Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Status
Not open for further replies.
Ha ha ha!
Na utanaki eke yako ukiona vivuli vya CHADEMA wakati hata Mbunge wako amesepa!
Nyumba inaanguka hiyo!
 
Lissu anasema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.

Duh. Walishaomba kujiuzulu? Kama hii ni kweli (na nadhali hili lina ushahidi kwa kuwa waliwasilisha barua), basi hawa jamaa wamepata haki yao. I have always given Zitto the benefit of the doubt. Ila kwa hili, nadhani hatima yake CHADEMA imewadia. Na sijui ni nini mustakabali wake kisiasa?
 
Chadema Daima.
Wazalendo wote ktk Taifa changa kama hili" Tunahitaji umoja, Kwa Maana umoja Wetu ndio Nguvu, Haiwezekani Watanzania tunahitaji Ukombozi wa Mara ya pili, Kupitia Chadema, Sasa watu wanapoanzisha chama ndani ya chama ndio ukpmbozi gani.
Taifa linahitaji kamati maalum za kushughulikia matatizo ya wananchi na sio makundi ambayo zitto analeta.
Taifa vile vile linahitaji chama makini jasiri na chama hicho si kingine bali ni Chadema, Ni Matumaini yangu kuwa chadema kitazidi kuungwa mkono zaidi na watanzania wa kada zote.
 
hiyo siyo sababu, mbona hata CCM walimfukuza yule Mzenji hata NCCR walimfukuza David, pia CUF Rashid

SEMA JINGINE UELEWEKE, !
 
Mkuu nimeiona hii, mbona kwenye hili Zitto bado ni mshindi kaka. Tunasubiri kauli ya Zitto tujue what next.
mwenyewe amesha kubali ana ukimwi na amejipanga kuishi kwa matumaini; wewe unaekataa hana ukimwi tunakushangaa!
 
chadema ni chama makini but wanafiki wataanza kuponda uamuz sahihi ulioafikiwa na makamanda wakuu,ccm jiandae kisaikolojia
 
Chadema Daima.
Wazalendo wote ktk Taifa changa kama hili" Tunahitaji umoja, Kwa Maana umoja Wetu ndio Nguvu, Haiwezekani Watanzania tunahitaji Ukombozi wa Mara ya pili, Kupitia Chadema, Sasa watu wanapoanzisha chama ndani ya chama ndio ukpmbozi gani.
Taifa linahitaji kamati maalum za kushughulikia matatizo ya wananchi na sio makundi ambayo zitto analeta.
Taifa vile vile linahitaji chama makini jasiri na chama hicho si kingine bali ni Chadema, Ni Matumaini yangu kuwa chadema kitazidi kuungwa mkono zaidi na watanzania wa kada zote.

CDM inaonyesha njia! Ndivyo nchi inavyotakiwa kuongozwa hakuna alie maarufu zaidi ya nchi!
 
Siku zote ustaarabu unaanza kwa jamii husika kujisafisha na kujichuja ikiwezekana hata kwa uamuzi mgumu,HONGERA CDM kupita katika wakati huo mgumu,ninachosubiria ni magamba kukosa inside men ndani cdm katika wakati muhimu wa kuelekea 2015!
 
hapa nilipo natafuta penye mkaa niichome moto hii kadi ya Chadema.

Nimechoka Upuuzi wa haya majamaa.
 
zitto aondoke bhaana , watu tukale posho na kupumzika Dubai ! hawajui chadema ni ya kaskazini .....? zile hesab jamaa alikuwa anaitaji kwenye kamati Fulani spidi itapungua sasa........
 
Kweli kabisa,hii ndio chadema tunayoitaka.Kama chadema inataka kuongoza nchi ilhali haiwezi kufanya maamuzi yoyote isingetufaa chochote maana ingekuwa ni ccm in different clothings.
Hii inatutia hamasa kwamba hawa jamaa serikali yao itakuwa inauwajibikaji.HONGERENI CHADEMA CC.
 
Wana Jf

Hapo mwanzo, mtumishi mkuu wa serikali ya CCM mtume Wasira Stephen alitabiri kuparaghanyika kwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania (Chadema). Na sasa utabiri huo umekamilika na haya yote yamethibishwa na hizi breaking news na live update zinazotokea hapa jamvini zinazogusa uongozi wa juu wa chama cha chadema.

My take; kwa siasa hizi za tanzania!!!! nini matumaini ya watanzania waliochoka na udhalimu wa serikali ya CCM????
 
Taarifa zilizopo sasa huku MTWARA wananchi wamefurahi sana maamuzi yaliyofanyika CHADEMA,hivi sasa wanafanya maulid kubwa sana hapa na naziona kadi nyingi sana za CHADEMA zikiteketea kwenye moto mkubwa sana.

Weka ushahidi wa picha mkuu usibwabwaje tuu
 
Live Updates: Ndugu Wanachama na Watanzania na wote muda si mrefu tutawaletea Mkutano na Waandishi wa Habari kuwajulisha Watanzania maazimio na maamuzi ya Kamati Kuu iliyokutana kwa siku mbili tarehe 20-21/11/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam

================
UPDATES

- M/Kiti Mh. Freeman Mbowe ameshawasili na ameanza kwa kusema kuwa Kamati Kuu imemteua Mh. Tundu Lissu kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama na pia Kamati Kuu imefikia maamuzi ya kinidhamu kwa baadhi ya viongozi.

Anamkaribisha Mh. Tundu Lissu kwa ajili ya kutoa taarifa ya maazimio ya Kamati Kuu kwa niaba ya M/Kiti

- Tundu Lissu anaanza kwa kusema kuwa Kamati Kuu imenasa waraka wa mkakati wa siri wa kukipasua Chama vipande vipande unaohusisha watu wanne ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana.

- Anasema lugha iliyotumika katika waraka huo ni ya siri ambapo kuna mtu anaitwa MM ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr. Kitila Mkumbo, M2. Hajajulikana na Dr. Mkumbo alikana kumfahamu kabisa M2, na M3 ni Mwigamba.

Lissu anasema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA.

Lissu anasema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu

- Anasema Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.

Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake

Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.

- Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

- Lissu anasema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.

- Kamati Kuu pia imeazimia kuusambaza waraka huo kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili watanzania waone na kujua ukweli.

Lissu anamalizia kwa kuwaomba watanzania na Wanachama wote wa CHADEMA nchi nzima wasife moyo na waendelee kukijenga Chama na nchi yao.

- Kamati Kuu pia imemteua Wakili Msomi Mh. Peter Kibatara kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chama

- Mh. Mbowe anasema waraka wa siri za Zitto haukutengenezwa wala haukutoka Makao Makuu. Alikuwa akijibu swali la Mayage kuhusu zitakapopatikana fedha za kutekeleza mpango huo

Hawa walikua ni mzigo na wanafiki wakubwa na wasaliti wa Watanzania wengi walio maskini kwa kuendekeza maslahi yao binafsi huku wakijinasibu watetez wa wanyinge.Nashauri isiishie tu kuwavua uongozi wa chama bali wafukuzwe kabisa uanachama na naomba hata vyama vingine vya siasa visiwapokee watu wa nanma hii.
 
Nimeamua kuchukua uamuzi huo baada ya kugundua kuwa CDM:
1. Inaongozwa na kamati ambayo imejaa great thinkers na wanafanya kazi kwa maslai ya chama na Taifa kwa ujumla.
2. Kamati iko tayari kufanya maamuzi magumu mda na wakati wote inapobidi.
3. Chama kimedhamilia kweli kuchukua NCHI ifikapo 2015 hivyo hakiko tayari kuwavumilia mawakala (vipandikizi) wa vyama vingine.
4. Chama kina dhamila ya dhati ya kumkomboa Mtanzania.

Hayo ni machache sana tu. Naipenda CHADEMA na nitaendelea kuipenda.
PAMOJA TUTASHINDA

Karibu sana kamanda tuungane kuutokomeza ugonjwa wa ukoma uitwao ccm.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom