwapo utaagiza gari yoyote used kutoka kwa Mandela, hata kama ni ya mwaka huu 2022 ila used basi utalipa kodi kama vile ukiagiza Japan ama mahala popote Duniani.

Hivyo, usidanganywe na mtu kwamba South Afrika kuna nafuu ya magari, ni magari mapya tu.

Jambo lingine, kwa uzoefu wangu, Magari ya south Afrika hasa used yamechoka kuliko ya Japan ama Thailand. Kukuta gari ya South Afrika ya mwaka jana leo hii ina Kilomita 100,000 ni kawaida sana ila kwa Japan ni ngumu sana.

Wakuu, nimeona nijaribu kuchangia uzoefu wangu.

Nashukuru sana.
Point Mkuu. Ford Ranger nimeitumia South miaka 2 kufika Tunduma Kodi 32m
 
Tunachopaswa kuelewa
1. Je tofauti ya bei ya gari used japan na S.A zinarange kiasi gani (FOB)
2. Usafiri inakuwaje hadi linafika tunduma
3. Risk yake ipoje
4. Forodha na vibari vya interpol gharama zake zipoje

Hii yote tunafanya ili tulinganishe unafuu wa kuagiza S.A vs Japan
Mfano kwa sasa usafiri kutoka japan kuja huku upo juu sana je ukiagiza hilo gari utasave kiasi gani??
 
Back
Top Bottom