Ufafanuzi wa hili jambo, mimi limenishangaza kidogo.

Ufafanuzi wa hili jambo, mimi limenishangaza kidogo.

kidi kudi

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
2,450
Reaction score
2,013
Wasalaa wanajamvi.
Naomba nijielekeze kwenye mada moja kwa moja.

Nina rafiki yangu hivi karibuni miezi michache imepita aliniambia anafikiri ana tatizo la kifua baada ya kukohoa kohozi lenye damu.

Ukweli niliogopa kwani nilihisi haraka haraka atakua na TB hivyo nikamshauri akachek hospitali. Japo mwanzoni hilo la kwenda kupima alikuwa akilipotezea lakini siku moja alikubali na kuniomba nimsindikize hospital.

Tulienda na akaenda kupiga x- ray na kisha kupewa vikopo vya kuweka makohozi. Alipotoka kwa daktari nilibaini amekua mnyonge sana tofauti na nnavyomjua, hilo lilinipa mashaka kidogo japo sikumuonyesha.

Siku ilofuata tulirudi tena hospitali kufuatilia majibu ya makohozi, ndipo nilipomuona akitoka na daktari wakapelekana hadi clinic ya CTC. Kiukweli nilianza kupata majibu ya kwanini rafiki yangu huyu jana yake tulivoenda mara ya kwanza alikuwa na hali ya utofauti kidogo.

Niliendelea kumsuburi takribani saa zima kisha akaja huku machozi yakimtoka, akaja akanikumbatia kisha akaniambia twende nyumbani tukifika kuna jambo atanishirikisha kwavile mimi ni rafiki yake mkubwa( tangu sekondari A-level hadi university tumesoma wote tena kozi moja na bahati nzuri kazi tumepata sehemu moja).

Kweli jioni ya siku hiyo alinipigia simu tukaenda sehem moja tulivu akaagiza nyama choma na kisha tukaanza maongezi taratibu. Ndiposa akafunguka alichopanga kuniambia.

Aliniambia kwamba siku zote alikuwa anajisikia kuumwa kifua na kukohoa sana akajua fika tayari atakua na TB na ikibidi UKIWMI vilevile. Nkamuuliza kwanini, kweli alinipa jibu ambalo mpaka leo nikimuona rafiki yangu huyu nakubali kuna watu ni majasiri na wana mioyo mipana.

Aliniambia kuwa aliekua mpenzi wake ni muathirika [mpenzi wake amekua nae kwenye mahusiano takribani miaka 4 tangu tukiwa chuoni, na sasa hivi wamevunja uhusiano kwa sababu ambazo ni nje ya ishu ya ugonjwa.] na alijua kuwa ni muathirika mwaka mmoja uliopita.

Alinieleza pia baada ya kugundua mpenzi wake huyo ni muathirika alifadhaika sana lakini alijipiga moyo konde akiamini kuwa tayari nae kaukwaa tu kwani wana muda mrefu kwenye mahusiano na hajui mwenzake aliupata lini yaani kabla hawajaanza mahusiano au baada ya kuwa wapenzi.

Kweli alijijua tayari tu nae ni muathirika kwahiyo alikua anasubiri tu nayeye ajipange kwenda hospitali kuanza clinic. Baada ya kuongea hayo, alitoa cheti cha hospitali cha vipimo alivyofanya jana yake na kunipa.

Nilikipokea kilikua cha rangi ya kijani kikionyesha ni cha matibabu ya TB, niliendelea kusoma mpaka kwenye sehemu ya HIV status kama ni +ve au -ve, sikuamini nilichokiona kutokana na maelezo ya awali niliyopata toka kwa muhusika.

HIV status ilionyesha ni -ve!! Ilibidi nimuulize vizuri kilichoandikwa ni kweli ama amejijazia mwenyewe hiyo sehemu, akanambia nikionacho ndicho kilivyo hajaedit sehemu.

Nilijikuta natoka machozi sikujua ni ya furaha ama uchungu! Tulikumbatiana kwa kama dakika nzima. Ilikuwa ni siku ya utofauti sana kwangu kuwahi kuexpiriensi kitu kama hicho.

Ok, baada ya maelezo yooote hayo kilichonifanya kuleta jambo hili hapa ni kutaka kujua kitabibu mambo haya yanamekaaje kaaje maana mi kwa uelewa wangu najua asilimia ya mtu kuathirika akiwa na mpenzi alieathirika ni kubwa tena ikizingatiwa huyu jamaa yangu alikua ameshaanza kuishi nae japo si rasmi na yupo nae takribani mwaka tangu waanze kuishi pamoja mbali ya miaka mitatu ya mahusiano.

Nitumai ntapata darasa mujarabu, na pia itatusaidia wengi humu ambao labda tulikuwa na mitazamo au dhana potofu kuhusiana na huu ugonjwa, nawasilisha.
 
jamaa alikuwa anapiga kistarabu,Ukijifanya kusimamia kucha kwenye mtanange lazima uwake maana michubuko iko jirani

shida watu wanapiga ile maneno kama wanakomoa, piga tako zako taratiiiiiiibu hakuna shida
 
ukimwi unatisha, ila kansa ni funga kazi.....dah huyo jamaa ni jasiri sana, sasa baada ya kugundua bado yupo fresh, yeye anafikiria nini kwa sasa?
 
My sister is HIV +VE ila anaishi na jamaa yake ambaye ni -ve kwa muda mrefu tu. Na jamaa alikuja kujua kuwa sister ni +ve baada ya kumpa ujauzito na pale alipohitajika kuanza clinic tu ndio walimpa wakagundua yote hayo. Bahati nzuri mtoto mpaka leo yupo na wala hana maambukizi yoyote yale .
 
Aisee mimi kwa hili nililoshuhudia kwa huyu jamaa yangu, naamini kabisa Mungu hajaacha kuTenda miujiza yake hata sasa
 
jamaa alikuwa anapiga kistarabu,Ukijifanya kusimamia kucha kwenye mtanange lazima uwake maana michubuko iko jirani

shida watu wanapiga ile maneno kama wanakomoa, piga tako zako taratiiiiiiibu hakuna shida
nimejifunza kitu hapo
 
ukimwi unatisha, ila kansa ni funga kazi.....dah huyo jamaa ni jasiri sana, sasa baada ya kugundua bado yupo fresh, yeye anafikiria nini kwa sasa?
yupo tu ametafuta bebi mwingine ndo anafanya michakato avute ndani, jamaa ni jasiri sana pamoja na kumjua mtu wake amdathirika lakini hakuonyesha kupanic japo sisi marafiki zake tulikuwa tunamuona amekua tu mpoleee asiependa sana story tofauti na zamani, kumbe alikuwa na mzigo moyoni daaah!
 
Tofauti na kula kistaarabu.... Kingine kinachosaidia hua ni group la damu.......

Watu wenye group 0 baridi hua ni ngumu sana kuunyaka kama group nyingine za damu.
 
Tofauti na kula kistaarabu.... Kingine kinachosaidia hua ni group la damu.......

Watu wenye group 0 baridi hua ni ngumu sana kuunyaka kama group nyingine za damu.
huyu jamaangu ana blood group B+ sasa sijui nayo ina connection yoyote
 
kufanya mapenzi na mtu alieathirika sio kigezo cha moja kwa moja kwamba lazima na wewe utapata,,,,,, inategemea, namna mnavotayarishana kabla ya tendo(foreplay), pia inategemea umeenda mishindo mingapi pia kwa kila mshindo unatumia mda gani,,,,,
 
Swali lilikua ..ukifanya mapenzi na muathirika lazima upate maambukizi?

Jibu langu likawa hili

1.Mtu aliye na ARVs sio lazima ziwe zake au anazitumia labda kama umethibitisha hivyo kwa kupata na kadi yake ya CTC
2.Prostitutes wengi mjini wanatumia ARVs huku wakiwa hawana HIV.....hutumia kama Pre exposure prophylaxis(PrEP) yaani kujikinga na maambukizi kutoka kwa wateja wao..zinapatikana ktk black market
3.Kama ni kweli yeye ni muathirika wa HIV na anatumia hizo dawa vizuri basi huna sababu ya kuchanganyikiwa....
Reason and facts;
-Possibility ya kupata HIV kwa tendo moja ni 0.03%.
Possibility hii imesimama kwenye ground ya Viral Load(wingi wa virus ktk damu)
Kwa mgonjwa aliyetumia dawa vizuri bila kuchakachua anategemewa kuwa na Undectable level of virus....hii inamaanisha ukipima viral load unakuta 0 ingawa mgonjwa ana HIV.....Sasa mgonjwa mwenye undetectable level of virus au hata mwenye viral load ndogo uwezo wake wa kuambukiza unapungua sana na hivyo unaweza ukafanya "ngono peku"na usipate maambukizi..../Ushauri.....Usipanick....ukipima leo HIV ukaikuta basi sio ya huyo dada..ulikua nayo,Kama ukipima ukakuta Negative basi nenda kwa daktari na utapewa ARVs dozi ya siku 28 Post Exposure Prophylaxis na utasalimika....dawa hii huwa effective kama dozi ya kwanza itatumika ndani ya masaa 72 post event....

I hope utapata kitu katika jibu hili
 
Duh pole sana kwa rafiki yako Mungu yupo na ndie kila kitu kwetu. Hii ishu kwakwel ilinitokea Ila duh niliposikia story za mdada niliyekuwa nae mbona kulitokea mabadiliko ya ghafla Ila duh nikapiga moyo konde nikawa kwa kila baada ya kipindi hununua test na kujipima miez mitatu tofaut alhamdulillah Mungu kaniepusha nao. Mara ya mwisho nikawa dah mwili ukawa unauma nikasema wacha tu nikapanga day moja niende hospital baada ya kufika hospital nikatafuta dokta nikaongea nae pemben nikamwambia nataka nifanye chek up ya mwili wangu wote kabisa nikampelekea na mkojo achek kuwa hamna tatzo, akanitoa damu ya kutosha ya kufanyia vipimo vyake kwenye fundo LA mkono kwa mbele baada ya hapo akaniambia subir majibi yako nikaa kama roboo SAA hivi akaniita dah yaan majibu akanimabia huna tatzo lolote linalokusumbua kiafya na pia kwenye mkojo hakuona tatzo lolote Ila nikamuambia mbona mwili unaniuma sana ndio kuna dawa akaniandikia nikatafuta dispensary ikawa kila baada ya wiki ninaenda na kunipiga sindano lile tatzo lilipotea aalhamdulillah.
 
Tofauti na kula kistaarabu.... Kingine kinachosaidia hua ni group la damu.......

Watu wenye group 0 baridi hua ni ngumu sana kuunyaka kama group nyingine za damu.
Hakuna study yoyote hadi sasa iliyoonyesha uhusiano kati ya blood group na maambukizi....kuna watu wachache sana ambao hawaambukiziki...na hao wana mutation ya receptors ambazo ndio mlango wa HIV kuingia ktk seli za binadamu.....study ilifanyika Zambia na kuthibitisha hilo kwa baadhi ya prostitutes there
 
Swali lilikua ..ukifanya mapenzi na muathirika lazima upate maambukizi?

Jibu langu likawa hili

1.Mtu aliye na ARVs sio lazima ziwe zake au anazitumia labda kama umethibitisha hivyo kwa kupata na kadi yake ya CTC
2.Prostitutes wengi mjini wanatumia ARVs huku wakiwa hawana HIV.....hutumia kama Pre exposure prophylaxis(PrEP) yaani kujikinga na maambukizi kutoka kwa wateja wao..zinapatikana ktk black market
3.Kama ni kweli yeye ni muathirika wa HIV na anatumia hizo dawa vizuri basi huna sababu ya kuchanganyikiwa....
Reason and facts;
-Possibility ya kupata HIV kwa tendo moja ni 0.03%.
Possibility hii imesimama kwenye ground ya Viral Load(wingi wa virus ktk damu)
Kwa mgonjwa aliyetumia dawa vizuri bila kuchakachua anategemewa kuwa na Undectable level of virus....hii inamaanisha ukipima viral load unakuta 0 ingawa mgonjwa ana HIV.....Sasa mgonjwa mwenye undetectable level of virus au hata mwenye viral load ndogo uwezo wake wa kuambukiza unapungua sana na hivyo unaweza ukafanya "ngono peku"na usipate maambukizi..../Ushauri.....Usipanick....ukipima leo HIV ukaikuta basi sio ya huyo dada..ulikua nayo,Kama ukipima ukakuta Negative basi nenda kwa daktari na utapewa ARVs dozi ya siku 28 Post Exposure Prophylaxis na utasalimika....dawa hii huwa effective kama dozi ya kwanza itatumika ndani ya masaa 72 post event....

I hope utapata kitu katika jibu hili
Nashukuru kwa maelezo yako, japo jamaa alipiga dozi ya TB na ameimaliza, siku ya mwisho kurudi kuchukua dawa ya mwisho pia nilienda nae nakumbuka alipimwa tena HVI jibu likawa vilevile yaani -VE, kwasasa jamaa hataki kabisa kusikia habari za kumwambia akapime hahaaaa
 
Back
Top Bottom