Ufafanuzi: Nafuu ya kodi unapoagiza/kununua gari za Afrika Kusini

Ufafanuzi: Nafuu ya kodi unapoagiza/kununua gari za Afrika Kusini

South Africa unafuu unakuja endapo gari ilizalishwa palepale. S.A ni member mwenzetu kwenye jumuiya ya SADC na kwenye hii jumuiya kuna makubaliano kwa ajili ya kukuza biashara kati ya nchi wanachama ambapo kodi ya bidhaa wanazozalisha wanachama hazitozi bei kubwa ili kupunguza importation ya nje.

Kwenye TRA used vehicle calculator baadhi ya gari za South Africa zimewekwa kama Fortuner na Ford Ranger. Ili upate unafuu wa kodi lazima ukienda TRA uambatanishe na certificate of origin au wao wakijua ilipozalishwa lazima kodi iwe tofauti na za Japan
 
Soma makubaliano ya SADC kwenye certificate of origin. Unafuu wa kodi uko kwa kitu ambacho ni brand new tu sio used.
 
Habari wakuu.

Naomba kutoa angalizo ama ufafanuzi kidogo kuhusu nafuu ya kodi pale utakapoagiza gari zilizotengwa South Afrika.

Nimeona mijadala mingi humu watu wakisema kuna unafuu mkubwa wa kodi ukiagiza gari South Afrika kuliko Japan.

Hilo jambo linaweza kua sahihi ama linaweza kua na ukweli ndani yake ila kuna masharti magumu ya kufanya ili kupata hiyo nafuu.

Ni kweli South Afrika wanatengeneza baadhi ya models za magari 'exclusively' ya makampuni makubwa Duniani, kuna assembly plants za magari kama Toyota, Ford, Hammer, Benz, BMW, Nissan nk.

Ni kweli pia kwamba kuna makubaliano ya nchi za kusini mwa Afrika ama SADC kupeana nafuu ya kodi iwapo hicho kitu kimetengenezwa ndani ya nchi wanachama. Tanzania na South Afrika ni wanachama hivyo mikataba hiyo iko halali kabisa.

Pamoja na hayo, sharti la kupata nafuu ya kodi ni iwapo tu gari utakayoiagiza ni brand new zero kilometers, haijawahi kutumika mahala popote.

Iwapo utaagiza gari yoyote used kutoka kwa Mandela, hata kama ni ya mwaka huu 2022 ila used basi utalipa kodi kama vile ukiagiza Japan ama mahala popote Duniani.

Hivyo, usidanganywe na mtu kwamba South Afrika kuna nafuu ya magari, ni magari mapya tu.

Jambo lingine, kwa uzoefu wangu, Magari ya south Afrika hasa used yamechoka kuliko ya Japan ama Thailand. Kukuta gari ya South Afrika ya mwaka jana leo hii ina Kilomita 100,000 ni kawaida sana ila kwa Japan ni ngumu sana.

Wakuu, nimeona nijaribu kuchangia uzoefu wangu.

Nashukuru sana.
Asante sana
 
Mali safi sana mkuu
Scania
Screenshot_2023-06-22-10-15-21-050_com.android.chrome.jpg
 
Usiache kuwaeleza kuwa hizo gari za kutoka Riyaadh ni lefthand
Naomba ufafanuzi chief....ina maana hizo gari zina punguzo la ushuru kutokana na kua ni left handed au ni sababu zinatoka Riyadh
 
Back
Top Bottom