Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Status
Not open for further replies.
Kuondolewa kwa Zitto Chadema ni hasara kwa CCM maana waliwekeza sana kwake !
Lakini pia ni hasara kwake maana hatoendelea kutumika.
Na pia ni faida kwa yale mashirika ya umma aliyokuwa akiyakamua
 
Tuliwavumilia sana, sijui kwa nini waliwachelewesha?
 
Kuondolewa kwa Zitto Chadema ni hasara kwa CCM maana waliwekeza sana kwake !
Lakini pia ni hasara kwake maana hatoendelea kutumika.
Na pia ni faida kwa yale mashirika ya umma aliyokuwa akiyakamua

Ndo ajue maana ya kutumika Kama co.nd.om.... Mwisho wanamtupa... Watetezi wake humu ambao wengi ni wafuasi wa CCM walitakiwa waanze kumkaribisha kujiunga nao ila kuna aliyesema Zitto hawezi kuongoza chama makini Kama CCM and they are the same people who were defending him here.... He he heeeee!! Zitto ulishauriwa sana lakini tamaa imekuponza kijana mdogo
 
Last edited by a moderator:
kujifariji kupo, lkn ukweli maamuzi ya kuwafukuza kina zitto na mkumbo yamewacost sana tena sana. si kila wakati ubabe unasaidia kujenga.


Dr Slaa na Mbowe na wenzao pamoja na vifaranga vyao wataisoma namba. na nnasubiri yule makamo wa bara nae karibu atoe tangazo la kujiuzulu.

na kila ataejiuzulu mwiteni mamluki au msaliti. Mnalo hilo. walipokuwa wakijenga chama kwa damu zao hamkuona uzalendo wao ?


poleni ndugu zangu na kwa kweli mnashuka vibaya sana
 
kweli chama kimechukua maamuzi mazito

Kuna watu Arusha na kwingineko walikufa kwa ajili ya CHADEMA na kuna maelfu wapo gerezani kwa sababu ya CHADEMA!

Kama kweli kuna usaliti miongoni mwa viongozi wake ni jambo la kushangaza itakuwa!
 

....you have said it all doctor!
 
Last edited by a moderator:
safar ndo imeanza wasaliti wote wawajibishwe maana sio tunaumiza vichwa kwa ajili ya mabadiliko wakati kuna wenzetu wana tu backbite
 

Hongereni sana Viongozi wa CHADEMA kwa maamuzi magumu na mazuri kwa wakti mwafaka!Mungu awabariki sana.
Hapa CHADEMA mmemaliza mchezo! Kama kutakuwa na Mtanzania hataelewa uamuzi huu basi ni Mhaini na haitakii mema Tanzania yetu!

Mtu yeyote haini iwe ndani ya Chama au Serikali anastahili kusulubishwa kwa kufukuzwa kazi,kufungwa maisha au kunyongwa! Ulizeni walioko Jeshini au waliopitia huko.......!

Sasa Watanzania wanaweza kujua wazi kabisa kuwa Zitto Zuberi Kabwe ni mtu hatari sana katika Jamii ya Kitanzania. Kama ameweza kukisaliti chama ni wazi kabisa anaweza kuisaliti hata Nchi yetu Tanzania. Huyu siyo mtu wa kuamini hata kidogo. ZZK ni Mbwa Mwitu ndani ya ngozi ya Mwanakondoo!

Sasa naweza kujua ni kwanini alikuwa akifanya usanii kwenye maswala ya msingi ya Chama. Baada ya kugundulika njama ya kukihujuma chama na kuomba ajiuzulu na kukataliwa ndipo akaanza kelele za mara nimepigwa mishale sana, nimesemwa sana, CDM haijawahi kukabidhi mahesabu ya Chama kwa CAG, mara hataki Posho ya Vikao, mara yuko nje ya nchi anafuatilia Fedha ya Tanzania iliyofichwa ughaibuni, mara ana udhuru wa kuhudhuria kikao cha CC etc,etc! yote hii kumbe ilikuwa danganya toto! ZZK alishajua AMENYEA KAMBI hakuwa na namna ya kukwepa kibano ndiyo maana akanza kuweweseka!!!!!!

Pole sana Bwana ZZK. Ukweli ni kwamba Umetuangusha Vijana wengi sana wa Kitanzania ambao tulikuwa na imani na wewe na tulikuchukulia kama a Political icon for this generation but now you have totally let us down!
Tunaomba kwa heshima na taadhima urudi kwa HAO WALIOKUTUMA wakakupe kazi nyingine itakayokufaa zaidi! Tunajua ulikuwa uko karibu sana na JK na Vijana wake kwa hiyo utakuwa unarejea nyumbani kwenu kwa shangwe na hoihoi!!!

Kwa vile Ubunge ni haki yako uliyoipata kupitia CHADEMA utaendelea kuingia mjengoni kwa raha zako. Tunaomba tu usije ukaanza kuchukua posho za Ubunge kwa vile sasa mrija wa CDM umekatika!!!!Tunajua ulishaaga jimboni kwako kuwa mwaka 2015 hutagombea tena Ubunge, nasikia una mpango wa kugombea Urahisi kwa tiketi ya CCM. Kila la kheri mwanakwetu, katusalimie Chigoma na ukale migebuka kwa wingi.

Alamsiki.
 
Wadau, baada ya kusoma andiko la huu mpango mzima nimekuta napata swali hii, hivi haya yote yalikuwa ni kwa manufaa ya nani? Bado naendelea kutafajari sijapata majibu. Hebu tutafakarini pamoja ili ikiwezekana tupate majibu pamoja
 
Wadau kwa mwenendo wa kinafiki wa dr kitila ni wazi kua amei aibisha jumuia nzima ya udsm,kama msomi mzima anakosa misimamo,anakua na ndimi mbili vipi kwa malayman? inatia hasira kuona mtu anaeitwa msomi anakua kinara wa kurudisha nyuma harakati za kuikomboa nchi yetu,tabia ya kinafiki ya watu dizaini ya kitila si ya kuichekea popote pale iwe cdm,ccm,cuf,nccr whatever.

UDASA imekua ikipwaya shauri ya mwenendo wa watu kama mkumbo,swali la kujiuliza ni hili kwa vipi prof baregu alitimuliwa udsm kwa sababu tu alikua cdm na kitila mpaka leo bado yupo ilihali ana faamika kua ni cdm? jibu nadhani umeshalipata.....mkumbo ameitia aibu jumuiya ya wasomi wa UDSM.
 
Taarifa kutoka katika vyanzo vya kuaminika
kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
demokrasia na Maendeleo ambae pia ni mbunge
wa jimbo la mpanda Said Arf ameweka nia ya
kujiuzulu nafasi yake hiyo na anatarajia kuita
vyombo vya habari kutangaza azma yake hiyo.
Naomba kuwasilisha.
UPDATES:
Said Arfi - Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA
amejiuzulu rasmi nafasi yake jioni hii.
Arfi ambaye pia ni mbunge wa Mpanda mjini
(CHADEMA) amefikia uamuzi huo leo baada ya
Kamati Kuu ya CHADEMA kuwavua uongozi Zitto
Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo.
Nafasi ya Zitto amepewa mchungaji Peter
Msigwa
=============
BARUA YAKE YA KUJIUZULU:
UPDATES:
Prof Baregu nae ajiuzulu nafasi zake ndani ya
Chadema. Nitawapa taarifa zaidi, kama kutakuwa
na tamko la maandishi la kujitoa kwake.....
 
Kama kweli CDM imefikia maamuzi haya kwa kuzingatia tu, ule waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, basi ninadhubutu kusema uongozi wa Chama ni wepesi.

Mbona yaliyomo kwenye huo waraka ni changamoto za kawaida kabisa kwa Taasisi kubwa kama CDM

Yaan wanachama kuweka mkakati wa kumsimamisha yule wanayemtaka inakuwa nongwa!

Labda kama kuna sababu nyingine
 
CDM ndo chama imara cha upinzani hilo halina ubishi, kina watu imara na makini. Msiogope kwani CDM si mtu mmoja. Ushauri kwa ZZK kama kweli aliyotendewa na kamati kuu ni ya kweli hakika ZZK usaliti ni mbaya sana, utajaribu kuukimbia lakini utakufuata wewe kwani utakuwa umekaa ndani ya nafsi yako popote utakapoenda, kukiri na kuomba msamaha ndo muamara wake. Kama umesingiziwa na kamati kuu nakuomba utulie, Mungu atakuwa upande wako popote pale. CDM bado kitakuwa imara sana,kwani ndani na nje ya chama kuna watu wako tayari kufa na wengine wametangulia mbele ya haki kwa ajili ya chama na kwa ajili ya Taifa lao.
 
Nashukuru kwa taarifa hii kwa watanzania wote wapenda mabadiliko.Naipongeza kamati kuu ya CDM
kwa kuchukua maamuzi magumu.Binafsi naamini kupitia hili hata mkichukua serikali hakuna waziri atakayevumiliwa kwa sababu ya umaarufu wake huku akiendeleza yasiyositahili kwa watanzania.
Naamini,kila mtu mzalendo angependa kuona tanzania inakuwa na amani na utulivu wa kweli
Nasema amani na utulivu wa kweli nikimaanisha hata mwenye njaa huonekana mtulivu,kumbe ni
kwa sababu ya njaa.
Nasubiria uzalendo wa akina Zitto na wenzake kwa taifa hili kama yale waliyoyasema ndivyo walivyokuwa wanamaanisha.
Nikiwa na maana kwamba,kama kweli akina zitto walikuwa wazalendo,hatutegemei malumbano bali watatafuta vyama vingine
waendeleze mapambano na kuhakikisha watanzania wanapata amani ya kweli(hapa nitoe mfano wa kafurila anajenga taifa akitokea NCCR).
Lakini kama walikuwa masalia,tunategemea kuona wakiungana na waliowatangulia kupita mikoa kwa mikoa
kuvunja yale waliyoyajenga na hapo ndipo nitakapojua kuwa mwana wa nyoka naye ni nyoka.
Nawaomba watanzania wote wapenda mabadiliko tusife moyo bali tuombe Mungu tumalize safari hii salama.
Sisi tusimame imara.
Tungependa kuiona tanzania yenye vyama viwili au vitatu vyenye nguvu ya kubadilishana madaraka na siyo
mfumo wa chama kimoja ktk taifa lenye vyama vingi,na hii itawezekana tu pale ambapo wanachama fulani
watakuwa wanachama wa ukweli,siyo wale wa mfumo wa ninanufaika kivipi nikiwa mwanachama wa chama husika.
 
Nakubaliana nawe mleta mada. Makongamano anayoyaandaa pale UDSM hues na mwelekeo wa kuiumiza CCM but kwa nini Bado yupo??????
 
finally I feel relieved for Chadema to get rid of that betrayal, now he can use the money he can being getting from ccm to start businesses or new political party
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…