Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Status
Not open for further replies.
Maamuzi ya Chadema leo hii ni maamuzi ya kijasiri na yanayoakisi msimamo wa chama dhidi ya mafisadi,wezi,wazembe,wanafiki,waoga,waroho,wenyewivu,wakatili,wabinafsi,vigeugeu,wadini,wakabila,wachawi,ndumilakwili, wavivu,wachoyo,majuha,wenye viburi,wadhihaki,malimbukeni,mamluki, wajivuni,wasiojali,mabwanyenye,wajuaji na WASALITI.

Nitashangaa sana watu wa namna hii wakiachwa kuendelea kukaa chamani na kufubaza harakati za ukombozi!

Kuna wanaotakiwa kuheshimiwa na kuenziwa kama yayi katika chama lakini si hawa waliopewa siku 14....rejea watoto waliokufa soweto -Arusha.

Siku 14 za hukumu ni nyingi mno kwani madhila waliofanya dhidi ya chama,wazalendo na wananchi ni makubwa mno.....hawastahili siku 14 bali bakora 14 wakahadithie vizazi vyao!

Siku 14 zisitumike kumeza matapishi bali zitumike kupeleka taarifa kwa yule yoyote awaye msaliti...kwamba hatujali jina,umri,dini,cheo,elimu,umaarufu,ukwasi au jinsia .....ukichezea mafuriko ya mabadiliko basi utasombwa tu!

Siku 14 za kupeleka ujumbe kwa Wassira na wenzi wake kwamba we are here to stay!

Ni SIKU 14 ZA HITIMISHO LA MAAMUZI!!

Ni siku 14 za kubaki na sisi wananchi au zitto.....Naam ni siku 14 za mwisho wa hili zimwi litujualo..,.!

Cc: Mungi LiverpoolFC Crashwise meningitis Mzeewarula Ritz et al
Ni siku 14
 
Last edited by a moderator:
Yangu macho na masikio ila siamini kama democracy inaweza kuchezewa kiasi hiki tena na mtu ambaye binafsi namwamini 'philosopher of theology!
 
mi wakigoma zzk za kabulu ndo walewale m2 unamuamini mwisho wa siku anakugeuka na hii yote tamaa kama alikua na nia ya madara angesubiri mda wake ungefika angeongoza
 

Nimependa uchambuzi wote...
 
Last edited by a moderator:
Iko haja ya kutazama upya namna yetu ya kufikiri juu ya chama kama taasisi na si mtu fulani kwa sababu flaniflani. wengi tumejilemaza sana na umaarufu wa watu na kusahau umuhimu wa vyama imara na thabiti. mfumo wetu wa kuendesha serikali ni wa siasa, chini ya taasisi yaani vyama vya siasa, hivyo, ili kua na serikali makini, ni lazima uwe na mfumo makini sana wa siasa. maamuzi ya kamati kuu ya CHADEMA yanatupa kufikiri zaidi juu ya mifumo yetu ya siasa. awali tumekua very myopic wa kufikiri, tumejenga fikra zetu katika unyonge wa kuogopa umaarufu wa mtu ndani ya vyama vyetu hii imepelekea kuwapa watu maarufu ujasiri wa kujiona wako juu ya mfumo mzima wa taasisi, na kwa makusudi kabisa wanasahau kua umaarufu wao walionao ni kwasababu taasisi imewalea na kufanya wawe leo walivyo, wanatumia umaarufu wao kufanya chama kile 'mlamba viatu' wao. hapana. lazima badiliko liwepo. watu wote wenye hekima za kipumbavu namna hii lazima wakemewe na kudhibitiwa vikali, hata kama itagharimu nusu ya chama ni heri sana. hatuwezi kamwe, kujenga chama chini ya huruma au woga wa umaarufu wa mtu ambae ni kinda la chama, kamwe.

Endapo chama kitaogopa gharama ya kuwakemea na kuwadhibiti hawa, basi kitaanguka na kufa wakati wowote bila gharama yeyote. ukijenga taasisi kwa gharama kubwa 'risk' ya maamuzi magumu, kamwe haitaanguka kirahisi.
bila kua mnafiki, nasema, zitto kabwe alionesha kua mwanasiasa mahiri, amelelewa na chadema na kufahamika uwezo wake mzuri akiwa ndani ya chadema, lakini kamwe hii haitishi hata kwa dakika, kua sababu ya kumuonea haya kumkemea na kumdhibiti anapokua na dalili za ukinzani mbaya/ usaliti au kwa kua neutral huku akijifunika na kivuli cha uzalendo, si kweli kua kua mzalendo ni kutothamini chama kilichokupa kuonekana katika jamii kua mtu makini.

Udhaifu wa kuweka taasisi nzima rehani kwa umaarufu wa mtu mmoja una madhara makubwa sana. mtu hataishi vizazi vyote, upo mwiso wa maisha, pili mtu anamaamuzi binafsi, anaweza akasema sitaki tena siasa! je chama kama taasisi tumlambe viatu kwajili ya huruma ya umaarufu wake? kesho anaweza kusema anahama chama, je tumlilie kwa ajiri ya umaarufu wake? lazima tupevuke sana, tujenge taasisi za siasa imara ili zidumu hata vizabi vijavyo!
 
Mtakumbuka Nccr Mageuzi walikuwa na katibu mkuu W.Kaborour na alipendwa sana ndani ya chama lakini baadae alikuja kununuliwa na ccm na kuiacha nccr katika mazingira magumu sana.

Nitalizungumzia kidogo tu kuhusu swala la Zitto, Zitto ni kiongozi mzuri ila nimwonavyo mimi anatamaa ya madaraka kwanini nasema ivyo, ukisoma waraka iliyotolewa na kusema ndio iliyosababisha akavuliwa vyeo ndani ya cdm. Na kuna matoleo mengi ambayo ukifuatilia huko nyuma alizokuwa akitoa Zitto zinadhihirisha kuwa aliitaka cheo cha uenyekiti tangu muda mrefu.

Wanasema kuna kipande kilingolewa kwenye katiba, kama walikuwa wanalijua hilo ilikuwaje wakae kwa kipindi chote hicho bila kukizungumzia ndani ya vikao vya chama. Kama naibu katibu mkuu analalamika je ww mwanachama wa kawaida itakuwaje.

Wanasema Zitto ni msomi sikatai ni msomi na angetumia usomi wake katika kubadilisha cdm na kuijenga, kubuni mbinu mbalimbali za kuliingizia chama mapato. Kwani alishindwa nini kwa muda huo wakati yeye ni naibu katibu mkuu wa chama. Ina maana yeye hizo mbinu na mikakati anaweza kuzitoa mpaka tu awe mwenyekiti wa chama?

Wanasema uchaguzi wa chama ulifanyika 2009 ukiangalia uchaguzi mwingine ilikuwa/inatakiwa ufanyike 2014. Ila chama walifikiria uchaguzi ufanyike mwaka huu ili mwakani waweze kuwa na mikakati mingine. Lakini hii haikuwa rasmi ilikuwa inaweza kubadilika wakati wowote kutokana na mikakati ya chama. Haya maneno ya kutofanya uchaguzi wangeyatoa mwaka 2014 kama ingevuka bila uchaguzi kufanyika lakini sio sasa.

Ukiangalia cdm zitto alikuwa/ananguvu sana ndani ya chama na anapendwa na wengi kiasi kwamba hata ingefika mwaka 2019 kama labda Mbowe angepewa nafasi nyingine ya kuongoza kwa vyovyote vile Zitto ndio angepata hiyo nafasi hapa hakuna mizengwe na isitoshe Slaa akigombea urais 2015, Kwa vyovyote Zitto angegombea urais 2020 na hapo umri wake ingemruhusu kugombea.

Tatizo la Zitto anakuwa na haraka bila sababu nafasi yake katika uenyekiti na ugombeaji urais katika cdm upo. Ila yeye niwazavyo mimi alitaka madaraka kwa haraka chama kimetoka mbali na yeye alitakiwa kuvumilia na kuendelea kukijenga Cdm. Ndio maana nakuwa na mawazo kuwa labda alikuwa au anatumiwa na ccm. Na ndio maana yananikumbusha ya W. KABOUROUR wa nccr.

Zitto alikuwa mtu mkubwa katika cdm naibu katibu mkuu sio cheo kidogo,hakutakiwa kulalamika kila mara kwenye mitandao au kutumia watu atuambie alikaa wapi katika vikao vyao vya chama na kueleza namna ya kukijenga chama na kamati wakampuzia na kumkatalia. Wangemkatalia angejiuzulu unaibu katibu mkuu na wana cdm wangekuwa upande wake. Sio anavyotaka yeye kuwa cdm itaweza kwa yeye kuwa mwenyekiti kwanza si kweli hapo alipokuwa angeweza kufanya makubwa. Lakini mengine tulikuwa tukiyaona kwenye baadhi ya kukiendeleza chama atakuwepo kwa kipindi fulani au usimwone kabisa.

Kilichopo atulie na kutafakari ni wapi alipoteleza kwani katika cdm bado anayo nafasi kubwa asiwe na tamaa ya kukimbilia chama kingine au kuanzisha chama hapa ataonekana kumbe lengo lake lilikuwa ni uongozi.
 
kigoma bwana tunatia aibu alianza kabulu akapendwa sana ikafikia hadi kubebwa kama mfalme akafuata daniel nsanzugwanko wa kasulu na sasa huyu zito jamani jamani wakigoma tubadilike tuwenamisimamo isiyoyumbishwa na kitu chochote tutashindwa kuaminiwa mbele ya uso wadunia
 
Nawapongeza kuchukua mamuzi mazito ambayo hayakuangalia umaarufu, cheo cha mtu wala athari inayoweza kutokea ndani ya chama. Hilo ni sahihi na manastahili pongezi.

Lakini ni muhimu kamati kuu kuzingatia hoja za msingi zilizotolewa katika waraka wa mabadiliko na kutuweka wazi kama hiyo ndio hali halisi iliyopo andani ya chama. Je ni kweli mahesabu ya chama hayakaguliwi? Je ni kweli viongozi hamna mikakati yoyote ya kuendelza chama mfano kuanzisha miradi kwa ajili ya kuimarisha chama kimapato. Namengine mengi yaliyotolewa si ya kuyapuuza hata kidogo bali nikayatolea majibu sahihi kuliko kuonekana ninyi mnajua kuchukua maamuzi magumu bila kujibu hoja za msingi zilizopelekea kundi hilo kufikia maamuzi yakuandaa mtandao wa kugawa chama. Tunahitaji majibu ili tujue kuwa huo mtandao ulikua na nia mbaya au la walikua katika hali ya kukinusuru chama kifikie malengo tuliyokusudia baada ya kuona labda ngazi ya juu mmelala.
Tunahitaji majibu na uwazi kuhusiana na hoja zilizotolewa

Nawasilisha
 
Hoja za kijinga tu hizi.
 
Walid Aman Kabourou alikuwa makamu mwenyekiti wa Chadema na siyo Nccr. Mada yako irudie au ifutwe, haistahihili kuchangiwa!!!!
 
Hakuna mtu ambaye ni zaidi ya Chama! Anaruhusiwa kumfuata mmewe!

KNCU Mnajifanya mmewasimamisha akina KITILA kana kwamba ni wasaliti kumbe sababu ni itikadi za kidini na ukabila unaoitafuna CHADEMA.
 
Sijawahi katika maisha yangu kuelewa shabaha ya zitto kisiasa, kama ambavyo roho yangu ilisita kabisa kumkubali jakaya kikwete kuwa raisi kipindi kile akiungwa mkono kwa zaidi ya asilimia 80, rekodi ambayo kamwe haitakuja kuvunjwa katika uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi. Nimejiridhisha siku nyingi kuwa zitto anatafuta aidha asichokitaka ama asichokijua manufaa yake siku akiwa anafanya bethidei yake ya miaka ya 40!
 
Napendekeza Ben Saanane ateuliwe kuwa Naibu Katibu Mkuu na Mkuu wa Kanda ya Magaharibi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…