kidi kudi
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,450
- 2,013
Wasalaa wanajamvi.
Naomba nijielekeze kwenye mada moja kwa moja.
Nina rafiki yangu hivi karibuni miezi michache imepita aliniambia anafikiri ana tatizo la kifua baada ya kukohoa kohozi lenye damu.
Ukweli niliogopa kwani nilihisi haraka haraka atakua na TB hivyo nikamshauri akachek hospitali. Japo mwanzoni hilo la kwenda kupima alikuwa akilipotezea lakini siku moja alikubali na kuniomba nimsindikize hospital.
Tulienda na akaenda kupiga x- ray na kisha kupewa vikopo vya kuweka makohozi. Alipotoka kwa daktari nilibaini amekua mnyonge sana tofauti na nnavyomjua, hilo lilinipa mashaka kidogo japo sikumuonyesha.
Siku ilofuata tulirudi tena hospitali kufuatilia majibu ya makohozi, ndipo nilipomuona akitoka na daktari wakapelekana hadi clinic ya CTC. Kiukweli nilianza kupata majibu ya kwanini rafiki yangu huyu jana yake tulivoenda mara ya kwanza alikuwa na hali ya utofauti kidogo.
Niliendelea kumsuburi takribani saa zima kisha akaja huku machozi yakimtoka, akaja akanikumbatia kisha akaniambia twende nyumbani tukifika kuna jambo atanishirikisha kwavile mimi ni rafiki yake mkubwa( tangu sekondari A-level hadi university tumesoma wote tena kozi moja na bahati nzuri kazi tumepata sehemu moja).
Kweli jioni ya siku hiyo alinipigia simu tukaenda sehem moja tulivu akaagiza nyama choma na kisha tukaanza maongezi taratibu. Ndiposa akafunguka alichopanga kuniambia.
Aliniambia kwamba siku zote alikuwa anajisikia kuumwa kifua na kukohoa sana akajua fika tayari atakua na TB na ikibidi UKIWMI vilevile. Nkamuuliza kwanini, kweli alinipa jibu ambalo mpaka leo nikimuona rafiki yangu huyu nakubali kuna watu ni majasiri na wana mioyo mipana.
Aliniambia kuwa aliekua mpenzi wake ni muathirika [mpenzi wake amekua nae kwenye mahusiano takribani miaka 4 tangu tukiwa chuoni, na sasa hivi wamevunja uhusiano kwa sababu ambazo ni nje ya ishu ya ugonjwa.] na alijua kuwa ni muathirika mwaka mmoja uliopita.
Alinieleza pia baada ya kugundua mpenzi wake huyo ni muathirika alifadhaika sana lakini alijipiga moyo konde akiamini kuwa tayari nae kaukwaa tu kwani wana muda mrefu kwenye mahusiano na hajui mwenzake aliupata lini yaani kabla hawajaanza mahusiano au baada ya kuwa wapenzi.
Kweli alijijua tayari tu nae ni muathirika kwahiyo alikua anasubiri tu nayeye ajipange kwenda hospitali kuanza clinic. Baada ya kuongea hayo, alitoa cheti cha hospitali cha vipimo alivyofanya jana yake na kunipa.
Nilikipokea kilikua cha rangi ya kijani kikionyesha ni cha matibabu ya TB, niliendelea kusoma mpaka kwenye sehemu ya HIV status kama ni +ve au -ve, sikuamini nilichokiona kutokana na maelezo ya awali niliyopata toka kwa muhusika.
HIV status ilionyesha ni -ve!! Ilibidi nimuulize vizuri kilichoandikwa ni kweli ama amejijazia mwenyewe hiyo sehemu, akanambia nikionacho ndicho kilivyo hajaedit sehemu.
Nilijikuta natoka machozi sikujua ni ya furaha ama uchungu! Tulikumbatiana kwa kama dakika nzima. Ilikuwa ni siku ya utofauti sana kwangu kuwahi kuexpiriensi kitu kama hicho.
Ok, baada ya maelezo yooote hayo kilichonifanya kuleta jambo hili hapa ni kutaka kujua kitabibu mambo haya yanamekaaje kaaje maana mi kwa uelewa wangu najua asilimia ya mtu kuathirika akiwa na mpenzi alieathirika ni kubwa tena ikizingatiwa huyu jamaa yangu alikua ameshaanza kuishi nae japo si rasmi na yupo nae takribani mwaka tangu waanze kuishi pamoja mbali ya miaka mitatu ya mahusiano.
Nitumai ntapata darasa mujarabu, na pia itatusaidia wengi humu ambao labda tulikuwa na mitazamo au dhana potofu kuhusiana na huu ugonjwa, nawasilisha.