PostGE2025 Ufafanuzi wa Serikali Kuhusu Kura ya Kamati za Bunge la Ulaya (EU) Dhidi ya Tanzania

PostGE2025 Ufafanuzi wa Serikali Kuhusu Kura ya Kamati za Bunge la Ulaya (EU) Dhidi ya Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wakuu,

Tumekuwa na mijadala na taarifa mbalimbali hapa JF na mitandao mingine kuhusu hatima ya ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU). Ili kuweka mambo sawa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetoa ufafanuzi rasmi kama inavyoonekana hapa:

View attachment 3600799

Kwa wanaopata changamoto ya kuisoma taarifa hiyo kwa kina, nimekuleteeni muhtasari wa mambo ya msingi yaliyofafanuliwa na Serikali:

1. Nini Hasa Kilitokea?​

  • Kamati ya Mambo ya Nje na Kamati ya Maendeleo za Bunge la Ulaya zimefanya kikao na kupiga kura kuhusu mapendekezo yanayohusiana na Mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo wa mwaka 2025 kati ya Tanzania na EU.
  • Katika kura hiyo ngazi ya kamati, mapendekezo yalipitishwa kwa kura 81 za kuunga mkono, kura 1 ya kupinga, na kura 4 za kutokuwa na msimamo.

2. Ufafanuzi wa Serikali (Mambo 3 ya Kuzingatia)​

Ili kuepuka 'taharuki', Wizara imefafanua kuwa haya sio maamuzi ya mwisho, na mchakato uko hivi:
  • Ni Hatua ya Awali: Kura hii imepigwa na Kamati mbili tu na ni sehemu ya taratibu za ndani za Bunge la Ulaya za kufanya maamuzi.
  • Mchakato Bado Haujakamilika: Mapendekezo haya lazima yapelekwe kwenye Kikao cha Bunge zima la Ulaya (lenye Wabunge zaidi ya 700) kwa ajili ya mjadala na uamuzi wa mwisho. Hivyo, kura ya kamati haiwakilishi msimamo wa mwisho wa Bunge zima la EU.
  • Mamlaka ya Kiutendaji yako kwa 'Tume ya Ulaya': Kama ilivyo kwenye mifumo mingi ya kibunge, maazimio ya Bunge hupelekwa kwenye chombo cha utendaji. Kwa upande wa EU, uhusiano na nchi washirika huendeshwa na Tume ya Ulaya (European Commission). Hivyo, mapendekezo hayo hayapaswi kutafsiriwa kuwa ndiyo uamuzi wa moja kwa moja unaobainisha mustakabali wa mahusiano.

3. Hali ya Mahusiano ya Tanzania na EU kwa Sasa​

  • Serikali inatoa hakikisho kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya unaendelea kuwa imara na unazidi kustawi.
  • Ushirikiano huu umejengwa kwa muda mrefu kupitia mazungumzo na kuheshimiana, na Serikali ina dhamira ya dhati ya kuendelea kuimarisha ushirikiano huu kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili.
Diplomasia ina michakato yake mirefu na kila taasisi (kama Bunge la Ulaya) ina uhuru wa kujadili na kutoa mapendekezo, lakini haimaanishi ndio mwisho wa ushirikiano. Suala hili bado lipo kwenye ngazi za taratibu za kawaida.

Nini maoni yako kuhusiana na tamko hili la Serikali ya Tanzania?
Sababu kuu ya kura kuwa nyingi za kuunga kunyimwa,ni matokeo ya 29 October 2025,Hivyo asilimia nyingi huenda tukanyimwa!
 
Kombo ni Waziri mzigo, mtapigwa Ban USA na EU, stay tuned.

Kuna Kombo na Kabudi ha watu ni bure, nyie hamna ubavu wa kushindana na mataifa hayo, uchumi wenyewe huu ambao hata Jamaa wa Facebook anatupita, achaneni kuua watu na mkaongee na upinzani mjinusuru, hizo tume mnajiundia kujifurahisha dunia inajua ni mchezo tu. Mmezoe kujipa matumaini hewa, mtakoma.
 
Walidhani hao ni gen z wanayoikoromea hapa kimewaramba. Wamechanganyikiwa hadi wameenda kuomba jamvi kilioni. Sasa urusi ni juzi tu imetoka vitani wana msaada gani huku kama sio kuchanganyikiwa. WHO ARE YOU?
 
Walidhani hao ni gen z wanayoikoromea hapa kimewaramba. Wamechanganyikiwa hadi wameenda kuomba jamvi kilioni. Sasa urusi ni juzi tu imetoka vitani wana msaada gani huku kama sio kuchanganyikiwa. WHO ARE YOU?
Kusaidiwa sio sifa.
 
Walidhani hao ni gen z wanayoikoromea hapa kimewaramba. Wamechanganyikiwa hadi wameenda kuomba jamvi kilioni. Sasa urusi ni juzi tu imetoka vitani wana msaada gani huku kama sio kuchanganyikiwa. WHO ARE YOU?
Vita Bado vinaendelea mkuu!
 
hata sio kuendelea ndo bado vimeanza hata mafisadi wanalijua hilo wamechanganyikiwa hadi wameenda kuomba jamvi kilioni. Nani hajui urusi ni juzi tu walikuwa na vita sa mtu kwenda huko kuomba misaada wakidanganya ni ziara, ziara gani.
Bado, vita vinaendelea mkuu!Urusi vs Ukraine.
 
Hawa huwa hawana utamuduni wa kunyoosha maelezo.

Mtu anayesoma hii press release bila kuwa ameshasikia kilichojiri huko Ulaya hawezi kuambulia chochote cha maana.

Hawataki kusema kwamba kura iliyopigwa ni ya kuinyima Tanzania msaada!
Kitu unachotamani zaidi,hapo nchimbi mkatoliki akiwa rais upinzani wote unatupa kapuni,kuku maji nyie!
 
Back
Top Bottom